McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 889
- 2,863
Wakuu,
Siku ya leo ndo ile siku ambayo Mahakama itaanza kusikiliza kesi ya CHADEMA baada ya kushtakiwa na wanachama wao wa Zanzibar kwamba wanatumia mali za chama vibaya
==============
Alichoandika Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche
Kesi ya kina Said Issa ni Kesi ya kisiasa kujaribu kuzuia chama chetu kufanya shughuli zake halali..
Jaji aliepanga Kesi leo anakosaje kuwepo mahakani siku ya Kesi tena Kesi muhimu kama hii kwa Nchi?
Jaji aliefanya maamuzi ya haraka na kutoa maamuzi tena bila hata upande wetu kuwa na uwakilishi wa wanasheria!!
Mahakama ya Tanzania isikubali kutumiwa na wanasiasa ambao wameshindwa kufanya kazi za siasa za kushawishi umma.
==========================
Shauri ambalo limetoa zuio kwa Chadema kufanya siasa limeahirishwa ikidaiwa Jaji ana majukumu mengine
Kesi namba 8323/2025 ambayo imetoa zuio la muda kwa Chama cha Chadema kufanya shughuli zozote zile kiutendaji na oparesheni mpaka pale kesi ya msingi iliyofunguliwa itakapoanza kusikilizwa, imeahirishwa mpaka Julai 10, 2025 kutokana na Mh. Jaji Hamidu Mwanga anayesikiliza kutokuwepo.
Katika kesi hiyo ambayo imetajwa leo June 24, 2025 kwa ajili ya kusikilizwa, ilifunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, Saidi Issa Mohamed na wenzake wawili (2) dhidi ya Baraza la Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA.
Akizungumzia shauri hilo baada ya shauri kuahirishwa Wakili Utetezi, Hekima Mwasipu amesema kuwa Jaji hajatokea Mahakamani ikidaiwa kuwa yupo na majukumu mengine.
Ikumbukwe Shauri hilo lilikuja kufuatia maombi yaliyowasilishwa Mahakamani hapo na Mawakili wa waleta maombi wakiongozwa na Wakili Gido Thomas Simfukwe ambao waliiomba Mahakama kuweka zuio hilo hadi kesi ya msingi itakapoanza kusikilizwa.
Kwenye kesi ya msingi waleta maombi wamewasilisha madai kuwa CHADEMA imekuwa ikiitenga Zanzibar katika masuala mbalimbali ikiwemo mgawanyo wa raslimali fedha n.k .
Pia soma Pre GE2025 - Mnyika ashangazwa na kitendo cha Jaji kutokufika mahakamani