Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,783
- 14,975
Kesi namba 458 ya mwaka 2016 (Jamhuri dhidi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence Melo na mwenzake Mike William) imeendelea leo tarehe 23 Machi 2020 mbele ya Hakimu Huruma Shaidi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Katika shtaka la pili kwenye Kesi hiyo, Watuhumiwa wanashtakiwa kwa kuzuia upelelezi wa Polisi kwa kutokutoa taarifa za Mteja aliyeandika taarifa kuhusu Benki ya CRDB ikihusishwa na makato katika miamala zaidi ya inavyotakiwa
Kwa siku ya leo, upande wa Jamhuri umewakilishwa na Wakili Janeth Magoho huku upande wa utetezi ukiwakilishwa na Mawakili Hekima Mwasipu, Benedict Ishabakaki na Hassan Kiangio.
Wakili wa Jamhuri amesema bado hawajapata shahidi wa kuendelea naye katika shauri hili.
Kwa mara ya Mwisho kesi hii kuwa na shahidi Mahakamani ilikuwa mwaka 2018. Na kesi imekuwa ikiahirishwa kwa sababu mbalimbali. Tarehe ya mwisho shahidi kusikilizwa ilikuwa ni Novemba 12, 2018 ambapo Mpelelezi Kitengo cha Upelelezi wa Makosa ya Mtandaoni kutoka Makao Makuu ya Polisi (HQ), Inspekta Beatrice Majule ndiye alikuwa shahidi.
Hakimu Shaidi ameonyesha kutofurahishwa na maahirisho ya shauri hili kwa zaidi ya mwaka na kuutaka upande wa mashtaka kuja na msimamo unaoeleweka kwani anatambua akiifuta washtakiwa watakamatwa na kesi kuanza upya.
Leo kesi imeahirishwa hadi tarehe 23 Aprili 2020.
***
Shauri jingine namba 456 lililo chini ya Hakimu Thomas Simba dhidi yao linatarajiwa kutolewa hukumu mnamo Aprili 02, 2020
Kujua kilichojiri awali kwenye shairi hili na mengine ya JamiiForums, tembelea Muendelezo wa Kinachojiri Kisutu: Kesi za Jamhuri dhidi ya JamiiForums - JamiiForums