Kesi hizi ziliishia wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi hizi ziliishia wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, May 28, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Dk Hoseah

  MKURUGENZI wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah jana amesema kesi za ufisadi zitakazofikishwa mahakamani hivi karibuni ni nzito na zitastua wengi.

  Dk Hoseah pia alisema uchunguzi wa kesi mbili kati ya hizo umeshakamilika na zitaanza kunguruma mahakamani mwezi ujao na kwamba kesi hizo tatu zimeibuliwa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG).

  Kigogo huyo wa Takukuru, ambaye alikuwa akizungumzia uhusiano wa ofisi yake na CAG kwenye mkutano uliohusisha wakaguzi wa mahesabu na wanasiasa kutoka nchi mbalimbali, alisema tayari majalada ya mashauri hayo matatu yameshawasilishwa ofisi ya mwendesha mashtaka huyo kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.


  "Tumemaliza kuyafanyia uchunguzi mashauri matatu mazito ya ubadhilifu na matumizi mabaya ya fedha uliofanywa serikalini ambayo yaliibuliwa na CAG," alisema Dk Hoseah.

  "Kesi hizo ni nzito na zitastua," alisema Dk Hoseah akionekana kujiamini.


  Awali Dk Hoseah hakutaka kufafanua juu ya kesi hizo, lakini alipopigiwa simu baadaye alisema uchunguzi uliokamilika ni wa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo na ile ya sakata la mbolea ya Kigoma.

  Katika sakata hilo la Bagamoyo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alitimua watumishi wanne vigogo baada ya CAG kubaini ubadhirifu wa zaidi ya Sh900 milioni za miradi, lakini kauli ya Dk Hoseah inamaanisha kuwa kuna mengi makubwa yataibuliwa kwenye kashfa hiyo, ambayo mmoja wa mawaziri wa serikali ya awamu ya nne anatajwa kuhusika.


  Akizungumza katika mkutano huo uliowakutanisha wakaguzi wa mahesabu pamoja na wanasiasa kutoka ndani na nje ya nchi, Dk Hoseah alisema rushwa katika manunuzi ya umma inasababishwa na serikali kutokana na kutokuwa makini katika kufuatilia manunuzi hayo.

  "Mfano ni gari aina ya shangingi; Tanzania italinunua kwa Sh100 milioni, lakini Uganda na hata Zambia wao watanunua chini ya hapo au hata kwa asilimia 50 ya bei hiyo," alisema.


  "Hapa unaona jinsi serikali isivyokuwa makini katika kusimamia manunuzi ya vitu vya umma."

  Akizungumzia kuhusu rushwa kubwa, Dk Hoseah alisema taasisi yake imekumbana na changamoto kubwa ya kuwafungulia kesi watu wanaojihusisha na vitendo hivyo.

  Alifafanua wengi wa wanaojihusisha na rushwa kubwa, wana mbinu nyingi ikiwemo ya kuhifadhi fedha nje ya nchini na mara nyingi huzihamisha kwenda nchi nyingine.

  "Mfano baada ya mtu kula rushwa, fedha ataweka katika benki ya Barclays nchini kisha atazihamishia Barclays ya Uingereza kisha ataziamishia katika Barclays iliyopo nchini Shelisheli au Italia," alifafanua.


  "Ili ufanikishe kumtia nguvuni ni lazima ushirikiane na Wizara ya Mambo ya Nje na pia upate ushirikiano wa karibu na nchi husika na mara nyingi majibu kutoka katika nchi hizo unaweza kuyapata baada ya miezi sita."

  Alisema kutokana na hali hiyo, Takukuru hulazimika kuchukua muda mrefu kukamilisha uchunguzi dhidi ya rushwa kubwa, tofauti na ilivyo kwa rushwa ndogo na za kawaida.

  Akizungumzia mfumo ambao unaiweka Takukuru chini ofisi ya rais na hivyo kuifanya isiwe na uhuru katika uwajibikaji, Dk Hoseah alisema hiyo si hoja ya msingi na kuwa taasisi hiyo inafanya kazi katika mazingira huru na yanayofuata sheria, kanuni na utaratibu uliopo.


