chakarikamkopo
Member
- May 24, 2012
- 79
- 54
Nimekuwa nikitumia line ya voda kwa muda wa zaidi ya miaka 12. Nimepoteza hiyo line nikaamua kwenda kurenew pale Vodashop Ubungo Plaza. Ajabu nikaambiwa niorodhesha namba tano (5) nilizopiga mara ya mwisho. Ile line nilikuwa natumia kwenye modem ya voda. Sijaitumia kwa calls kama miezi mitano hivi. Katika namba tano, moja tu ndo imeonekana. Nikaambiwa siwezi kuhuisha line hiyo hadi namba tano zitimie.
Mimi nimeona huu ni ''ujima'' wa hali yajuu sana maana ile line nilishaisajili na kitambulisho nilichotumia kusajili ndio nilikuwa nacho. Si ingetosha kucheki taarifa zangu za usajili na kulinganisha na kitambulisho? Hivi haya mambo ya simu tano yanasaidia vipi,watu tuna mambo mengi sana isitoshe tunapiga simu bila hata kukumbuka umempigia nani maana mtu unakuwa na laini zaidi ya moja.
Hii pia ni kero kubwa jamani....