KERO YA VIPAZA SAUTI MISIKITINI NA MAKANISANI

KERO YA VIPAZA SAUTI MISIKITINI NA MAKANISANI

Neno la Mungu lazima litangazwe kwa namna zozote zile. Sahivi unayaona kero ipo siku utatamani uyasikie japo dakika moja tu ila haitawezekana.. Haya maisha ukiwa mzima wa afya unakua na kiburi flani rohoni

Mkuu ww utakuwa ni sheikh lazima, sio kwa utetezi huu. Usilazimishe kila mtu kuwa kwenye ibada yako maana kwa wengine ni kero tu. Anayetaka hiyo offer ya kwenda mbinguni kupitia nyumba ya ibada atakuja huko ndani kupata huduma.
 
Mkuu bora hao waislam kuna wakolokole wanapiga kelele usiku kucha halafu maneno yasioeleweka utaskia sabagaraga gahsndbnsika natamani nitoke nirushe mawe siku nyingine hawazid watatu lakin balaa lake mtaani sio dogo.

Bwaahaa bwahaaa nimecheka vibaya sana. Halafu unakuta wamevaa nguo zimechakaa lakini zimefuliwa vibaya sana. Kisha wana sauti (tone) fulani ya kama ya kizungu, wenyewe huiita sauti ya kiutumishi. Nilikuwa nakaa nyumba moja ya kupanga wakawa ndio zao mida ya usiku, siku hiyo nikawatolea uvivu. Wakaanza kuniombea eti mimi ni pepo, ilibidi mwenye nyumba na wapangaji wengine wanunue ugomvi, kumbe ni tabia iliyokuwa inakera wengi japo walikuwa wanaoogopa kuwaambia wasije kosa kwenda mbinguni.
 
nadhani hili jambo ndio linatakiwa lifuate baada ya mifuko ya rambo

Kweli kabisa, na sasa hivi kuna walokole huwa wanaingia kwenye mabasi na kuanza kuhubiri mambo yao ya dini utadhani ni mabasi ya Yesu. Kama mtu anahitaji hiyo huduma ya injili ataifuata huko huko kanisani.
 
Hivi mambo Dini, unaweza kutoa mfano wa Ulaya, kule ni mtu mmoja ndiye huabudu, hawana mtazamo kama jambo la kijamii.

Ndiyo maana wakapitisha sheria kuoana watu wa jinsiya moja, kule wanaume kwa wanaume kulana Denda hadharani siyo kosa, ila kumtaja Mungu hadharani ni kosa.

Acha upotoshaji dogo, kwani huko ulaya mambo ya jinsia moja unalazimishwa? Kuna popote kwamba huko Ulaya umesikia kumtaja Mungu ni kosa? Kaeni misikitini au makanisani muhubiriane mnaotaka,sio imani zenu muhubirie hata wasiotaka hiyo huduma.
 
Suala la kelele zinazozalishwa na vipaza sauti kwny nyumba za ibada ni kukosa maarifa ya ustaarabu. Na haiishii hapa tu angalia hata kwny maharusi, bar, na sherehe zote...... waafrika tuna hii kasumba ya kufunga maspika na sauti kubwa na ni kero kero kerooo.

Sio kila cha wa magharibi ni chema ila kwa hili wametuzidi mbali. Makanisa na misikiti yote hairuhusiwi kutoa sauti za ibada nje, watu wanaabudu kwa ukimya na ustaarabu wa hali ya juu.

Uhuru wa kuabudu ndio tunao kisheria lakin kuexercise haku zako kisheria inaendana na level ya ustaarabu. Yakitolewa maspika misikitini na makanisani bado tunaweza kuendela kuabudu vzuri tu bila shida.
 
Kwa umri wangu naweza kuwa sawa na Baba yako, kwa usidhani ni mtu wa kuniita hivyo.

Kuto lazimisha hakuondoi utambuzi wa mahusiano ya jinsia ya aina moja, Tanzania ndoa ya jinsia moja ni halali na inatambuliwa na serikali je, wanalazimisha kuona.

Unapojibu hoja ya mtu jibu kwa hoja, huna hoja pita kimya, kumbuka jina la forums hii ni jamii forums, ndiyo maana tunaitana "mkuu" hakuna anaemwita mwinzie bwana, dogo, hata mpwa.

Hutuonani nguvu ya kuniita dogo inatoka wapi, leo tupo mbande mbili tofauti, kesho tunaweza kuwa upande mmoja wa mada.

Ni huko facebook peke yake watu huandika maneno ya kuwaudhi wengine, Samahani kwa kukwaza ila umri wangu inaniambia niwe nitangulize busara.
Acha upotoshaji dogo, kwani huko ulaya mambo ya jinsia moja unalazimishwa? Kuna popote kwamba huko Ulaya umesikia kumtaja Mungu ni kosa? Kaeni misikitini au makanisani muhubiriane mnaotaka,sio imani zenu muhubirie hata wasiotaka hiyo huduma.
 
Kwa umri wangu naweza kuwa sawa na Baba yako, kwa usidhani ni mtu wa kuniita hivyo.

Kuto lazimisha hakuondoi utambuzi wa mahusiano ya jinsia ya aina moja, Tanzania ndoa ya jinsia moja ni halali na inatambuliwa na serikali je, wanalazimisha kuona.

Unapojibu hoja ya mtu jibu kwa hoja, huna hoja pita kimya, kumbuka jina la forums hii ni jamii forums, ndiyo maana tunaitana "mkuu" hakuna anaemwita mwinzie bwana, dogo, hata mpwa.

Hutuonani nguvu ya kuniita dogo inatoka wapi, leo tupo mbande mbili tofauti, kesho tunaweza kuwa upande mmoja wa mada.

