Kero kero kero!

Pole Bishanga kama haya yota uliyotaja yanamuhusu muhusika mmoja, ila navyojua mimi hayo uliyotaja kuna kila mwanamke linamhusu in one way or another, tumekusikia tutafanyia kazi na kujirekebisha tuwe wake wema.Thanx kwa kutukumbusha
 
Hapo Bishanga umeongea kweli kabisa.
Sisi wanawake tunazo hizo tabia na mimi nakiri na ninaoba wanawake wenzangu tujirekebishe ili kunusuru mahusiano yetu. ILA SASA HAPA JF BADALA YA WADADA KUCHANGIA UTASIKIA WANA COMMENT SIYO WANAWAKE WOTE. NYIE KILA KITU KIBAYA MNAKUWA NDO TOFAUTI NA WANAWAKE WENGINE. TOENI COMMENT NINI KINATUFANYA TUWE HIVYO AND NOT CHEAP TALKS LIKE SIYO WOTE. I HATE THOSE FLUFFY TALKS

Hai wewe noti inaf mbona watunanga hivi? hujambo lakini? neiba?
 
Hai wewe noti inaf mbona watunanga hivi? hujambo lakini? neiba?

Sijambo jamani Gaga, Jirani kaamua mpaka kubadilisha njia watu walichonga sana JF na ninahisi nae ni MDAU humu ndani. Ila Alunta Continua
 
Pole kaka, Mungu akusaidie utulize hasira kwa afya yako mwenyewe.
Ndo maana Imeandikwa Wanaume wanatakiwa waishe na wanawake kwa akili.
Tumia akili ya kiume kukabidhiana na hayo!!!!!!!
 
Mwe! Pheeeeewwwww! Labda nifikirie kujibu la kuongea sana. Sie tumeumbwa hivyo mwayego. Tuna idadi kamili ya maneno ya kuongea kwa siku, sasa we unataka tusiongee? Tukiongea sie twataka kusikilizwa tu na sio lazima utoe solution ya tunayoongea. Hapo nadhani hujatuelewa tukoje, hatufanani na yie namna tunavyofikiri.... Jaribu kidogo kutuelewa tuu jameniiii.... :behindsofa:
 
Pole sana mkuu, sitapenda kuingia kwenye ubishi wala ushindani (kuwa hizi tabia usiombe awe nazo mume, nisiharibu thread manake ni topic inayojitegemea), ila ni kweli kuwa baadhi yetu tunazo hizo tabia. Ila angalau moja moja kwenye hizo, manake kama zote ndio mama mmoja anajaaliwa nazo, mmh maisha hayawi rahisi. Ila kama alivyosema mdau mmoja, kina mama unatakiwa uishi nao kwa akili na hekima ya hali ya juu....
 
Wadau ahsanteni kwa michango kede kede,nashukuru na kikubwa zaidi asubuhi nimecheki presha imeshuka.Lol mambo magumu sana haya,harusini ukiangalia wanavyomeremeta ,tabasamu hadi gego la mwisho,ngoma ,nyimbo,mavyakula,mipombe,hotuba ndefu,mabusu kwa maharusi unadhani maisha ya ndoa ni kambingu kadogo kumbe mmmhhhh.....
 
Kila kukicha kinamama wana MMU kazi kutusimanga,sasa leo na mimi ngoja niwatolee uvivu.Kinamama mnatukera kwa haya yafuatayo:
1.Utegemezi: Unambeep mmeo/hawara/bf,nini mama?unamuuliza, 'naomba unitumie vocha',sawa nakurushia ya elfu kumi,muda mchache baadae unanibeep,nakupigia 'luku imeisha baba'sasa nambieni hiyo vocha elfu kumi huwa mnampigia nani? au ni kwa ajili ya kupigia umbea,'Eh mwenzangu jana si nikamwona Bishanga anaingia gest',inahusu?
2.Wivu: Mara upekenyue simu yangu,nikirudi nyumbani 'oh ulikuwa wapi' mara 'nani huyo ulimpakia kwenye gari',nikivua nguo mara unuse kufuli langu, jamani ya nini yote haya? mbona sisi hatuwafatilii hivyo?
3.Kununa: Mara unune,mara uvimbe,mara unisonye kwa mbali,nimekukosea nini? nikuuliza husemi kitu,mkoje jamani?
4. Gubu:Hata kama nilikukosea mwaka 1947 na nikakuomba radhi ukajitia umenisamehe ni bure tu,nikikukosea kidogo leo ,utasikia 'oh ndo mana nilikubamba na hausgel'sasa jamani tukio la 1970 unalibebea bango mpaka leo,we umenikosea mangapi mbona huwa sirudii kuyakumbushia?
5.Mnaongea mno: Wanawake mnaongea jamani, pich pich pich pich,du,hamchoki mkaacha na waume/hawara/bf zenu wakaongea?
6.Uvivu: Sasa kuajiri housegirl ndo iwe sababu ya huyo housegirl kufua hadi kufuli zangu,na kibaya zaidi baba akiumwa eti yeye ndo anamkumbusha dawa,chakula anampakulia yeye,halafu mzee akimfanzia mnakuja juu.
7.Ubinafsi: Nikilipa schoolfees za mdogo wako poa tu,paa la nyumba ya shangazi yako likiepuliwa na kimbunga nikatoa pesa ya mabati poa tu,mama yako akiumwa nikampeleka India poa tu,lakini shuhudia mtoto wa dada yangu akose karo nimlipie au nimnunulie ka gari baba yangu mstahafu,huo mziki wake utaukoma,'eh ndo mana hatuendelei sijui nini sijui nini' lol!
Ngoja nipumzike kwanza ntarudi baadae,nina hasira flan hivi.


Kumbe wewe ni kaka
 
Back
Top Bottom