Kero za kuajiriwa ... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kero za kuajiriwa ...

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by ngoshwe, Jul 17, 2011.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Nafanya kazi, laki tisa KITU NI mshahara wangu wa mwezi unasoma kwenye "salary slip" lakini kiasi nachoingiziwa benki ni laki nne na USHEE tu. Hii inatokana na makato kibao, nakatwa bima ya afya (27, 565.20) , malipo ya bodi ya mikopo ya vyuo vikuu (18,377.08), mfuko pensheni, (45,942) , mkopo mdogo niliokopa benki (ZAIDI YA 200,000). Kodi ya mapato (163,882).

  Inaonekana kodi kwa kuajiriwa ni klubwa sana. Miaka fulani serikali ilifuta kodi ya kichwa na baadae ushuru kwa mazao ya kilimo ili kuwaondolea kero wakulima (wananchi). Lakini cha kusikitisha nchi hii kufanya kazi imekuwa kero, tupu, ukiwa unafanya kazi na wakati huo huo ni mkulima na mfanyabiashara nadahani utayaona maumivu ya hizi kodi.

  Sisi tulioajiriwa hatulalamiki sana tunapokatwa " pay as you earn (paye)" ambayo wajanja wachache wanaitumia kuishi japo ilitarajiwa kuwasaidia wengi lakini bado hao wengi ndio imekuwa mzigo kwetu, tuna ishi nao majumbani tukitumia nao hicho hicho kidogo tunachopokea baada ya kukatwa !.

  Kule ulaya na marekani, wale wanaoishi kwa kutegemea posho na uwezeshaji wa umma ( "ma-benefit" ) wengi wameamua ni heri wasifanye kazi kabisa ili waendeelee kuhudumiwa na serikali kuliko kufanya kazi halafu ukaishia kupokea mshahara kichele baada ya makatio kibao.

  SINA HAKIKA KAMA HIVI VYAMA VYETU VYA WAFANYAKAZI VINAJUA MAJUKUMU YAKE VIZURI..SISI WANYONGE TUNAUMIA. NI HERI SERIKALI INGEAMUA KUANDIKISHA KILA FAMILIA NA KUJUA MAHITAJI YAO NA IKIWEZEKANA IKAANZISHA UTARATIBU WA KUZIHUDUMIA ZILE AMBAZO HAZINA UWEZO..UNAKUTA KATIKA FAMILIA NYINGI ZA KITANZANIA PENGINE MTU MMOJA TU NDIE ANAEFANYA KAZI LAKINI ANAWAJIBIKA KULISHA NA KUTOA HUDUMA ZA JAMIII KWA KAYA ZAIDI YA TATU ZENYE WATU WASIOPUNGUA KUMI KATIKA KILA KAYA (MTU MMOJA ANAHUDUMIA FAMILIA YAKE YA MKE/MUME NA WATOTO, ANAHUDUMIA PIA FAMILIYA YA WAZAZI WAKE, WAKWE ZAKE NA ANAWAJIBIKA PIA KUTOA MICHANGO YA MAENDELEO YA JAMII IKIWEMO HARUSI, NK...) HALI HII INAWAFANYA WATANZANIA WENGI WAISHI MAISHA MAFUPI KUTOKANA NA MARADHI YANAYOWAPATA WAKIWA BADO VIJANA....NA HATA WAKIENDA KUTAFUTA HUDUMA ZA AFYA, KILE WANACHOKATWA HAKIONEKANI KUPELEKWA HUKO ILI KIWASAIDIE KUWATIBU..
   
 2. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2011
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  hakuna kinachoniumiza moyo kama kodi ya mapato aisee!!!
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  dawa ni kujiajiri

  kuajiriwa nchi hii ni upumbavu saana
   
 4. s

  sanjo JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Ni mbaya sana kulipa kodi wakati manufaa yake huyaoni. A Tax system should bring in equity and fairness to taxpayers.
   
 5. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Kodi inaliwa na Kikwete katika safari zake, mnafikiri nani anafadhili Safari zake kama sio wewe kufanyakazi
   
 6. babuwaloliondo

  babuwaloliondo JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 378
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mtazamo wa maisha yetu watanzania unamatatizo makubwa, kwa umaskini wetu tutaendelea kuwa maskini mpaka tutakapobadilika.
  Haiwezekekani mtu uwe na watoto 5 wakati huo unategemee ndugu wakusaidie, wakati unalipuwa unakula raha ukiwatafuta, hukuomba kusaidiwa matokeo yake ndio haya.
  Watu wengi wamebebeshwa majukumu yasiyo yao, na hicho ndio chanzo cha matatizo yote.
  Working class are paying so much in this country, na hao ambao unawasaidia wengi ndio wanaohongwa t-shirt na kofia na wafuja kodi zetu wa magamba.
  in general working class are the most exploited people in this country kuliko hata wananchi wanaolala njaa, na wengi ndio wanataka mabadiliko, ila kinachoumiza ni unaowasaidia hawaelewi wapowapo tu na kuchukuliwa na malori kusikiliza uongo wa kina 6 na nape.
   
 7. P

  Parachichi JF-Expert Member

  #7
  Jul 17, 2011
  Joined: Jul 22, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  paye ni muhimu kwa kila nchi!ila hapa kwetu rate yake ipo juu sana!tupiganie jamaa wapunguze tax rate!
   
 8. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #8
  Jul 17, 2011
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  ni vizuri sana lkn haiwezekani kila mtu ajiajiri, wapo watakaoajiriwa na malalamiko kama haya hayataisha BOSS
   
 9. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #9
  Jul 18, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mkuu, bado hata ukijiari kwa mfiumo wa maisha yetu ya kitanzania, huna guarantee ya kuendesha maisha. Hata wafanyabiashara ambao wameajiri wana machungu makubwa pengine unatakiwa ukiuke sheria na taratibu ili uweze kufanikisha ajira binafsi kwa mfano kukwepa kodi, kuwalipa mishahara midogo wale wanaokusaidia nk. Lakini kwa kuwa tunaishi katika mfumo wa kutegemeana kama kupe (mutually defendants), inakuwa vigumu pia kufanikiwa, inakupasa utokwe jasho la kutosha kulisha familia zetu za utegemezi wa mabehewa ya "TRENI"
   
 10. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #10
  Jul 19, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Kuna haja ya kutazama upya mfumo wetu wa ajira; kweli wapo wanoumia sana na wapo pia walio peponi
   
Loading...