Ni huko facebook peke yake watu huandika maneno ya kuwaudhi wengine, Samahani kwa kukwaza ila umri wangu inaniambia niwe nitangulize busara.

Kwanza pole kwa kukuita dogo, nisamehe kwa hilo, lakini hiyo dogo imekuja baada ya ww kusema kumtaja Mungu huko ulaya ni kosa. Utumie umri wako vizuri bila kuleta upotoshaji kuepuka kuonekana umri wako ni mdogo.
 
Unajua unapotaka ku quote mtu, angalia alikonzia huko juu. Mimi nimeandika hivyo kwa sababu kuna membar alieandika, kuna Muhubiri wa Dini huko London alikamatwa na polisi akihubili, kwamba kule huhubili ni kelele.

Ndipo nikaandika vile, hata hivyo hatakama hupendezwi na alichoandika anaetetea hoja kwa upande kinzani, hutakiwa kumwandika Lugha ya kuudhi.
 
MBONA HAMSEMI HAYO MASPIKA YANAYOTANGAZA BIASHARA KILA DUKA HUKO KARIAKOO NAYO NI KELELE MBONA HAMSEMI WALE WANAOPITA NA MASPIKA KWENYE MKOKOTENI INAPINGA NYIMBO ZA INJILI MPAKA KERO MUISLAM AKIFANYA HIVYO ATAAMBIWA HANA KIBALI UTAMKUTA MTU KANUNUA SPIKA LAKE KUBWA NA MIKE ANASIMAMA PEMBENI YA BARABARA ANAHUBIRI KELELE NYINGI HIYO AKIFANYA MUISLAMU SWEKA NDANI HUNA KIBALI
 
Umasikini ndio chanzo cha matatizo yote haya.
Sasa hivi mitaani kila kona kuna mashindano ya kujenga misikiti na makanisa na lengo kuu wala sio kuwajenga watu kiimani bali ni kuwageuza waamini wao kua chanzo cha mapato (ujasiria dini).
Misikiti na makanisa yenye lengo la kuwajenga watu kiimani hua hawana mambo ya kipuuzi na kuwaudhi majirani wanaowazunguka (maana dini zote hizo zimefundisha ubaya wa kumuudhi jirani) nyumba nyingine kuna watoto, wagonjwa, wazee ambao wanahitaji muda wa kupumzika lakini wao wanakua kikwazwo.

watu wanazidi kujenga misikiti na makanisa kwa sababu waumini wamekuwa wengi kwa hiyo haitoshi pili zama za makufuli watu hawana pesa za kuchezea kulewea kuhongea wameamua kurudi misikitini na kanisani kufanya ibada
 
Ndugu zangu Waislamu na Wakristo kuna ulazima gani kuweka vipaza sauti nje ilihali ibada mnafanyia ndani!!?.... spika za ndani pekee zinatosha kuendesha ibada zenu , ningeomba mamlaka husika iliangalie hili

Napendekeza muito(adhana) pekee ndo utumike kwenye kipaza, zaidi ya hapo ni usumbufu kwangu mimi nisiyehusika na ibada zenu

kama watu mshawaita na tayari wameingia ktk nyumba ya ibada, hakuna ulazima wa kuendelea kuiachia sauti ya nje inisumbue mimi

Asante naimani mtajirekebisha ndugu zangu wakristo (baadhi) na Waislamu View attachment 1118084
Kwa sisi wakristo au wagalatia kama walivyotubatiza ndg zetu wachungaji na mitume na manabii inaonekana kuna ushindani maana kanuni zinasema 10% unayotoa ile ni ya Mchungaji au Nabii au mtume sasa spika lazima itatumika.kuvuta kondoo.

Sijujua kwa wenzetu waislamu10% ya zaka anakula nani lakini inaonekana motisha ya spika ni mwito wa kusisitiza ibada, ila inachanganya zaidi pale spika moja sauti inakutana na spika ya msikiti mwingine.

hapa nianpoishi Goms makanisa 3 msikiti 1 na bar ya nyumbani ya kibosile moja vyote full speaker ijumaa ndio balaa.
 
Mkuu mbona kumbi za starehe zinazopiga mziki wa kero umezisahau?

Kero kubwa mitaani na watu hata kutamani kuuza na kuhama makazi yao waliyojenga karibu na nyumba za ibada ama kumbi za starehe, ni hizo kero.

Miziki, mahubiri katika ibada kwa kutumia vipaza sauti kwa madhehebu yote na mikesha ya walokole ni kero kubwa isiyomithilika.

Hapo bila kutungiwa sheria lazimishi kama hii ya kukomesha matumizi ya mifuko ya 'rambo', kero hii itaendelea kuumiza jamii isiyo na hatia.
 
watu wanazidi kujenga misikiti na makanisa kwa sababu waumini wamekuwa wengi kwa hiyo haitoshi pili zama za makufuli watu hawana pesa za kuchezea kulewea kuhongea wameamua kurudi misikitini na kanisani kufanya ibada
Sawa warudi kufanya ibada ila viongozi wao watambue kua hayo majengo yao ya ibada yamezungukwa na nyumba za watu, hivyo wanapaswa kuwatendea wema majirani zao kwa kua mafundisho ya dini zote yamehimiza katika kutendeana wema.
 
Sijui kwa walioishi nje, labda watupe uhalisia wa mambo huko

Nimekaa Dubai kwenye waislam na misikiti mingi husikii adhana kwenye vipaza sauti hadi unaweza kudhani hakuna misikiti. Ni wastaarabu sana. Tatizo sisi watu weusi tunajipendekeza sana kuliko wenye dini zao
 
Astaghfirullah, Mwenyezi MUNGU Atusamehe hatujui tulitendalo.
 
Back
Top Bottom