Kesi ya kamanda Lema Arusha

John W. Mlacha

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
3,504
1,341
Huyu Millya hakuhusika kuleta fitna kwenye hii kesi? nauliza tu nataka nipate jibu...kama hujui usiharibu hali ya hewa
 
Alihusika sana sababu alikuwa kati ya makada wa CCM waliokuwa wanahudhuria mahakamani kwa mbwembwe sasa ni muda muafaka atueleze hela za kumuhonga JAJI zilitoka kwa nani.
 
Kitu nawapongeza chadema ni kukataa kumpa cheo chochote na kumnyima asigombee ubunge wa Arusha.
 
Hivi huyu Millya, haiwezi kuwa njama ya kutaka kuwania Ubunge Arusha lakini kwa mgongo wa yule Mzee ambaye anatajwa tajwa sana ?
 
Tunataka akampige chini yule mpuuzi wa Simanjiro.
Arusha ataisikilizia kwenye bomba tu.
 
Alihusika sana sababu alikuwa kati ya makada wa CCM waliokuwa wanahudhuria mahakamani kwa mbwembwe sasa ni muda muafaka atueleze hela za kumuhonga JAJI zilitoka kwa nani.
Una ushahidi na unayo yasema....umoja wa vijana haukujihusisha na saga hili mkuu na hata wakina benno walipokuja sijui kamailikuwa unafiki ama la walisema aachwe mbunge afanye kazi zake....
 
Mbunge mteule wa Simanjiro Mhe James Millya.Waooooooooo.....!!!!!!
 
Una ushahidi na unayo yasema....umoja wa vijana haukujihusisha na saga hili mkuu na hata wakina benno walipokuja sijui kamailikuwa unafiki ama la walisema aachwe mbunge afanye kazi zake....

mkuu Crashwilse tufumbue macho basi kidogo..au unamtetea kwa vile ameshaingia ndani? hatujui kuwa ana nini moyoni.
 
Siasa kweli sihasa. UVCCM inapokuwa nzuri kuliko CCM!
 
Huu usije ukawa mtego kwani January Makamba aliwahi kuandika katika mtandao wa Twitter kuwa dawa ya Arusha iko Jikoni!

My take:- CHADEMA tuwe makini
 
Una ushahidi na unayo yasema....umoja wa vijana haukujihusisha na saga hili mkuu na hata wakina benno walipokuja sijui kamailikuwa unafiki ama la walisema aachwe mbunge afanye kazi zake....

Mkuu si wewe ndio ulituambia humu JF kuwa Millya hana lolote anapewa hifadhi na mama wa kizungu...kweli kwenye siasa hakuna adui wa kudumu wala rafiki wa kudumu.
 
Mimi huwa siandiki habari za kipumbavu kama hizo labda utakuwa umesahu aliandika Kiwte.....
 
mkuu Crashwilse tufumbue macho basi kidogo..au unamtetea kwa vile ameshaingia ndani? hatujui kuwa ana nini moyoni.
Siwezi kujua ya moyoni mwake lakini kitambo alishaonyesha nia ingawa sikujua kama ilikuwa ni kwa masilahi yake na kambi yake na Lowasa au msimamo wake kama yeye....
 
hata Rosatam Aziz waliekuwa wakimtukana kila siku, akiamua kujiunga chadema leo, basi atakuwa jembe. chadema kweli wanashughuli. inakuwaje mtu huyo huyo mumuite mchafu akija kwenu bila ya kubadilika lolote awe msafi ?
 
Mabadiliko ya mtu yapo moyoni. Kama unategemea Millya abadilike ngozi awe mweupe ili uamini kwamba amekuwa msafi hilo ni juu yako. Mimi binafsi naamini kwamba ubaya wa CCM si kutokana na watu wenyewe bali hilo lichama lenyewe tu lilivyokaa kimfumo hata ukiwa mzuri vipi itabidi uwe fisadi, mwongo, mnafiki ili uweze kusurvive ndani ya chama.

Millya anaweza kuwa ameamua kuanza maisha mapya ndani ya chama kipya. Ya kale yamepita tazama yote yamekuwa mapya. Kwangu mimi hata Lowassa akiamua kuhamia Chadema poa tu, ali mradi afahamu kuwa ethics na standards za chadema ni za juu sana na kwa mtu kama yeye zahitaji badiliko la kweli la moyoni.
 
Back
Top Bottom