Kesi ya IGP Mahita na tuhuma za kuzaa na mtumishi wake wa ndani

1) Mahakama ina wajibu na ulazima wa kuhakikisha kama huyo mtoto kweli ni wa mdaiwa/mshitakiwa re Mahita. Hivyo mahakama inapaswa kutoa amri mdaiwa akapimwe ikiwa mdaiwa anakataa kupima i.e. dna test.

Katika kesi kama hii ambapo mtuhumiwa kwa kiburi anakataa kuchukua DNA test, mahakama imeonyesha woga katika kutoa haki. Ilitakiwa itoe amri na kama Mahita angekaidi, alistahili adhabu kali kwa kitendo chake cha kudharau mahakama. Hapa bado ana mwanya wa kukata rufaa kwa kisingizio cha kukosekana ushahidi wa DNA kuwa yeye ndiye baba halisi.

1)ama hukumu ndiyo hiyo iliyotolewa, basi mahakama iliridhika na matokeo ya test iliyofanyika.

Mahakama imefanya kosa kubwa ama kwa makusudi ya kumnusuru Mahita au kwa woga kutokana na shinikizo zilizo nje ya uwezo wake.

1)Tusisahau kwamba katika kesi zinazowahusisha watu wenye public profile kama Mahita, details nyingi za kesi hiyo nazo kwa kiasi kukubwa zinakuwa kwenye public eye; nyingine huwa ni za aibu kwani zilifanywa faragha - sasa zinakuwa public - kinyume na hulka na staha ya binadamu.

Hii yawezekana Tanzania tu na inatokana na ama mapungufu ya sheria au Hakimu kutokuwa makini. Kosa ni kosa na binadamu wote wanatakiwa kuwa sawa mbele ya sheria. Mahita alipombaka mfanya kazi wake wa ndani alijua vema anafanya nini - kama kuna heshima yoyote aliyokuwa nayo kwenye Jamii, aliivua kwa kitendo chake hicho. Hahitaji huruma ya mtu yeyote.

1)Sasa pointi ni kwamba mshitakiwa ana familia - mke, watoto, wazazi, ndugu - ambao wote ghafla wanalazimika kushuhudia mambo aliyofanya baba/mume yao/wao hadharani. Moyo wangu unalenga watoto wake na mke wake, ambao katika scenario hii wanakuwa "collateral damage" ya vyombo vya habari.

Toka hii kesi imeanza sijasikia wakitajwa hao watoto wake wala huyo mke wake. Hawa ni watu wazima na walitakiwa wampe ushauri baba yao tangu awali lakini kwa kuwa inaonekana walikuwa upande wa huyu mbakaji, hizo unazoita "collateral damage" kwa sasa ni halai yao. Kama kesi ingeamuliwa vinginevyo hawa hawa wangegonganisha glasi wakishangilia na kumlaani malalamikaji.

1)Kwa kweli katika compassionate society hawa watu wanapaswa kufikiriwa re suffering ambayo wata-go through katika hii sakata yote hadi itakapokwisha.

Ni mhalifu gani hana ndugu na marafiki - wauaji, wabakaji, wezi, mafisadi wote wana ndugu na jamaa wanaosononeka. Je, ni haki kuacha sheria kuchukua mkondo wake eti kwa sababu ya kufikiria the so called suffering ya ndugu. Je, ndugu wa victim, wao unawaweka wapi ?
1)Tusisahau pia kwamba kuna ki-changa ambacho wakati huu wote huenda kinapata shida; japokuwa hii ni regrettable & unnecessary na imesababishwa na pig-headed behaviour ya mshitakiwa/mdaiwa.

Hapa tuko pamoja, tukifikirie hiki kichanga na shida kinachopata kuanzia ya kimwili na kisaikolojia kwa kukataliwa na baba yake mzazi. Kwa Mahita, aliyekuwa na jukumu la kulinda usalama wa raia, kuwa kinara wa uvunjaji wa sheria kunahitajika adhabu kali kama fundisho kwa wote wanaokabidhiwa nyadhifa kama hizo - hapa hakuna cha kumwamgalia nyani uso.

1)Ninachotaka kusema ni kwamba, tujaribu kujenga jamii yenye compassion, inayofikiria na kujali victims halisi i.e. watoto na mama/baba katika kesi za namna hii.

Hapa utakwaa kisiki kwa sababu victim wa kwanza ni huyo binti mdogo ambaye katika kutafuta ajira nyumbani kwa IGP aliishia mikononi mwa mbakaji. Na Mahita bila haya yoyote, baada ya kumpachika mimba akaamua si tu kumtelekeza bali pia kumdhalilisha kwa kutumia kofia yake ya Ukuu wa polisi. Victim wa pili ni Juma Mahita ambaye haukuwa uchaguzi wake kukuzaliwa na nani na kwa wakati gani - Omari Mahita panapomfaa ni Keko.
 
