Kesi ya dawa za Kulevya: Mwintanga aachiwa huru

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Sep 7, 2011
3,295
2,500
Ni baada ya miaka minne tangu akamatwe kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevwa akishirikiana na mabondia wa timu ya taifa waliokamatwa huko Mauritius.

Mahakama ya Kisutu leo imemuachia huru Alhaj Salum Mwintanga kwa kukosekana ushahidi wa dhati katika kesi hii.

Ni pigo kwa serikali kutokana na udhaifu wa wanasheria wake au ndio namna watanzania wengi wanavyoonewa kwa kubambikiziwa kesi?

Just thinking aloud
 
Aisee bora.

Huyu jamaa nilimuonea huruma sana kipindi kile alipokamatwa.

Sasa inabidi arudi kwenye cheo chake, maana aliwezesha kufanikisha vema maendeleo ya mchezo wa kupigana.
 
Whaaat?? Hivi wale mabondia wenyewe walisharudishwa Bongo? Au serikali ilikua inatumia ushahidi gani? Manaake kesi nyingine wanafanya makusudi kushindwa halafu wanapiga mlungula kwa mshtakiwa
 
Sumaye kishasema CCM na Serikali kuna Rushwa, sasa tunategemea nini kutoka kwa wazungu wa unga.

@POMPO unataka kusema jamaa katoa rushwa? sidhani mkuu ukisema udhaifu wa wanasheria wa serikali nitakubaliana nawe
 
Whaaat?? Hivi wale mabondia wenyewe walisharudishwa Bongo? Au serikali ilikua inatumia ushahidi gani? Manaake kesi nyingine wanafanya makusudi kushindwa halafu wanapiga mlungula kwa mshtakiwa

mabondia bado wanashikiliwa kule kule Mauritius mkuu
 
Aisee bora.

Huyu jamaa nilimuonea huruma sana kipindi kile alipokamatwa.

Sasa inabidi arudi kwenye cheo chake, maana aliwezesha kufanikisha vema maendeleo ya mchezo wa kupigana.

sidhani kama ana hamu tena na uongozi wa ndondi
 
Ni baada ya miaka minne tangu akamatwe kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevwa akishirikiana na mabondia wa timu ya taifa waliokamatwa huko Mauritius.

Mahakama ya Kisutu leo imemuachia huru Alhaj Salum Mwintanga kwa kukosekana ushahidi wa dhati katika kesi hii.

Ni pigo kwa serikali kutokana na udhaifu wa wanasheria wake au ndio namna watanzania wengi wanavyoonewa kwa kubambikiziwa kesi?

Just thinking aloud

Huyu hakubambikiwa kesi, kesi yake ingesikilizwa alikokamatiwa leo hii angeozea jela. Serikali iliiomba serikali ya Mauritius Mwintanga aje ashtakiwe huku; wenye akili tukajua its only a matter of time jamaa watakuwa huru (na waendeleze biashara yao haramu).

Huyu si wa kwanza, mnamkumbuka yule msomali alieachiwa kwa kuwa magazeti "yalimhukumu kabla ya kesi kusikilizwa"?
 
Yupi huyo mkuu? Rage au?
 
Nimecheka na pia kuhudhunika na UHUNI unaofanywa na wachache.
Off side trick
 
Sijawahi sikia mtu kafungwa kwa kesi ya madawa ya kulevya

Ni kweli hata mimi sikumbuki kusikia.
Ninachokumbuka kusikia ni mbwembwe za polisi wakati wanapowalamata.
Baadaye tunakuja kuambiwa kwamba zile hazikuwa dawa za kulevya, bali ni unga wa ugali!
 
Ni baada ya miaka minne tangu akamatwe kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevwa akishirikiana na mabondia wa timu ya taifa waliokamatwa huko Mauritius.

Mahakama ya Kisutu leo imemuachia huru Alhaj Salum Mwintanga kwa kukosekana ushahidi wa dhati katika kesi hii.

Ni pigo kwa serikali kutokana na udhaifu wa wanasheria wake au ndio namna watanzania wengi wanavyoonewa kwa kubambikiziwa kesi?

Just thinking aloud

Mkuu haki imetendeka!
 
..... Nchi hii bwana! we acha tuuu! Maana yake ukiongea mengi utaambiwa unaingilia uhuru wa mahakama! ..........au iko mahakamani.... ndivyo tulivyo.... madawa ya kulevya yana maaajina mengi.... lakini jina kubwa ni unga.... ndo maana kesi nyingi ushahidi unakuwa haupo kwa kuwa unaweza kubadilisha huo unga ukawa unga kweli........... katika katiba mpya nimependekeza wanaokamatwa na maswala ambayo ni READ handed hakuna haja ya upelelezi.. wanapeleleza nini.... wakati mtu amekamatwa nacho? kwa wenzetu especially China .......... hukumu iko tayari ... kifo au miaka 70 .... hakuna longolongo.. sijui upelelezi.. dhamana NOOOOOOO!

Back
Top Bottom