Kero tunazokumbana nazo kwenye usafiri wa umma

Luqman mohamedy

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
892
1,226
Mara nyingi watumiaji wa usafiri wa umma tumekuwa tukikumbana na kero mbali mbali kutoka kwa wamiliki mpaka abiria wenzetu ambazo hazitatuliki, sababu nyingi zinalindwa na uhuru wa kikatiba kwani katiba zetu hueleza halali na haramu ila neno 'inakera' hazielezi. Na hii hapa ni moja wapo ya kero hizo:

KWENYE DALADALA NA MABASI.
(1)Kuangalia video au kusikiliza radio kwenye simu binafsi kwa sauti. Baadhi ya wenzetu wamekuwa na tabia hii sasa sijui ni ushamba au wanaamini wanachosikiliza kila mtu anakipenda au vipi??
Utakuta mtu anaaangalia livideo la mziki kwa sauti au speech za mahubiri kwa sauti kubwa huu ni ushamba jamani.

(2)Kulalia abiria mwenzio ukisinzia nayo ni kero aisee. Kama una usingizi tunakushauri uegemee magoti sio kulalia mabega ya abiria mwenzio akusukume sukume kila muda na bega.

(3)Kupiga simu na kuponda wenzio hata kama hatuwajui, kuongea ongea uongo wa sehemu ulipo kwa sauti hata kama haituhusu mnatukera ndugu zetu.

(4)Kuongea kwa sauti story zenu ambazo hazituhusu, kweli ni public car ila kwa kelele hizo msitunyime amani wenzenu. Utakuta mtu anacheka kwa makelele ni ile basi ana uhuru tu.

(5)Kwa wamiliki mabasi kuweka mziki kwa sauti kubwa au kuweka video za dini kwa wale wa mabasi ya mikoani ni kweli mna uhuru ila tunatofautiana itikadi mtusamehe.

Kwa ndugu zetu wa bajaji na boda boda hii habari ya kulazimisha story wakati mnatuendesha huwa mnatueka roho juu aise.
Utakuta mtu anaongea mpaka anawageukia njia tuangalia sisi, usukani kashika yeye. Kwani kijiweni huwa mnapigaga story gani mpaka mtulazimishie abiria, story zenyewe kusikia hatusikii tunaitika tu aah nima. Mtatuuua.

Wale wenzangu wa ndege za economy kero zetu kawekeni kwenye ukurasa wa ATCL
 
Back
Top Bottom