Kesi ya dawa za Kulevya: Mwintanga aachiwa huru

Kesi ya dawa za Kulevya: Mwintanga aachiwa huru

Mabondia wote walikwisha achiwa zamani,hakuna nayeshikiliwa huko Mauritius
 
Ni kweli hata mimi sikumbuki kusikia.
Ninachokumbuka kusikia ni mbwembwe za polisi wakati wanapowalamata.
Baadaye tunakuja kuambiwa kwamba zile hazikuwa dawa za kulevya, bali ni unga wa ugali!

Wapo waliofungwa hivi karibuni Mkoani Tanga na Jaji Kipenka Musa.
 
Hii kesi serikali imefanya makusudi kumuachia huyo jamaa, ukiangali mwenendo wake, hivi kweli serikali inashindwa kuwaleta mahshidi kutoka huko Maurtania? angekuwa kesi ya mahalu mbona walihangaika nayo sana? mwenye akili aambiwi tazama

Ni baada ya miaka minne tangu akamatwe kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevwa akishirikiana na mabondia wa timu ya taifa waliokamatwa huko Mauritius.

Mahakama ya Kisutu leo imemuachia huru Alhaj Salum Mwintanga kwa kukosekana ushahidi wa dhati katika kesi hii.

Ni pigo kwa serikali kutokana na udhaifu wa wanasheria wake au ndio namna watanzania wengi wanavyoonewa kwa kubambikiziwa kesi?

Just thinking aloud
 
sio udhaifu wa wanasheria, ni serikali yenyewe imeshindwa kuwaleta mashadi muhimu toka nchi mzigo ulipokamatwa

@POMPO unataka kusema jamaa katoa rushwa? sidhani mkuu ukisema udhaifu wa wanasheria wa serikali nitakubaliana nawe
 
Basi kama wale walishaachiwa kulikua hamna kesi hapo! Ukweli ni kwamba bado waandaa mashtaka wengi bongo ni bogus aidha kwa uzembe au wanajifanyisha makusudi kwa ahadi maalum
 
Precisely! Hilo ndilo jina nililokuwa nalitafuta, Akasha aliachiwa huru - he is dead now - kwa "kuhukumiwa" na magazeti!

Mkuu, huyu jamaa alifungwa lakini miaka kumi ama 12 kama sijakosea na alimaliza kifungo chake ndipo akatolewa kama sijakosea
 
Basi kama wale walishaachiwa kulikua hamna kesi hapo! Ukweli ni kwamba bado waandaa mashtaka wengi bongo ni bogus aidha kwa uzembe au wanajifanyisha makusudi kwa ahadi maalum

nakubaliana nawe,
 
Mkuu, huyu jamaa alifungwa lakini miaka kumi ama 12 kama sijakosea na alimaliza kifungo chake ndipo akatolewa kama sijakosea

Mkuu, Akasha alikata rufaa na kuachiwa on the basis mentioned before! Madai ya rufani yake - na ilikubaliwa - ni kuwa hukumu aliyopewa ilikuwa influenced na magazeti.
 
..... Nchi hii bwana! we acha tuuu! Maana yake ukiongea mengi utaambiwa unaingilia uhuru wa mahakama! ..........au iko mahakamani.... ndivyo tulivyo.... madawa ya kulevya yana maaajina mengi.... lakini jina kubwa ni unga.... ndo maana kesi nyingi ushahidi unakuwa haupo kwa kuwa unaweza kubadilisha huo unga ukawa unga kweli........... katika katiba mpya nimependekeza wanaokamatwa na maswala ambayo ni READ handed hakuna haja ya upelelezi.. wanapeleleza nini.... wakati mtu amekamatwa nacho? kwa wenzetu especially China .......... hukumu iko tayari ... kifo au miaka 70 .... hakuna longolongo.. sijui upelelezi.. dhamana NOOOOOOO!


kwa tanzania vita ya kupambana na biashara ya unga imshatushinda
wale mabondia waliobaki Mauritias nahisi utetezi wao ulikuwa mzigo huo walipewa na Mwitanga kwa hiyo hapa kawaruka wenzie au walimsingizia ili iweje?
mtakumbuka Jk alituambia kuwa anayo orodha ya wauza unga alishafikisha mahakamani hata mtu mmoja?
 
mabondia bado wanashikiliwa kule kule Mauritius mkuu

mbona hao mabondia walishaachiwa huru kitambo! mmojawapo ni EMILIAN PATRICK yule ambaye waTZ walishaanza kumchangia pesa ili akawakilishe vyema ktk mashindano ya OLYMPICS kule BEIJING mwaka 2008,ndo wakati anaenda kufanya maandalizi MAURITIUS akakumbwa na mkasa huo ila sasa yupo uraiani kitambo sana.
 
mbona hao mabondia walishaachiwa huru kitambo! mmojawapo ni EMILIAN PATRICK yule ambaye waTZ walishaanza kumchangia pesa ili akawakilishe vyema ktk mashindano ya OLYMPICS kule BEIJING mwaka 2008,ndo wakati anaenda kufanya maandalizi MAURITIUS akakumbwa na mkasa huo ila sasa yupo uraiani kitambo sana.

Thanx for info mkuu sikujua kama walishaachiwa
 
Haki kutendeka ni pamoja na mtuhumiwa kutia hatiani, kuachiwa na hata kesi kutupwa. Hivyo haki kutendeka siyo lazima ushinde. Hata ukishindwa ni haki pia. Vile vile siyo ujuvi kulalamikia kila jambo kwani kwa mawazo ya baadhi yetu ni wazi kila mmoja hata bila ushahidi angeweza kuhukumu atakavyo. Lakini kwa mizania ya kisheria na panapokosekana ushahidi madhubuti hakuna namna nyingine zaidi ya kuipiga chini kesi!!!!!!!!!! Pia ni vema tukaelewa kinachothibitishwa mahakamani siyo ukweli bali ushahidi!
 
hii nchi ni full disco yaani ukitaka kucheza cheza hakuna utawala hakuna sheria ndio maana wanasheria ni mabwenge kiasi hata nje ya nchi wanawaelewa kuwa wanasheria waserikali tanzania wanatumika
 
Mwanaweja
Wanasheria wa serikali si wajinga ila wamejitengenezea kanjia ka kupata ugali na wenyewe kutumia loopholes

Ndo hawa walisaini mkataba na mzungu wa RICHMOND eti ametumia busness card kama utambulisho kama sio maigizo ni nini?
 
Last edited by a moderator:
" If the law supposes that... the law is an ass"
George Chapman- Revenge for Honour
 
Back
Top Bottom