Kesi tata!

Kesi tata!

Jaguar

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2011
Posts
3,440
Reaction score
1,029
Siku moja Karim,John na James waliweka kambi jangwani.kila mmoja alikuwa na hifadhi yake ya chakula na maji.Karim alikuwa na chuki ya kisirisiri dhidi ya John,wakiwa wamelala usiku Karim alitia sumu ndani ya chupa ya maji ya John.James naye alikuwa na chuki na john,kabla John hajanywa maji yake,James alitoboa tobo kwenye kitako cha chupa ya maji ya John,maji yote yakavuja.John alipoamka kutaka kunywa maji aliyakosa na hatimaye alikufa kwa kiu.Nani aliyemuua John?James au Karim?
 
aliyemuua mwenzie si huyo James aliyemwaga maji, maana kama hakuyamwaga yeye basi angekuwa kauwawa na Karim kwa ile sumu,very simple but kiufupi James na Karim ni magaidi, ila hii kesi tukiipeleka The Hague, kiu kitahukumiwa kifo
 
Jibu ni simple kama ulivyosema,ila kama wewe ni mpelelezi,umeikuta maiti ya John pamoja na ile chupa yenye tundu chini ikiwa na mabaki ya matone ya maji yenye sumu.utamjuaje muuaji?
 
Jibu ni simple kama ulivyosema,ila kama wewe ni mpelelezi,umeikuta maiti ya John pamoja na ile chupa yenye tundu chini ikiwa na mabaki ya matone ya maji yenye sumu.utamjuaje muuaji?

hiyo unamuachia Mungu
 
hayo ni mambo ya kusadikika, ambayo kuwako kwake n kufikirika.
 
muuwaji ni kiu ndo kilichofanikisha kifo cha mshikaj
 
kwani kifo nae alikuwa rafiki yao? walisafik¡ri nae? au alikuwa anawavizia?
 
mtu hafi kiu kwa siku moja wewe, mbona wenzake wali-survive
 
mtu hafi kiu kwa siku moja wewe, mbona wenzake wali-survive
Ni kweli mkuu,mtu hafi kiu kwa siku moja,ila katika thread sikuandika alikufa baada ya siku ngapi?
 
Labda tujiulize pia,hatia ya uuaji ni ile NIA ya kuua au FANIKIO la kuua?
 
Du, swali tata kweli...kiupelelezi tutamhukumu aliyeweka sumu kwenye chupa, maana hata kama chupa isingetobolewa bado angekufa kwa sumu. na isitoshe, mwenye nia wa kwanza ndiye nshtakiwa wa kwanza,lol! sijui nimekaribia ukweli!???
 
kutokana na utaratibu wa bongo hakika hapo inahitajika iundwe Tume Huru ichunguze!
 
Back
Top Bottom