Kesho kuna watu watalia kwa furaha na kuna wataohuzunika na kuumia pia

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,176
144,755
Kibinadamu, kumuona Lissu akiwa hai lakini anachechemea, kutosababisha mixed reaction kubwa sana kwa wataofika kumpokea na popote atapokwenda kwa kipindi cha muda fulani mpaka watu wazoee kumuona katika hali mpya aliyonayo.

Lissu mwenyewe, kama anavyoonekana katika clips zilizoko mitandaoni, atakuwa ni mtu wa furaha na kutabasamu, ila kwa wengine, hali inaweza kuwa tofauti. Tutarajie kuona watu wakilipuka kwa furaha hiyo kesho, lakini pia tusishangae ikitokea wengine wakaonekana kufuta machozi kwa vitambaa.

Attention ni kubwa sana na Twitter kwa sasa imetekwa na clip za Lissu na wenzake wakiwa wanajiandaa kurudi nyumbani.

Mungu ni wa ajabu, hasa kwa sisi tuliobahatika kumuona Lissu akipandishwa kwenye ndege usiku ule wa September 7, 2017 kwani alikuwa kwenye very critical condition na hii inaleta hisia sana.

Nakumbuka kuona drip ya maji/dawa, drip ya damu na mashine ya kupumulia vikiwa ni sehemu ya mwili wa Lissu uliokuwa ukipandishwa katika ndege na kundi kubwa la wabunge wenzake.

Wanaosema huu ni muujiza,waacheni waseme.
 
Lissu anakuja kuamsha hamasa ya siasa za upinzani Tanzania, anakuja kuonesha ni kwa kiasi gani CCM kama chama cha siasa kilishakufa siku nyingi sana, wamebaki raia wachache humu wanaolipwa kwa kuandika uongo kukilinda, ila ukweli hizi ni zama za upinzani.
 
Back
Top Bottom