Very nice cause the law is standing in the right side.Absolutely Mahita is the responsible one.And that is an example to those who run after problems.I real impressed by that news.I advise for parents to show good care to their children
 
Nadhani jamaa alitegemea kutumia ujiko wake kuzima hiyo kesi. Hana maana kabisa na amejidhalilisha. Angekuwa mjanja angechomoa kesi mapema na kumaliza kila kitu uani. Sasa ameanika mchele barazani na ndege wako kibao. Mahakama zetu nazo zinatia huruma. Ilikuwaje akakataa kufanya paternity test? Napandwa na hasira hadi natamani niende nikampime mwenyewe!:mad:

Mkuu hii ni case ya madai, Civil case. Sasa kama ingekuwa criminal mahakama ingemlazimisha ila kwa kuwa ni kesi ya madai alikuwa na hiyari.

Ila Mahakama pia inaweza kutoa amri ya kutaka akapimwe bila kujali ni kesi gani. sema ndiyo hivyo tena penye udhia...
 
Very nice cause the law is standing in the right side.Absolutely Mahita is the responsible one.And that is an example to those who run after problems.I real impressed by that news.I advise for parents to show good care to their children

Naomba nijuzwe vizuri.... wazazi gani wanaitwa kuonyesha malezi bora ya watoto..kesi ya Mahita kutembea na hausgeil ambaye hakuwa mtoto bali mtu mzima...hapo wazazi na malezi vinahusuje?
 
1. Amhakikishie elimu katika shule na vyuo vinavyotambulika. Kipimo kiwe shule walizosoma wanawe wengine na uwezo alionao sasa hivi.
2. Amgharamie malipo yote ya tiba hadi hapo atakapokuwa mtu mzima.
3. Amhakikishie makazi yenye hadhi anayostahili.
4. Malipo yake kwa mwezi yahakikishe kuwa anaweza kupata mavazi, chakula na usafiri wa hakika na wa hadhi anayostahili.

Kama Mahita atafariki, huduma hizi aendelee kupata kutoka katika urithi wa baba yake.

Hako ka laki moja ni pesa ya peremende na big G !

Amandla........
 
1. Amhakikishie elimu katika shule na vyuo vinavyotambulika. Kipimo kiwe shule walizosoma wanawe wengine na uwezo alionao sasa hivi.
2. Amgharamie malipo yote ya tiba hadi hapo atakapokuwa mtu mzima.
3. Amhakikishie makazi yenye hadhi anayostahili.
4. Malipo yake kwa mwezi yahakikishe kuwa anaweza kupata mavazi, chakula na usafiri wa hakika na wa hadhi anayostahili.

Kama Mahita atafariki, huduma hizi aendelee kupata kutoka katika urithi wa baba yake.

Hako ka laki moja ni pesa ya peremende na big G !

Amandla........


Huyu ni mstaafu..hana pesa hata ya kulipia kipimo cha DNA -
 
Mtoto wa zinaa astahiki hata kidogo kupata urithi. Hilo ni jukumu la mama yake kumlea na kumtunza.

mama amejidhalilisha na amethalilisha mtoto wake. sasa sijui kama mtoto ataweza kusoma. unajuwa atakuwa ame athirika kisaikolojia kuhusu kadhia nzima.
 
Mtoto wa zinaa astahiki hata kidogo kupata urithi. Hilo ni jukumu la mama yake kumlea na kumtunza.

mama amejidhalilisha na amethalilisha mtoto wake. sasa sijui kama mtoto ataweza kusoma. unajuwa atakuwa ame athirika kisaikolojia kuhusu kadhia nzima.
huyu nae ni walewale,mzee we unao wangapi huko mtaani?maana naona umekurupuka kusikia urithi,matunzo,malezi unamtetea mahita tuambie bwana
 
Mtoto wa zinaa astahiki hata kidogo kupata urithi. Hilo ni jukumu la mama yake kumlea na kumtunza.

mama amejidhalilisha na amethalilisha mtoto wake. sasa sijui kama mtoto ataweza kusoma. unajuwa atakuwa ame athirika kisaikolojia kuhusu kadhia nzima.

Halafu watu kama nyie ndio mnakuwa mahakimu kwenye Mahakama ya Kadhi! Kama hukumu ndivyo zitakavyokuwa basi heri wanaowapinga. Hiyo zinaa alifanya mama peke yake kwa hiyo ni yeye peke yake ndie atakaewajibika? Na mtoto akitokea kuwa kama Obama ndipo mnapoanza kujishaua! Iko kazi.

Amandla.......
 
Mtoto wa zinaa astahiki hata kidogo kupata urithi. Hilo ni jukumu la mama yake kumlea na kumtunza.

mama amejidhalilisha na amethalilisha mtoto wake. sasa sijui kama mtoto ataweza kusoma. unajuwa atakuwa ame athirika kisaikolojia kuhusu kadhia nzima.

Sikutegemea this low attitude kwa mtu kama wewe!!! Huyo mama alitiwa na mbuzi??? Tena akiwa mjakazi asiye na sauti wala elimu??? Na siajabu hata mshahara alikuwa hapewi.... Inatia uchungu na aibu saana kusikia hivi wakati sisi wanaume tunachangia haya matatizo na kuropoka kwamba at "mtoto wa zinaa hastahiki hata kidogo kupata urithi" kwani hukumu imezungumzia urithi au matunzo!!?????

