Kero: Tabia ya kurundika/kumiliki vitu vingi kuzidi uwezo wa kuvimudu au kuvitunza

Samwel Ngulinzira

JF-Expert Member
Aug 5, 2017
1,829
1,958
Habari ya wakati huu wakuu?

Naomba nijielekeze moja kwa moja kwenye hii tabia ya watu kupenda kumiliki vitu vingi visivyotumika. Nitavitaja kimoja kimoja lakini sioni mantiki ya wao kufanya hivyo kwa sababu wakati mwingine huishia kutengeneza uchafu.

1. Mabegi/mafurushi makubwa kwenye safari
Utakuta safari ni ya siku tatu lakini kafungasha begi ambalo hata hawezi kulibeba. Yaani kwenye begi kaweka vitu au nguo ambazo hawezi kuzitumia kwenye hiyo safari yake.

2. Makabati makubwa na vyombo vingi
Hapa sasa ndio vita ilipo. Unakuta familia ya watu wanne wana kabati la vyombo milango mitatu, vyombo navyo ni vingi sana. Unakuta kuna vyombo havijawahi kutumika karibia mwaka mzima, ukiuliza kwa nini utaambiwa ni vyombo vya wageni. ushauri wangu kama una familia ndogo weka kabati la mlango mmoja lenye vyombo vichache au makabati ya jikoni pekee yanatosha.

3. Kukaa na vitu visivyotumika
Sambamba na hilo kuna kasumba ya kurundika vitu visivyotumika ndani ya nyumba au chumba. Ninaamini kukaa na kitu ambacho hukitumii ni matumizi mabaya ya nafasi.

Unakuta mtu una godoro ambalo haulitumii ummelikunja limekaa kabatini. Una nguo ambazo hujazivaa miaka miwili ila zinakujazia kabati.

4. Kupenda kujenga majengo makubwa kuliko uwezo au kuliko idadi ya wanafamilia
Sijajua hasa target ya kufanya hivi hua ni nini, unakuta mtu umejenga nyumba kubwa ambayo hata kuimalizia umeshindwa. Unajenga nyumba ambayo huna uwezo wa kufanya usafi badhi ya sehemu.

Matokeo yake unalazimika kuwa na wasaidizi kama wawili ili kuifanyia usafi, au wakati mwingine ukarabati unakushinda kwa sababu ya gharama kubwa ya ukarabati.

5. Mrundikano mkubwa wa vitu ndani ya nyumba
Unakuta nyumba ina fenicha nyingi kupitiliza kiasi kwamba baadhi ya fenicha zinachakaa au muonekano wake unakua ni wa kizamani sana. Kutokana na uwingi wake inakua ngumu kuziboresha. Au mpangilio wa vitu unafanya nyumba ikose mvuto.

6. Kufanya sherehe kubwa kuzidi uwezo
Unakuta mtu anafunga ndoa anaandaa sherehe kubwa kuliko uwezo wake. Matokeo yake baada ya sherehe inakua ni dhiki kuu. Madeni kama yote mbali na madeni ndoa za siku hizi hazikai sana unaishia kupata stress.

7. kitanda kikubwa kuliko ukubwa wa watumiaji
Hapa napo siku hizi ni changamoto, unakuta mtu mwili mdogo lakini anataka kulala kwenye 6 kwa 6. wakati wangeweza kulala ata kwenye 4 kwa 6 na chenji ikabaki.

Ushauri wangu
Napendekeza watu wawe na vitu muhimu tu. Vitu visivyohitajika ndani ya nyumba visitumike. Usikae na fenicha zisizokua na kazi kwa mawazo kwamba kuna siku kitapata kazi. Pangilia mambo yako vizuri, kuwa na vitu vichache unavyoweza kuvimudu na kuvitunza. Kwa mfano vyombo vya ndani viwe angalau mara tatu ya idadi ya wanafamilia. Kwa mfano familia ya watu wan ne muwe na sahani 12 tu. Kukaa na vyombo ambavyo vinaweza kumaliza miezi 6 bila kuoshwa ni uchafu.

Tumia vyombo vikiisha ondoa nunua vingine, furahia maisha. usiishi maisha ya gharama kuzidi uwezo wako. ukipata wageni wakirimu kwenye vyombo vya kila siku, tusiishi maisha feki, tuishi uhalisia wetu.

Nawasilisha.

download.jpg
 
Njoo hapa mtaani kwangu kuna jamaa kila nikipita naye mahali utasikia na hiki ni kiwanja changu. Badala amalize kuendeleza kiwanja kimoja yeye amekazana tu kuongeza vingine, sasa kamahia kununua mashamba.
 
Njoo hapa mtaani kwangu kuna jamaa kila nikipita naye mahali utasikia na hiki ni kiwanja changu. Badala amalize kuendeleza kiwanja kimoja yeye amekazana tu kuongeza vingine, sasa kamahia kununua mashamba.
Duh! Hii hatari sana, inaweza kufikia kipindi akashindwa kuvimudu ata kupalilia majani.
kitu muhimu ni kuwekeza nguvu kwenye kuvimalizia halafu ndio aongeze viwanja vya ziada.
 
7. kitanda kikubwa kuliko ukubwa wa watumiaji
Hapa napo siku hizi ni changamoto, unakuta mtu mwili mdogo lakini anataka kulala kwenye 6 kwa 6. wakati wangeweza kulala ata kwenye 4 kwa 6 na chenji ikabaki.
😂😂😂😂😂😂 Ila we jamaa umewachoka kweli, kwani hutaki wajimwayemwaye wanapostarehe na usingiz wao?

By the way hizi concept za kiminimalistic zinapunguza stress ndogondogo zitokanazo na kuigaiga.

Mi mwenyewe minimalistic kwa baadhi ya vitu mfano vyombo na nguo, inaondoa stress za kufua na kuosha. Inajicheck and balance kiotomati
 
Njoo hapa mtaani kwangu kuna jamaa kila nikipita naye mahali utasikia na hiki ni kiwanja changu. Badala amalize kuendeleza kiwanja kimoja yeye amekazana tu kuongeza vingine, sasa kamahia kununua mashamba.
😂😂😂😂
 
Yote umeandika correct mkuu,Kila kitu tuwe na kias.....mi Kuna muda vikinizidia ndan nakusanya navimwaga usiku kwenye mtaa wenye watu wenye mahitaji zaidi yangu nikipita kesho yake hakuna kilichosalia.Nilikuwa na tabia ya kugawa nguo kilichonipata🙌 so sikuhizi ndo nafanya ivo
 
Yote umeandika correct mkuu,Kila kitu tuwe na kias.....mi Kuna muda vikinizidia ndan nakusanya navimwaga usiku kwenye mtaa wenye watu wenye mahitaji zaidi yangu nikipita kesho yake hakuna kilichosalia.Nilikuwa na tabia ya kugawa nguo kilichonipata so sikuhizi ndo nafanya ivo
Kilikupata nini mkuu?.
Nami nina tabia hiyo ya kugawa nguo kila baada ya mwaka.
 
Back
Top Bottom