  "Kwangu mimi kuwa huru ni kufanya kazi katika mazingira huru na kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizopo pasipo kuingiliwa. Hali hiyo ndiyo iliyopo Takukuru," alisema.


  Chanzo: Dk Hoseah: Kesi tatu zitakazotikisa zinakuja
   
 2. M

  Mzee2000 JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2010
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 491
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  Wamefungwa wangapi , Ni kesi ngapi bado zinaendelea?
   
 3. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #3
  Aug 13, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kuanzia lini Mkwere akawa serious na anachokiongea?
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Sep 15, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Nimeambatanisha statistics za malalamiko yaliyopokelewa na TAKUKURU tangu 1995 - 2009 na hatua zilizochukuliwa juu ya malalamiko hayo. Pamoja na hayo kuna kibonzo hapa chini kinachozungumzia juu ya Rushwa Kubwa (grand corruption)! Je, una manoni yoyote juu ya kibonzo (katuni) hicho?

  [​IMG]

  [​IMG]

  View attachment CASE STATISTICS OF PCCB.pdf
   
 5. n

  nmaduhu Member

  #5
  Sep 15, 2010
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ha ha ha ha , kwi kwi kwi kwi, sawa na panya wanobishana nani akamfunge paka kengere......
   
 6. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #6
  Sep 15, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kutoka kwenye tovuti ya TAKUKURU mambo yafuatayo yamezunguziwa:

  Statistics as from 1995 to April 2010 translate as follows: 43,007 allegations were received since 1995 to April 2010. Not all the allegations being reported are related to corruption.
  - Number of administrative actions taken against public servants proven to be inclined to take bribes and other corrupt behavior since 1995 to April 2010 are 912 Public Servants.
  - Number of new cases filed into courts since the new Act (PCCA, 2007) became operational are 624 cases.
  - Number of convictions against corrupt offenders in courts since 1995 to April 2010 are 203.
  - Money recovered by PCCB for the period 1995 to April 2010 is to the tune of Tshs. 97 Billions.

  Je, kazi iliyofanywa na Taasisi hiyo sio mfano wa kuigwa ukichukulia kwamba utashi wa kisiasa (Political Will) ya nchi yetu iko chini? Tujadili!
   
 7. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #7
  Sep 15, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Buchanan, hizi figure mwenzagu umezielewa kweli? Mimi naona kizunzungu.

  Kwa mfano 2007 allegations zilikuwa 8235, kati ya allegations hizo walipileleza kesi 1266 tu, halafu mwaka huo huo completed investigations ni 2015 yaani idadi ni kubwa kuliko zile zilizo pelelezwa inawezekana kweli hii?

  Tukiendelea baada ya upelezi kukamilika zilizopelekwa mahakamani ni kesi 196 tu kwa nini zingine hazikuenda mahakamani? Hesabu bado inapwaya ukichukulia admistartave action taken na cases transferred to other organs bado haifikii kesi ambazo upelelzi umekamilika. Kweli mahesabu haya yanahitaji maelezo ya kina.

  lakini hata hivyo utendaji wao ni wa kiudhaifu kwa mfano mwaka 2009 malalamiko yaliyopokelewa ni 5930 na kesi walizopeleleza na kumaliza upelelzi ni 1175 ina maana kesi 97 kwa mwaka kwa Tanzania nzima huu ni utani kabisa
   
 8. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #8
  Sep 15, 2010
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Ninavyoelewa:
  TAKUKURU ni chombo cha kisheria, kwa maana kwamba Taarifa wanazopokea na kuzifanyia kazi ni zile tu ambazo kimsingi ni Makosa ambayo yameainishwa katika Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa PCCA, No.11, 2007. Taarifa ambazo hazihusiani na makosa katika Sheria hiyo zinakuwa Refered ktk vyombo vingine vya kisheria/dola e.g Polisi etc. That means PCCB wanaweza pokea taarifa nyingi lkn zinazofanyiwa kazi ni zile tu ambazo zinahusisha makosa yaliyoainishwa ktk sheria yao, ambazo hawahusiki nazo zinakuwa refered pengine.
   
