Kesi ya kupinga matokeo Arusha mjini inaendelea

Nanyaro Ephata

JF-Expert Member
Jan 22, 2011
1,221
1,788
Wakuu
Kesi inaendelea tena leo,na shahidi wa nne Bwana Salim Mpemba ambaye alikuwa Katibu wa ccm wilaya anatoa ushahidi wake.
1.Wakili Mugwai.Wewe ni nani na nafasi yako
2.Shahidi.Mimi ni Salim Mpemba,katibu wa ccm wilaya ya Kyela,kabla ya kuhamia Kyela nilikuwa katibu hapa Arusha mjini,
3.wakili Mugwai.Je professional yako ni nini?
4.Shahidi.Mimi ni polisi,na niliazimwa na ccm mwaka 1984,hadi mfumo wa vyama vingi ulipoanza ambapo nilichagua kubaki ndani ya chama,na nimetumika kama Katibu wa wilaya
5.Wakilu Mugwai.Je unakumbuka mwaka 2010 kulikuwa na uchaguzi
6.Shahidi.Ndio nakumbuka
7.Wakili Mugwai.Nani alikuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya chama chako?
8.Shahidi.Dr Batilda Burian
9.wakili Mugwai.Nani alikuwa msimamizi mkuu wa uchaguzi?
10.Shahidi.Mkurugenzi wa manispaa ya Arusha,ambaye namfahamu kwa jina moja la Bwana Changa.
11.Wakili Mugwai.Msimamizi wa uchaguzi aliwapa maelekezo yoyote?
12.Shahidi.Ndio,alitutaka vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi,kupeleka ratiba za mikutano ya hadhara,ikionyesha,mahali,tarehe,na muda,na mimi nikamtuma Katibu mwenezi wa wilaya Bwana Semy Kiondo,kupeleka ratiba hiyo.
 
Mods,naomba uinganishe hii na ile thread ingine.
Wakili.Je mliwahi kukaa vyama vyote vilivyoshiriki uchaguzi kupanga ratiba?
2.Shahidi.Ndio tulikaa 2.8.2010,vyama vyote chini ya uenyekiti wa Msimamizi wa uchaguzi,tukapanga ratiba na tulikubaliana vyama vyote.
3.Wakili Mugwai.Mbali na hayo,je kuna maelekezo mengine mlipewa na msimamizi wa uchaguzi?
4.Shahidi.Baada ya kikao tuliletea vitabu vya maadili ya uchaguzi,ambavyo nililetewa na na Bwana Mbunda,tarehe sikumbuki,ila vitabu vilikuwa vitatu
 
ya doing good job Nanyaro, maximum respect. keep news coming
 
Jaji anapitia vifungu vya kisheria,baada ya wakili mgwai,kuomba kuwasilisha ratiba ya mikutano kama kielelezo namba moja,na wakili wa serikali kupinga kwa madai kuwa ni fotocopi,hivyo kumtaka shahidi aileze mahakama wapi nakala halisi zilipo.Baada ya uchambuzi wa kisheria mahakama imepokea ratiba hii kama kielelezo cha awali
 
Wakili: Mbunge wako wa Arusha Mjini unamjua?
Shahidi: Simjui kwakuwa hatokani na chama changu cha magamba

Just joking Wakuu........Kamanda Nanyaro tuhabarishe zaidi
 
1.Wakili Mugwai.Uliwahi kuhudhuria mkutano wowote wa CHADEMA wakati wa kampeni?
2.Shahidi.Sikuwahi kuhudhuria mkutano wowote wa CHADEMA,bali nilihudhuria mikutano ya chama changu cha ccm pekee
3.Wakili Mugwai.Je unafahamu kama aliyekuwa mgombea wa chama chako,Dr Batilda aliwahi kuhudhuria mkutano wa CHADEMA?
4.Shahidi.Sifahamu
5.Wakili Mugwai.Je ulikuwa unamfahamu Bwana Lema Kabla ya kampeni?
6.Shahidi.Hapana nimemfahamu wakati wa kampeni
 
1.Wakili Mugwai.Je kampeni zilianza rasmi lini?
2.Shahidi.Tarehe 21.8.2010 na kuisha 30.10.2010
3.Wakili Mugwai.Je uchaguzi ulifanyika lini
4.Shahidi.31.10.2010
5.Wakili Mugwai.Matokeo yalitangazwa lini?na nani alitangazwa mshindi?
6.Shahidi,matokeo yalitangazwa Tarehe 1.11.2010؛‎ na mshindi ni bwana Lema
7.Wakili Mugwai,ambaye huyo bwana Lema ni nani?
8.Shahidi.Mbunge
9.Wakili Mugwai,Shahidi eleza mahakama vizuri,lazima Lema ana jina linaloanza,huwezi kusema Bwana Lema tu
10.Shahidi.Mheshimiwa Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema
 
Tunashukuru Mkuu kwa kutupa updates kutoka mahamakani.

Kuwa fair mkuu kwenye kuripoti upande wa pili usiripoti nagative!
 
Anajibu kipolisi polisi sana. Ila sina hakika kama kasema chama chakke cha 'magamba'
 
Tunasubiri huyu shahidi atuambie kwamba alimsikia Lema akimtukana Buriani kwenye kampeni wakati ameshasema hajahudhuria kampeni hata moja ya CHADEMA
 
  • Thanks
Reactions: FJM
1.Wakili Mugwai.Je kampeni zilianza rasmi lini?
2.Shahidi.Tarehe 21.8.2010 na kuisha 30.10.2010
3.Wakili Mugwai.Je uchaguzi ulifanyika lini
4.Shahidi.31.10.2010
5.Wakili Mugwai.Matokeo yalitangazwa lini?na nani alitangazwa mshindi?
6.Shahidi,matokeo yalitangazwa Tarehe 1.11.2010؛‎ na mshindi ni bwana Lema
7.Wakili Mugwai,ambaye huyo bwana Lema ni nani?
8.Shahidi.Mbunge
9.Wakili Mugwai,Shahidi eleza mahakama vizuri,lazima Lema ana jina linaloanza,huwezi kusema Bwana Lema tu
10.Shahidi.Mheshimiwa Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema[/QUOTE]

kumbe anantambua analeta jeuri harooooooooooooooooooo utachezea mbata
 
Kwa nyongeza:shahidi anaitwa salum mpamba na si Mpemba aliondolewa na CCM wakati wa uchaguzi baada ya kudaiwa kufanya kazi nyumbani kwa batilda badala ya ofisi za chama na pia kuwatenga viongozi wote wa juu wa wilaya ya Arusha katika timu ya kampeni ya Batilda na baada ya kushindwa uchaguzi chama kikamwadabidha kwa kumhamisha Kyela well done Nanyaro!
 
Back
Top Bottom