Kesi namba 457: Mahakama yasema Maxence Melo na Micke William hawana Kesi ya kujibu! Yawaachia huru

JAMII-FORUMS2.jpg
KESI namba 457 (Jamhuri v Maxence Melo na mwenzake Micke William) inayohusu kampuni za CUSNA Investment na Ocean Link kudaiwa kukwepa kodi Bandarini Dar na kunyanyasa wafanyakazi wa kitanzania imeendelea leo Juni 01, 2018 katika Mahakama ya Mkazi, Kisutu.

Akisoma shauri hilo Hakimu Godfrey Mwambapa amesema washitakiwa hawana kesi ya kujibu na hiyo Mahakama imewaachia huru kuanzia leo. Hili ni moja kati ya mashauri 3 yaliyokuwa yanawakabili washtakiwa. Kwa mantiki hiyo, bado kuna mashtaka 2 yatakayotajwa mahakamani hapa Juni 18.

Kesi hii namba 457 iliyokuwa ikiikabili JamiiForums, ilihusu kampuni ya CUSNA Investment ambayo ilidaiwa kufoji nyaraka bandarini, kukwepa kodi na kuwatesa wafanyakazi wazalendo na kupendelea wageni toka nje ya nchi.
JAMII-FORUMS.jpg
Asante kwa taarifa
 
mtu yeyote anayejaribu kurudisha nyuma ukuaji wa teknolojia...hawezi fanikiwa. zaidi atajaribu tu kupotezea muda wengine na kuonyesha mapungufu yake juu ya teknolojia mpya.

Hongera zake ziwe kwao akina bwana Melo...et al
 
Hii maana yake nini, maana yake ni kwamba pale waendesha mashitaka wanapolazimishwa ku-indict watu huku ikionekana wazi kesi haina "Merits" zozote kisheria basi tu ili mradi kutii amri kutoka juu. Very Shameful.
Mkuu umenena lakini ngoja niseme kitu. Kwa uzoefu wangu nchi yetu haijawahi kuwa na sheria za haki. Na hakuna anayejishughulisha kupigia kelele hili la kujaribu kuzifanya sheria zetu kuwa za haki. Kwa mfano hapo unaweza kukuta hata hao malaika na sultan wao walijua hakuna kesi hapo tangu mwanzo lakini wao waliridhika tu kutumia jeshi la polisi kusumbua watu tu basi na roho zao zimefurahi. Mfano hawa makarani wakubwa wa wilaya sijui mnawaita wakuu wa wilaya na wa mkoa eti wana mamlaka kisheria kumuweka mtu ndani masaa 48 bila hata kuhojiwa. Kungekuwa na upande wa pili kuwa ikithibitika kuwa haikuwa haki kuwekwa ndani, aliyafanya hivyo anawajibika kisheria, oooh hapo tungeenda sawa. Lakini sasa hivi ukigombania demu na mkuu wa mkoa ujue saa 48 jela inakuhusu ingawa wenyewe wanaita mahabusu.
Kwa mfano umepishana maneno na Mkuu jiwe au mwanae wanaweza kujifanya hawana habari na wewe, lakini siku moja unaweza kujikuta una kesi ya mauaji ambayo hata wanaokushitaki wanajua mwisho wa siku utashinda lakini bahati mbaya kwa sheria zetu kwa kesi hiyo unatakiwa ufungwe kwanza halafu mengine yatafuta yaani guilty till proven innocent. Wenyewe wanakuambia hujafungwa ila uko mahabusu,!!! the differrence here is technical I bet. Mara nyingi hawa watukufu wakuu malaika waheshimiwa watakatifu lengo lao ni kukukomesha tu kwa kesi iakayodumu miaka mitano baaasi
NAWASILISHA
 
Kuna mambo mengine ya ajabu sana hapa kwetu. Yaani mtu anakwambia kuwa fulani anawaibia, anawadanganya, na anaihujumu familia nzima. Badala ya kuichunguza taarifa hii na wahusika waliotajwa na raia mwema, wewe unaenda kushughulika na raia mwema aliyetoa taarifa kwenu. Kwa sababu hata sasa ukiwauliza kama zile taarifa ni za kweli au la watakwambia kuwa sisi tulikuwa hatuangalii hilo bali tulikuwa tunaangalia mtu kuchafuliwa. Je mmehakikisha kuwa hizo taarifa ni za uongo ikiwa ni pamoja na kuleta taarifa za uchunguzi baada ya taarifa ya raia mwema wa nchi hii? Utasikia hatujafanya uchunguzi bali tulikuwa tunataka kumkamata aliyesema. Huu ni upuuzi mkubwa sana!!Kwanini tusiseme kuwa mnahusika na waliotajwa???
 
Mkuu Tindikali,

Nichelee kufikiria umesema haya kwa kutoelewa vema na si kwa makusudi. Naomba ufahamu kuwa maelekezo yako si sahihi. Moja ya sababu (nje ya nyingi zilizotajwa na hakimu) ambayo ndiyo imebeba sababu kubwa, ni Mahakama kutoridhishwa na ushahidi na maelezo ya sababu za kuomba taarifa zilizodaiwa kukataliwa kutolewa na Washtakiwa kwa Jeshi la Polisi.

Izingatiwe kwamba JLP pamoja na kutembelea ofisi za Jamii bila taarifa, hawakuondoka na taarifa zozote za wateja ama zinazohusiana na platform moja kwa moja. Sababu ambayo ingekuwa sahihi kwa maelezo uliyotoa.

JAMIIFORUMS haijasema hawajui identity ya KWAYU na AMRI SHIPURI, bali wamekataa kuwatambulisha kwa polisi kwa sababu hakukuwa na arrest warrant pamoja na kuelezwa makosa yao.

Kwa hiyo serikali ikirekebisha criminal procedure ya kuomba majina ya wachangiaji JAMIIFORUMS itatuchondoa. Plain and simple.

That must scare the living daylights out of every person in these forums who treasures free expression.
 
Back
Top Bottom