1) Mahakama ina wajibu na ulazima wa kuhakikisha kama huyo mtoto kweli ni wa mdaiwa/mshitakiwa re Mahita. Hivyo mahakama inapaswa kutoa amri mdaiwa akapimwe ikiwa mdaiwa anakataa kupima i.e. dna test.
Katika kesi kama hii ambapo mtuhumiwa kwa kiburi anakataa kuchukua DNA test, mahakama imeonyesha woga katika kutoa haki. Ilitakiwa itoe amri na kama Mahita angekaidi, alistahili adhabu kali kwa kitendo chake cha kudharau mahakama. Hapa bado ana mwanya wa kukata rufaa kwa kisingizio cha kukosekana ushahidi wa DNA kuwa yeye ndiye baba halisi.
1)ama hukumu ndiyo hiyo iliyotolewa, basi mahakama iliridhika na matokeo ya test iliyofanyika.
Mahakama imefanya kosa kubwa ama kwa makusudi ya kumnusuru Mahita au kwa woga kutokana na shinikizo zilizo nje ya uwezo wake.
1)Tusisahau kwamba katika kesi zinazowahusisha watu wenye public profile kama Mahita, details nyingi za kesi hiyo nazo kwa kiasi kukubwa zinakuwa kwenye public eye; nyingine huwa ni za aibu kwani zilifanywa faragha - sasa zinakuwa public - kinyume na hulka na staha ya binadamu.
Hii yawezekana Tanzania tu na inatokana na ama mapungufu ya sheria au Hakimu kutokuwa makini. Kosa ni kosa na binadamu wote wanatakiwa kuwa sawa mbele ya sheria. Mahita alipombaka mfanya kazi wake wa ndani alijua vema anafanya nini - kama kuna heshima yoyote aliyokuwa nayo kwenye Jamii, aliivua kwa kitendo chake hicho. Hahitaji huruma ya mtu yeyote.
1)Sasa pointi ni kwamba mshitakiwa ana familia - mke, watoto, wazazi, ndugu - ambao wote ghafla wanalazimika kushuhudia mambo aliyofanya baba/mume yao/wao hadharani. Moyo wangu unalenga watoto wake na mke wake, ambao katika scenario hii wanakuwa "collateral damage" ya vyombo vya habari.
Toka hii kesi imeanza sijasikia wakitajwa hao watoto wake wala huyo mke wake. Hawa ni watu wazima na walitakiwa wampe ushauri baba yao tangu awali lakini kwa kuwa inaonekana walikuwa upande wa huyu mbakaji, hizo unazoita "collateral damage" kwa sasa ni halai yao. Kama kesi ingeamuliwa vinginevyo hawa hawa wangegonganisha glasi wakishangilia na kumlaani malalamikaji.
1)Kwa kweli katika compassionate society hawa watu wanapaswa kufikiriwa re suffering ambayo wata-go through katika hii sakata yote hadi itakapokwisha.
Ni mhalifu gani hana ndugu na marafiki - wauaji, wabakaji, wezi, mafisadi wote wana ndugu na jamaa wanaosononeka. Je, ni haki kuacha sheria kuchukua mkondo wake eti kwa sababu ya kufikiria the so called suffering ya ndugu. Je, ndugu wa victim, wao unawaweka wapi ?
1)Tusisahau pia kwamba kuna ki-changa ambacho wakati huu wote huenda kinapata shida; japokuwa hii ni regrettable & unnecessary na imesababishwa na pig-headed behaviour ya mshitakiwa/mdaiwa.
Hapa tuko pamoja, tukifikirie hiki kichanga na shida kinachopata kuanzia ya kimwili na kisaikolojia kwa kukataliwa na baba yake mzazi. Kwa Mahita, aliyekuwa na jukumu la kulinda usalama wa raia, kuwa kinara wa uvunjaji wa sheria kunahitajika adhabu kali kama fundisho kwa wote wanaokabidhiwa nyadhifa kama hizo - hapa hakuna cha kumwamgalia nyani uso.
1)Ninachotaka kusema ni kwamba, tujaribu kujenga jamii yenye compassion, inayofikiria na kujali victims halisi i.e. watoto na mama/baba katika kesi za namna hii.
Hapa utakwaa kisiki kwa sababu victim wa kwanza ni huyo binti mdogo ambaye katika kutafuta ajira nyumbani kwa IGP aliishia mikononi mwa mbakaji. Na Mahita bila haya yoyote, baada ya kumpachika mimba akaamua si tu kumtelekeza bali pia kumdhalilisha kwa kutumia kofia yake ya Ukuu wa polisi. Victim wa pili ni Juma Mahita ambaye haukuwa uchaguzi wake kukuzaliwa na nani na kwa wakati gani - Omari Mahita panapomfaa ni Keko.