Kesi ya Gwajima yaahirishwa mpaka Julai 14, 2025

Kesi ya Gwajima yaahirishwa mpaka Julai 14, 2025

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,603
Reaction score
22,717
Shauri lilofunguliwa na Bodi ya Wadhamini la kanisa la Glory of Christ Tanzania Church maarufu kwa jina la kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima limeahirishwa kusikilizwa leo Julai 11, 2025 mpaka tena Julai 14, 2025.

Bodi ya Wadhamini inaiomba Mahakama kutupilia mbali zuio la kanisa hilo kuendesha shughuli zake za kidini. Toka shauri hilo lilivyofikishwa Mahakamani mbele ya Jaji Juliana Masabo kikwazo kikubwa kilichojitokeza ni barua husika ya kufuta usajili.

Ambapo barua iliyowasilishwa Mahakamani kutoka kwa msajili ilikuwa na jina la Glory of Christ Church badala ya jina Glory of Christ Tanzania Church, jambo ambalo hata mawakili wa serikali waliita barua hiyo uzushi na haipo.Hata hivyo Wakili wa Kanisa hilo, Wakili Peter Kibatala aliweza kuwasilisha vielelezo vipya, na shauri hilo kupangiwa kusikilizwa leo.

Hata hivyo shauri limeahirishwa mpaka siku ya Jumatatu Julai 14, 2025, saa nane kamili mchana. Akiongea kwa njia ya simu wakili Kibatala amesema hiyo imetokana na mwingiliano wa shughuli mbalimbali za kimahakama.

“Maana imeonekana ni busara iahirishwe mpaka Jumatatu ambapo mambo mengine yataendelea kuhusiana na shauri hilo,” amesema Kibatala. Ikumbukuwe pia, kesi hiyo ilipaswa kusikilizwa Julai 8, 2025 na haikusikilizwa, huku wakili Kibatala akisema utaratibu huo ni wa kawaida.

“Kwa hiyo kama nilivyosema tulipata taarifa na tukawafahamisha wateja wetu na sisi wenyewe tukachukua hatua za ziada. Kwa hiyo tutaendelea tena hiyo tarehe 14 mwezi wa saba kama nilivyosema,” aliongeza Kibatala.
 
Hivi ndiyo Shetani anafanya kazi zake, anakupiga kitu kupitia Wachawi, utaenda Kwa Mganga atakupa Unga mkaa ukanywe week 2, ukimaliza unaenda Tena Kwa Mganga, unapewa Maji ya mwarobaini ukanywe week 2.

Baadaye anakupiga na kitu kingine, unatafuta Tena Mganga mwingine, ukienda anakuchanja Kwa majivu, anakupa sawa utumie Kisha urudi baada ya week mbili.

Watawala wamejifunza wapi mbinu hizi.
 
Back
Top Bottom