Kesho madereva wana kikao

Kesho madereva wana kikao

Egwugu

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2011
Posts
17,558
Reaction score
8,552
Kwa mujibu wa walivyosema kupitia habari ni kwamba kesho Jumatatu wanatarajia kuwa na kikao,hivyo ndugu zangu wasafiri kesho tujiandae kupanda bodaboda make vikao vyao kinachofata sote tunakijua.
 
Napita tu jamani. Naomba nisimame kidogo na kuuliza, huu mwaka wa shetani hatma yake ni nini?
 
Makoda nadhani ataitisha mgomo maana ndio ahadi yake
 
Kwa mujibu wa walivyosema kupitia habari ni kwamba kesho Jumatatu wanatarajia kuwa na kikao,hivyo ndugu zangu wasafiri kesho tujiandae kupanda bodaboda make vikao vyao kinachofata sote tunakijua.

Kwanini Kichwa Chako Cha Habari Kisingekuwa " Kesho Madereva Kugoma Tena "? Kwahiyo Wakiwa ktk Hicho Kikao Chao Tutaendeshwa Na Shangazi Na Wajomba Zako? au? Muwe Mnanyoosha Maelezo Na Maneno Yenu Bhana!
 
ni kikao au mkusanyiko wa madereva..
maana kile kikundi cha madereva walisema sio halali.
 
Kwanini Kichwa Chako Cha Habari Kisingekuwa " Kesho Madereva Kugoma Tena "? Kwahiyo Wakiwa ktk Hicho Kikao Chao Tutaendeshwa Na Shangazi Na Wajomba Zako? au? Muwe Mnanyoosha Maelezo Na Maneno Yenu Bhana!
Dah! ama kweli dunia hadaa...
 
Makonda alikimbia na Microphones ili kumnyima nafasi Kamanda Mbowe aliyekuwa na solution ya muda mrefu, asitoe mchango wake ili utukufu uende kwa Makonda!.

Haya sasa Makonda, ulidhani umepata utukufu, siku 12 leo tangu uwaahidi madreva. Au ndiyo umeitisha kikao ili utangaze mgomo wako?

Msiwafanye watanzania majuha. Kama huna solution, usikimbilie kuwadanganya bila mkakati.
 
Makonda alikimbia na Microphones ili kumnyima nafasi Kamanda Mbowe aliyekuwa na solution ya muda mrefu, asitoe mchango wake ili utukufu uende kwa Makonda!.

Haya sasa Makonda, ulidhani umepata utukufu, siku 12 leo tangu uwaahidi madreva. Au ndiyo umeitisha kikao ili utangaze mgomo wako?

Msiwafanye watanzania majuha. Kama huna solution, usikimbilie kuwadanganya bila mkakati. Sasa itajulikana nani juha kati ya Madreva na Makonda.

Kwani Makonda nao wanagoma au wamewadanganyaje madereva hapo mbona sijawaelewa?
 
kumbe siku 12 tokea makonda atoe tamko lake.

labda kesho atakuja na mrejesho wa suluhisho.
 
Duh kesho nina safari dar-mwanza hicho kikao cha madereva wanakutana wale wakuu wao au na madereva wote watakuwepo wekeni wazi.
 
kumbe siku 12 tokea makonda atoe tamko lake.

labda kesho atakuja na mrejesho wa suluhisho.

makonda ataweza kumaliza mgogoro ambayo waziri mkuu ameshindwa kwenda kutoa hiyo ahadi.
 
Makonda alikimbia na Microphones ili kumnyima nafasi Kamanda Mbowe aliyekuwa na solution ya muda mrefu, asitoe mchango wake ili utukufu uende kwa Makonda!.

Haya sasa Makonda, ulidhani umepata utukufu, siku 12 leo tangu uwaahidi madreva. Au ndiyo umeitisha kikao ili utangaze mgomo wako?

Msiwafanye watanzania majuha. Kama huna solution, usikimbilie kuwadanganya bila mkakati. Sasa itajulikana nani juha kati ya Madreva na Makonda.
Kwani Mbowe ni nani nchi? ana mamlaka gani! acheni kushabikia vitu kisiasa...au ni migomo ya kutengeneza!
 
Mgorogoro wa madreva hauna budi kuendelea tena kuzalisha mgomo wenye tija kudidimiza uchumi uliokwisha zama. Na hizo ni rasha rasha tu,Waalimu nao unafurukuta kabla ya Juni ukifuatiwa na madaktari.Mwezi Juni ni mwanzo wa hitimisho la ngwe ya nne CCM itakuwa imegawanyika pande mbili,Muungano nao utakuwa hati hati.Ifikapo Julai wananchi watakuwa barabarani kukabiliana na polisi ambao watakuwa wamechoka na kuungana na wananchi,Jeshi litashika hatamu kukabiliana na hali mbaya ya vurumai la kisiasa ,kiuchumi, na kijamii.Tanzania itatangazwa eneo hatari la Afrika ya Mashariki. Zitaibuka tabaka mbali mbali kutafuta kutuliza ghasia na ndipo itaundwa mahakama kama ile ya kimbari kusimamia mustakabali wa kidemokrasia kuirudisha nchi katika mstari.Voiongozi wengi watakimbilia nje ya nchi na wengine watakamatwa na mali zao kutaifishwa,
HATIMA YETU; Vijana watachukua nafasi za mstari wa mbele kuleta ushawishi wa mabadiliko,Uchaguzi Mkuu itabidi kufanyika mwakani kwa ncha ya upanga baada ya marekebisho ya kero nyingi kupatiwa muafaka.TUJIANDAE KUYAONA MABADILIKO HAYO.
 
Emma.

naamin na makonda atakuwepo pale madereva watapokutana na kutoa trh ya mgomo.
 
Last edited by a moderator:
Wasituyeyushe hao madereva kama wanagoma wagome moja kwa moja sio wanabeep tu tumewachoka na migomo yao ya kinjaa njaaa.
 
naamin kesho hamna mgomo maana hawa madereva huwa wanatoa tarehe ya mgomo cku kadhaa kabla.
 
Mkuu, kwenye mgomo uliopita, alikwenda ubungo, madreva wakamtupia mawe akajificha. Alipofika pale Kamanda Mbowe, madreva wakachangamka, wakawa calm, wakajiorganize wakimsubiri Mbowe ahutubie. Kabla Mbowe hajahutubia, akatumia utulivu huo Makonda kuongea nao akijua watamsikiliza kwa vile Mbowe yupo.

Makonda, kwa kuwa amendandia jukwaa na hoja hana, akawaambia Madreva kwamba matatizo yao ndani ya siku saba yatakuwa yameshughulikiwa. Na kama siku saba zikiisha hayajashughulikiwa, yeye mwenyewe Makonda ataongoza mgomo wa Madreva. Baada ya pumba hizo ambazo hazikuwa na backup wala support, akashuka jukwaani na aliposhuka akakimbia na Microphones ili Kamanda Mbowe aliyekuwa na neno lenye akili asizungumze. Na ndivyo ilikuwa.

Sasa siku saba zimekwisha leo siku ya 12, hakuna jibu limetoka. Sasa kwa kuwa Makonda aliahidi siku saba angeitisha na kuongoza mgomo, basi tunaona hiyo keshe yamkini ndiyo siku anakwenda kuorganize na kutangaza mgomo wa madreva ukiongozwa na yeye.

Kwani Makonda nao wanagoma au wamewadanganyaje madereva hapo mbona sijawaelewa?
 
Back
Top Bottom