 9. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #9
  Sep 15, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Sure!
   
 10. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #10
  Sep 15, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Sure!
   
 11. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #11
  Sep 29, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wakuu media in Tz ziliripoti kwa nguvu kubwa sana kesi hizi zilipoibuka, lakini cha kushangaza ni kama vile zilishajifia, je kuna mwenye updates kuhusu kesi hizi?

  1. Rostam Vs Mengi

  2. Mengi Vs Rostam

  3. Makongoro Mahanga Vs Msemakweli

  4. Govt Vs Mahalu & Grace Martin

  5. Police Vs Dereva wa Mwakyembe

  6. Wenyeviti wa CCM wa mikoa Vs Mwanahalisi

  7. Rostam Vs Mwanahalisi

  8. Police Vs CUF (Kuhusiana na visu uchaguzi 2005)

  9. Mengi Vs Habari Corporation

  10. Govt Vs Kweka (Former projecct manager wa BOT)

  11. Mengi Vs Masha

  12. Masha Vs Mengi

  NA JE KESI HIZI HAPA CHINI ZILIFUNGULIWA ?? (maana wahusika walisikika wakisema kwa mbwembwe kwamba wameshawaagiza wanasheria wao kufungua kesi)

  1. Rutabanzibwa Vs Dr. Slaa ( List of shame)

  2. Vicent Mrisho Vs Dr. Slaa (List of shame)

  3. Lowassa Vs Mwanahalisi ( Richmond)

  4. Sitta Vs Dr. Slaa (Kuhusiana na wizi wa EPA kwamba documents zimefojiwa).

  5. Chenge Vs NBC (Account yake kuwekwa hadharani)

  6. Chenge Vs Dr. Slaa (List of shame)
   
 12. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #12
  Sep 29, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Umesahau na ile ya Mengi na Masha. Au Masha na Mengi.
   
 13. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #13
  Sep 29, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nimeshaiweka mkuu!!!!!!
   
 14. Emma Lukosi

  Emma Lukosi Verified User

  #14
  Sep 29, 2010
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Jmani!, CCM wamewaletea akina Jay-z, 50 cent, Fiesta kila mwaka enh!, Wamewaletea Brazil Nchini ili msahau :becky:. Lakini Wabongo wabishiii :confused2:. Wali mleta Hadi Bush lakini wapi! duh!.
   
 15. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #15
  Sep 29, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Nyingi ya hizo za kuhusu "List of shame" zilikufa kutokana na ukweli wa tuhuma zilizotolewa na Dr Slaa kule Mwembe yanga. Usisahau kwamba wengi hukimbilia kortini ili kutaka kujikosha mara moja mbele ya umma kuhusu tuhuma nzito zilizotolewa, lakini baadaye huwa hawazifatilii kesi hizo kwani huwa hawana hoja madhubuti za kuzipinga tuhuma hizo mahakamani.
   
 16. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #16
  Sep 29, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hapo ndiyo huwa naishangaa media ya bongo, huwa hawawezi kufuatilia ishu ikawa concluded. If A alleges B of some high level allegations so to be judgded by the media and the court of public opinion. Mwaka, miaka inaisha bila upadate na media wala haitupashi tena kuhusu kinachoendelea katika msisimko uleule kama inavyokuwa wakati wana-break the nuwz.
   
 17. Nicky82

  Nicky82 JF-Expert Member

  #17
  Sep 29, 2010
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 939
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuna ile ya Alex Massawe ya kujihusisha na ujambazi, ilifunguliwa miezi ya mwanzoni kabisa ya JK
   
 18. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #18
  Sep 29, 2010
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
   
 19. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #19
  Sep 29, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu umekumbusha, hii nakumbuka ilitumika sana kum-elevate JK kwamba eti yuko serious na majambazi wakubwa wakubwa!!! Cry myh beloved country!!!!!!!!!
   
Loading...