KERO YA VIPAZA SAUTI MISIKITINI NA MAKANISANI

KERO YA VIPAZA SAUTI MISIKITINI NA MAKANISANI

Ndugu zangu Waislamu na Wakristo kuna ulazima gani kuweka vipaza sauti nje ilihali ibada mnafanyia ndani!!?.... spika za ndani pekee zinatosha kuendesha ibada zenu , ningeomba mamlaka husika iliangalie hili

Napendekeza muito(adhana) pekee ndo utumike kwenye kipaza, zaidi ya hapo ni usumbufu kwangu mimi nisiyehusika na ibada zenu

kama watu mshawaita na tayari wameingia ktk nyumba ya ibada, hakuna ulazima wa kuendelea kuiachia sauti ya nje inisumbue mimi

Asante naimani mtajirekebisha ndugu zangu wakristo (baadhi) na Waislamu View attachment 1118084
ili twende sawa na bar zisipige muziki kwa kuwa kuwa bar wengine ni ibada na inawakera watu pia.
au wakati mwingine bar muziki wa dansi unakesha usiku mzima hii imekaaje na bar haina sound proof!
hakuna haki bila wajibu.
 
Mbona Ulaya ukiwa ulaya huwezi kusikia sauti ya pub, adhana ya msikiti wala sauti za walokole[emoji113][emoji41]
Ndugu zangu Waislamu na Wakristo kuna ulazima gani kuweka vipaza sauti nje ilihali ibada mnafanyia ndani!!?.... spika za ndani pekee zinatosha kuendesha ibada zenu , ningeomba mamlaka husika iliangalie hili

Napendekeza muito(adhana) pekee ndo utumike kwenye kipaza, zaidi ya hapo ni usumbufu kwangu mimi nisiyehusika na ibada zenu

kama watu mshawaita na tayari wameingia ktk nyumba ya ibada, hakuna ulazima wa kuendelea kuiachia sauti ya nje inisumbue mimi

Asante naimani mtajirekebisha ndugu zangu wakristo (baadhi) na Waislamu View attachment 1118084
 
Ume andika nini?
naijatwittersavages-20190605-0002.jpeg
 
Unachoshindwa kujua ni kuwa Sheria London Uingereza, Siyo sheria Dar es alaam Tanzania. Uingereza Ushoga halali Tanzania ni kosa, Mbezi mwisho kuna muhubiri kila siku yupo pale alfajili kuwahubiria wasafiri na mambo ya kwenda.
Kuna muhubiri mmoja toka Nigeria alikamatwa jijini london akiwa ana hubiri, Polisi walimwambia analeta usumbufu, angalia hii
 
nadhani hili jambo ndio linatakiwa lifuate baada ya mifuko ya rambo
 
Kwa mantiki hiyo,hata adhana haina haja ya kutangazwa kwenye kipaza sauti kila wakati.

Kwani adhana haiwezi kufanyika bila maiki?
Hivi unaelewa maana ya adhana?
Au mnakurupuka tu.
Adhana ni dakika 1 tu na makanisa yanapiga disko usiku kucha.
 
Mbona Ulaya ukiwa ulaya huwezi kusikia sauti ya pub, adhana ya msikiti wala sauti za walokole[emoji113][emoji41]
Hivi mambo Dini, unaweza kutoa mfano wa Ulaya, kule ni mtu mmoja ndiye huabudu, hawana mtazamo kama jambo la kijamii.

Ndiyo maana wakapitisha sheria kuoana watu wa jinsiya moja, kule wanaume kwa wanaume kulana Denda hadharani siyo kosa, ila kumtaja Mungu hadharani ni kosa.
 
Umasikini ndio chanzo cha matatizo yote haya.
Sasa hivi mitaani kila kona kuna mashindano ya kujenga misikiti na makanisa na lengo kuu wala sio kuwajenga watu kiimani bali ni kuwageuza waamini wao kua chanzo cha mapato (ujasiria dini).
Misikiti na makanisa yenye lengo la kuwajenga watu kiimani hua hawana mambo ya kipuuzi na kuwaudhi majirani wanaowazunguka (maana dini zote hizo zimefundisha ubaya wa kumuudhi jirani) nyumba nyingine kuna watoto, wagonjwa, wazee ambao wanahitaji muda wa kupumzika lakini wao wanakua kikwazwo.
 
Ni kero sana...

Vipaza sauti muda wote...

Wale wa kupiga mangoma ukiku kuja kama live band...


Cc: mahondaw
 
Ni kweli kabisa ila kuna vitu vyengine ni UNTOUCHABLE. Ukichezea dini hakuna mtu atakaekupenda katika maisha hata wasio na dini pia watakuchukia (wengine wana maslahi nazo ya kidunia). Dini ni nature ya ulimwengu ambayo kamwe huwezi kuipitia kwa mbele na kuikinga, we tulia tu na uvumilie tu hiyo life span yako ya miaka inayoishia na 60, ili ukifa ukalale mahala pema peponi ameen!
 
Mada za namna hii hazijawahi kumpata mshindi wa moja kwa moja; zaidi tu ya watu kuparuana kwa misingi ya imani zao. Binafsi napitia changamoto kama hizo ninapokua ugenini tu! ila ninakoishi (kwenye makazi yangu ya kudumu) nimejitahidi kujitenga kabisa na hizo nyumba za ibada ili tu kuepukana na changamoto za aina hiyo.
 
Kweli ndugu mfano misikiti na makanisa inaanzishwa kiholela
Umasikini ndio chanzo cha matatizo yote haya.
Sasa hivi mitaani kila kona kuna mashindano ya kujenga misikiti na makanisa na lengo kuu wala sio kuwajenga watu kiimani bali ni kuwageuza waamini wao kua chanzo cha mapato (ujasiria dini).
Misikiti na makanisa yenye lengo la kuwajenga watu kiimani hua hawana mambo ya kipuuzi na kuwaudhi majirani wanaowazunguka (maana dini zote hizo zimefundisha ubaya wa kumuudhi jirani) nyumba nyingine kuna watoto, wagonjwa, wazee ambao wanahitaji muda wa kupumzika lakini wao wanakua kikwazwo.
 
Kiukweli kuna maeneo wamezidi,
Bora nikirudigi kwetu Iringa, Ndugu zangu waislamu si wasumbufu
 
Kwa mantiki hiyo,hata adhana haina haja ya kutangazwa kwenye kipaza sauti kila wakati.

Kwani adhana haiwezi kufanyika bila maiki?
nn maana ya uhuru wa kuabudu? nn maana ya taifa kutokuwa na dini?
 
tena kama walokore hao ndio "warogwa" wa makelele sasa[emoji851][emoji851]
 
Back
Top Bottom