Kimara Mwisho tuna shida kubwa sana ya upatikanaji wa maji safi toka DAWASA kuanzia mtaa wa bakery ni upande wa kushoto ukitokea mjini baada ya msikiti kwenda Stopover.
atizo hili ni la muda mrefu sana toka January hadi sasa, maji tunapewa mara moja kwa wiki yaani Jumatatu tuu.
Hapa toka wiki iliyopita hatujapata maji hadi leo, tumetoa taarifa DAWASA Kimara, bila msaada wowote.