Mtoto ambaye hana hatia wala uwezo wa kuamua atokee kwe tumbo lipi la uzazi halafu uasema haya??? Halafu hapohapo unakiri kwamba atakuwa ameathirika kisaikolojia... watu kama wewe si ndio mtaathari kubwa zaidi??........

Ni mungu gani huyo unayemuamini???

Mtoto huyu anahitaji na anastahili haki zote kama mtoto wa Mahita!!

Aaaaaaaaaaahhhhhggggggggghhhhhhhhhhrrrrrrrrrrrr
 
Mtoto wa zinaa astahiki hata kidogo kupata urithi. Hilo ni jukumu la mama yake kumlea na kumtunza.

mama amejidhalilisha na amethalilisha mtoto wake. sasa sijui kama mtoto ataweza kusoma. unajuwa atakuwa ame athirika kisaikolojia kuhusu kadhia nzima.

Shetani siyo lazima atishe, wewe ndiye kiongozi wa mashetani umetupwa duniani na dhambi zako, amehalalisha ubakaji na kuzikana roho zisizo na hatia duniani, eti Mtoto wa zinaa astahiki hata kidogo kupata urithi:rolleyes:.. Ni nani alizini? Kama mzinifu basi ni Mahita, kwa sababu anaye mke na bado akamwingilia binti asiyejua lolote, pengine na kwa kumtishia kumfukuza kazi.

Hayo ndo matunda ya uzinifu wa Mahita, wacha avune alichopanda. Huyo ni mmoja tu, wapo wengi waliotendwa na haki zao hazijapatikana. Angalia wewe kaka usijekuwa kuni huko ahera.

Mmehalarisha ubakaji huko mnakoabudu, na mnahalalisha kutoyatambua matokeo ya ubakaji. Kweli wewe na waaminio hayo mmeletwa duniani kuhatibu taratibu za Mungu.

Mwenyezi Mungu atazipigania roho zinazonyanyaswa bila hatia.

Namwomba Mungu akusamehe bureeeee!! sijui ulizaliwa wewe!! maana kama ulizaliwa na mwanamke, ukapewa matunzo na wazazi wako, elimu n.k, na kama wewe ni mzazi katu usingeyaandika haya uliyoyaweka hapa. Umeenika udhaifu wako. Pole sana.

Halafu wewe utakuwa wa kwanza kuilaumu serikali kwamba haiwajali watoto wa mitaani, na hali wewe ndo unaongeza idadi ya hao watoto mitaani.

Nitarudi baadaye kukupa vipande vyako zaidi. Huna haya hata kidogo.


 
Ndugu yangu H. M. Hafif (i am sorely tempted to abuse my privileges here and make fun of your name!), but i will just say that i condemn your stand in the strongest manner possible re: "mtoto wa zinaa hastahiki hata kidogo kupata urithi". umepata wapi mawazo ya kikatili, kinyama, kutojali namna hii!!?? hebu jiulize naujibu swali mwenyewe - huyo mtoto ana makosa gani mpaka apate hiyo adhabu unayopendelea kumpa? na huyo jamaa (ji-baba) aliyemtia mimba kijana wa kazi na yeye unampa nafasi ya kufanya ubaya huo na aende scott free!!??

kule stone age ulikotoka, tafadhali rudi hukohuko haraka.
 
Hayo ni matunda ya uongozi wa JMK, bado hatuyaoni?

Uhuru wa mahakama ni kitu cha kuvutia sana. Sijui JK ame-play part kiasi gani kufikia hapa. Mimi nadhani ni ma-judge wenyewe wameamua kuheshimu kazi yao na kuipa sifa inayotakiwa. Lakini papo hapo, unaweza ku-argue kuwa wana back-up ya JK.
 
Mahita(1).jpg

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (mstaafu), Omary Mahita.



Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (mstaafu), Omary Mahita, kupitia wakili wake, Charles Semigalawa, amesema kwamba anakusudia kukata rufaa kupinga uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam kumtaka atoe Sh. 100,000 kila mwezi kwa ajili ya matunzo ya mtoto Omary Mahita kwa maelezo kuwa ni baba halali wa mtoto huyo.
Akizungumza na Nipashe ofisini kwake, wakili Semigalawa alisema kuwa Mahita hakuridhishwa na uamuzi huo hivyo anakusudia kukata rufaa.
Semigalawa alisema Mahita hakuwahi kujua kama amezaa mtoto na mwanamke anayeitwa Rehema Shabani lakini alijitokeza baada ya miaka 10 kupita na alimburuza mahakamani moja kwa moja bila kufanya naye mazungumzo yoyote.
"Bado sijajua ni lini na mahakama gani lakini mteja wangu hakuridhika na kwamba tutakata rufaa kupinga uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Kinondoni dhidi yake (Mahita)," alisema Semigalawa.
­Mapema Septemba 10, mwaka huu, Hakimu Mkazi Susan Kihawa alitoa amri kuwa Mahita amtunze mtoto huyo kwa kulipa fedha hizo kila mwezi hadi atakapofikisha umri wa kujitegemea.

CHANZO: NIPASHE
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom