Kero: Sauti TBC1

Mutensa

JF-Expert Member
Feb 20, 2009
421
90
Wadau,
Heshima mbele. Wajameni suala la sauti ya TV yetu ya taifa TBC1 linakera. Kimsingi wale ambao ni wapenzi wa kuangalia television hiyo, mtakubaliana na mimi kuwa sauti inashuka halafu baadae inapanda ghafla sana. Nashauri wahusika walishughulikie suala hili mapema sana ili kuondolea kero watazamaji wao.
 
Ni kweli kabisa!!!

Kinachonikera zaidi ukiwa unaangalia TBC1 hata taarifa ya habari unatakiwa kuwa na remote karibu. Kuna nyakati sauti inapanda sana na kuna nyakati inashuka sana. Hii ni ovyo kabisa.
Najiuliza, wataalamu wote wanini katika kukifanya kipindi kirushwe ikiiwa mambo yenyewe ndiyo hayo. Maana utaona orodha; mtangazaji, muaandaaji,msimamizi, fundi mitambo, mhandisi wa sauti, nk.

Tatizo jingine TBC1 walilonalo ni kuwa wagumu wa kutendea kazi ushauri wanaopewa na wateja wake. Nilikwisha wahi kuwapa ushauri constructive ili huduma wanayotupa iwe njema hasa katika masuala hayahaya ya sauti.Matokeo zero.
 
Nadhani hawa jamaa wanatemebelea Jamvini walirekebishe hili. Pia kuna baadhi ya watangazaji hasa wale wa soka huwa wanapenda kuingiza mambo yao binafsi au kuongelea jambo wasilokuwa na uelewa wa kutosha hadi ina bore.
 
Sauti huwa inapanda kuwa kero hasa wanapoweka lile tangazo lao kuwa TBC1 inapatikana kila mahali etc
 
Kwa kweli TBC pamoja na matatizo hayo lakini wanajitahidi sana, maana taarifa yao ya habari naipenda zaidi kuliko ya vituo vingine. Actually nafikiria kumfikisha TIDO mahakamani kwa kudanganya umma maana wakati anapewa ukuu wa TBC alisema tumpe miaka miwili au mitatu wenyewe tutaipenda TBC. Hivyo mm nilikuwa nasubiri hiyo miaka ipite ndo nianze kuangalia TBC1. Sasa mwaka jana December kwa bahati mbaya nika tune TBC 1 duu ubora ule niliouona sikuamini tangu siku hiyo naangalia taarifa ya habari ya TBC1 na hata vipindi vingine. Nataka nimshtaki TIDO kwa kuninyima huo uhondo maana nimekosa mambo mengi ya TBC1........

Pia kuna watangazaji wawili wa michezo Enock Bwigane na Pendaeli Omari wale vijana ni wazuri sana tena - nawapa hongera vijana kazi yenu ni nzuri

Ushauri: TIDO najua unatembelea hapa, tafadhali zingatia maoni ya wadau mbalimbali- tuko pamoja
 
Hata hivyo vingine ni vizuri sana tu. Tofauti ni hiyo TBC 1 kutumika na mafisadi na hiyo kero.
 
Last edited:
Tatizo jingine pia ni kwamba sauti inachelewa na haindani na midomo wakati mtu anazungumza. Check na suala hili pia.

Nilijaribu kuwaulizia wakasema mitambo yao imechoka, so inabidi fungu litolewe wanunue mipya.
 
Tatizo ni seting zao kwenye input wanaweka audio ktk level ya juu na wakati signal from the source inakuwa juu mpaka hapo lazima sauti iwe mbaya inayokoroma.
Au unakuta mikono mingi kwe mixer zao.
 
TBC kodi hawalipi hata sula la sauti linawashinda? Tafadhali fanyeni marekebisho husika kombe la Dunia tusiadhirike. Sawli langu dogo ni - je hawawezi kuwapa TV zingine sehemu ya matangazo?
 
Kwakweli hapo ni balaa tupu. Yaani ni kelele za ajbu. Mimi mwanzoni nilikuwa nafikiri ni TV yangu ina matatizo,,, kumbe ni hawa TBC1 wenyewe.
Kwa kweli ni kero kubwa sanaaaaaa...

TIDO MHANDO, TUNAKUAMINI SANA KWA UTENDAJI BORA NA UAJIBIKA. TAFADHARI SANA TUNAKUOMBA UWAJIBIKAJI KWA HILO....
 
namuunga mkono mchangiaji mmoja hapo juu, ni kweli mara nyingi sauti na mdomo haviendani na hilo ni kero sana.naomba washughulikie tatizo hilo.akhsante.
 
Back
Top Bottom