Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Wakuu!
Kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti Zanzibar Said Issa Mohammed dhidi ya Bodi ya Wadhamini ya Chadema na Katibu Mkuu wa Chama John Mnyika inaendelea leo Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, ambapo leo Mahakama itaanza kusikiliza shauri ndogo la kumtaka Jaji Hamidu Mwanga kujitoa katika Shauri hilo, kutoka na washitakiwa kukosa imani nae.
Kesi namba 8323/2025 ambayo imetoa zuio la muda kwa Chama cha Chadema kufanya shughuli zozote zile kiutendaji na oparesheni mpaka pale kesi ya msingi iliyofunguliwa itakapoanza kusikilizwa.
Baada ya Chadema kuwasilisha ombi kutaka Mh. Jaji Hamidu ajiondoe kwenye Kesi Namba 8323/2025 iliyofunguliwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti Chadema -Zanzibar, Said Issa Mohammed dhidi ya Bodi ya Wadhamini ya Chadema na Katibu Mkuu wa Chama John Mnyika kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo Julai 14, 2025 unatarajiwa kutolewa uamuzi wa ombi hilo ikiwa ni baada ya upande wa waleta mashtaka nao kupata muda wa kupitia hoja za ombi hilo.
Kwa mujibu Mawakili wa walalamikiwa wanadai kuwa hawana imani na Jaji huyo hasa kutokana na uamuzi wake wa kusitisha Shughuli za Kiutendaji za Chama na utumiaji wa rasilimali ambalo linaendelea mpaka kesi ya Msingi itakapoanza kusikilizwa.
Julai 10, 2025 Mh. Jaji Hamidu Mwanga alisema kuwa suala hilo awezi kulitolea uamuzi bila kutoa nafasi kwa upande wa waliofungua kesi nao kupitia hoja. Ambapo upande wa wafungua shauri kupitia Wakili wao waliomba ahirisho ili kupata nafasi ya kupitia ombi hilo.
Katika kesi ya msingi waleta maombi waliwasilisha madai kuwa CHADEMA imekuwa ikiitenga Zanzibar katika masuala mbalimbali ikiwemo mgawanyo wa raslimali za Chama.
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche, akiingia Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam kufuatilia kesi ya mgawanyo wa mali iliyofunguliwa na Said Mohammed dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa chama hicho.
=========================
Mnyika: Kwa sasa Mali za Chadema zipo hatarini kuporwa kutokana na uamuzi wa Mahakama
Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA Taifa, John Mnyika akisoma hoja za kutaka Mh. Jaji Hamidu Mwanga kujitoa kwenye shauri Namba 8323/2025, amesema kuwa tangu uamuzi wa Jaji huyo kuzuia Ofisi ya Katibu Mkuu, Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa Chama kutofanya kazi pamoja na rasilimali za Chama kutotumika amesema uamuzi huo unahatarisha usalama wa mali za taasisi yao.
Amesema kutokana na uamuzi wa kutotumia rasilimali za Chama kwa sasa Wafanyakazi wote wa CHADEMA wamesimamishwa kazi kwa kuwa hata fedha za taasisi hawaruhusiwi kuzigusa kutokana na zuio la Mahakama.
Aidha, ameeleza uamuzi huo unaziweka mali za Chama kwenye hatari ya kuibiwa, kuporwa au kuharibiwa wakati ambao Katibu Mkuu na Bodi ya Wadhamini hawaruhusiwi kufanya chochote kwa kuwa wanazuiwa.
Pia, Mnyika amesema tangu uamuzi huo ulipotolewa Ofisi zote za Chama zinakosa ulinzi, hali ambayo inaziweka kwenye hatari kuvamiwa na kufanyika wizi na uporaji kwa kuwa kwa sasa hazipo chini ya ulinzi wowote.
Vilevile amesema kwamba zuio kutofanya shughuli za kisiasa likiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwamba linaleta athari kwa Chama.
Kesi imeahirishwa mpaka Julai 28, 2025
Kesi imeahirishwa mpaka Julai 28, 2025 ambapo Jaji atatoa uamuzi kama anaendelea na shauri hilo au anajitoa kama ombi lilivyowasilishwa na upande wa Chadema wakitaka ajiondoe kwenye shauri hilo wakidai kuwa ana mgongano wa maslahi.
Soma, Pia