Hii Funga kazi : Mapenzi mazuri kwa Mabinti wa Kazi.

Fyafyafya

Member
Nov 30, 2017
53
187
Habari wana Jamii.

Binti wa kazi ni msichana wa umri kati ya miaka 14 hadi 18 ijapo kuwa kuna wengine wamezidi umri huu hadi wengine kabisa kuwa watu wazima; wa mama wa makamo na hadi ma bibi vizee.

Binti wa kazi kwa sasa imekuwa changamoto kuwapata hasa baada ya hii sera ya Elimu bure kwani hapo nyuma mabinti wa kazi walikuwa hasa Standard seven failures au kabisa alieshindwa kuendelea na masomo kwa sabubu ya matatizo mbalimbali hasa ukosefu wa Ada.

Kwa sasa Tanzania kuna changamoto ya Ajira ilopelekea watu wengi kukaa bila kazi na wengine kuhangaika kutwa na usiku kusaka hii ajira kwa njia yoyote iwe haramu ( rushwa) au kwa vyovyote tu poa japo wengine wameamua tu yaishe na wabaki kuwa wategemezi.

Lakini kwa Sasa Tanzania Kazi ambayo unaweza kuipata kirahisi tena kwa kubembelezwa na kunyenyekewa na kutumiwa na nauli bila kujali umbali wa uliko na unakokwenda kufanya kazi hiyo ni kazi ya NDANI yaani u haouse girl.

Lakini kwa asilimia kubwa mabosi wa hawa mabinti wa kazi hutoa malalamiko kibao ya maovu; kasoro; makosa na mapungufu ya hapa na pale ya hawa mabinti wa kazi.

Utafiti haujafanyika kujua undani wa maswala haya na nini ni chanzo. Ama ni mabosi au niwao (mabinti wa kazi) wenyewe.

Hebu kwa leo tuone baadhi ya mambo wewe bosi utayafanya Binti wako wa kazi aipende kazi yake na kumpenda mwanao.

1.Epuka kumpa kazi za kufua Nepi za mavi/puu za mwanao kila siku

Ni kwamba; kumbuka wewe mwenyewe ulivokuwa mtoto mdogo wa umri kama wa huyo binti yako wa kazi ( umri kati ya 14- 18) ulivokuwa unakinyaa cha kugusa au kufua nguo zenye mavi ya wadogo zako. Kama ulikuw huna basi jua wote hawako ivo.

Asilimia kubwa ya watu wengi hasa wa umri huo wana kinyaa sana.

Kumrundikia manguo ya mikojo ; manepi ya mavi na yeye ayafikiche kila hasubuhi na jioni inatia kinyaa sana.

Kumbuka huyo mtoto ulimchukua kwao kwa kazi ya kumlea kumshika / kumwangalia mwanao. Kufua nepi na nguo zingine ni kazi ya ziada tu. Walio wengi hawapendi sana na wanakwazika sana.

Wewe Bossi hata siku moja hujawahi fua nepi za mavi ya mwanao toka aje huyo binti yeye ndo kazi hiyo kila siku tena hasubuhi na jioni kwa mshahara gani?

Wanakereka sana na ndo maana hata nguo/ nepi hizo hazitakati. Nepi ilikuwa nyeupe ndani ya siku tatu imekuwa ya kijivu! Imedina!

Wengine huenda mbali na kuwarundikia manguo kibao za kwao; waume zao na watoto wengine kama wapo! That is not fair!

Kabinti haka utaakuta kamechoka mpaka basi; bado haja fagia na kudeki nyumba; haja safisha choo; hajamlisha lishe mwanao; kama kunawengine wadogo hajawaogesha na kuwavika nguo na bado tena hajapika chakula, du!

Sasa wewe Mama mtoto; hebu jipangie utaratibu wa kufua hizo nguo na nepi zenye mavi/ puu ya mwao.

Kama unafanya kazi; muda mziri kwako ni wa hasubuhi na mapema au jioni unaporudi kazini.

Mruhusu kufua hizo nguo akijisikia na isiwe ndo kazi yake! Ukifanya hivo utamfany mtoto huyo wa mwenzio kujisikia faraja; amani na kuwa na muda mwingi na mwanao na kumpenda.

2. Mwamini na mfanye mmoja wa wanafamilia

Hapa duniani kila mtu anapenda kuona anajaliwa; anapendwa; yeye ni sehemu ya jamii anayoiishi.

Binti wa kazi mwite Mdogo wangu. Na waamru/ wafundishe wanafamilia kama wapo kumwita Dada hasa kwa wa umri wa chini yake. Na yeye pia kukuita wewe Bossi Dada na wa umri wake na wanaomzidi kuwaita ma dada, kaka ma Anko n.k.

Wambie majirani na marafiki zako wote kuwa huyo ni mdogo wako. Ni ndugu yako. Usiwe unasema eti yeye ni binti wa kazi!

Epuka kuonesha hata kidogo utofauti kati ya yeye na wanafamilia wengine. Mwache ajisikie huru.

Mruhusu apike chakula kama anauwezo wa kupika. Na asiwe yeye anapika vyakula vya hadhi ya chini tu kama maharage; mchicha n.k. mruhusu na mfunze kupika hata vyakula vingine kama nyama; samaki n.k. Mruhusu awe huru kupakuwa chakula na kukigawa.

Kama unaona anauwezo wa kumuogesha mwanao na yeye anatamani amwogeshe mruhusu afanye hivo.

Atafanya hivo mara ya kwanza kwa uangalizi wako;mala ya pili na ya tatu na baadae atakuwa ameshazoea kwani utakuwa umeshampa maelekezo na kumfundisha kwa pale ulipoona alikuwa anateleza.

Kama huyo binti ana mwili kama wa kwako na kuna nguo mnazovaliana mruhusu azivae kama anapenda.

kuna nguo ulizozivuka na yeye zinamkaa basi mwachie.

Pengine; mguu wake ni size moja na ya kwako. Basi vaaliane viatu. Weka ukaribu wa kutosha na yeye.

Jaribu kumpa ushauli na kumrekebisha baadhi ya tabia unazoziona hazifai. Mrekebishe freindly.

Kama anamuda wa kutosha yaani yuko free Usimbanie kuangalia Tv na vipindi mbali mbali anavovipenda ila vyenye maadili.

Mpe uhuru wa kushika remote control ya Tv.

Mfanye yeye awe mtu wa tatu katika nyumba. Yaani kuwepo Baba; wewe Mama na yeye awe wa tatu muhimu katika nyumba hiyo. Kama mnaishi wawili basi mfanye awe kila kitu baada ya wewe.

Mfanye yeye awe answerable kwa kila kitu; mpe uhuru wa kutosha isipokuwa tu wa chumbani kwako na mume wako!

Mpe uhuru wa kuwakanya/kuwadhubu wa toto kama wamekosea. Isiwe ile mtoto kakosea na yeye kamwadhibu halafu wewe ukija mtoto huyo anakupokea na mashitaka ya kuadhibiwa. Nawe bila hiana unaanza kumkaripia; kumfokea:"He! kwa nini umempiga mwanangu? amekukosea nini?Unajua uchungu wa Leba?....!!!!! unaanza; Mwanangu amekupiga wapi? ; amekupiga na nini? Unajifanya eti ; Pole Baba ngu/ Mama ngu!!! He! he! he ! Jamani!!! Aibuuuu!!!

Mpe uhuru wa kuongea na kila mtu; majirani na watu wa lika zote. Kuwa na mud wa kutaniana nae; kucheka nae.

Watoto hawa wanapatikana kwa sababu ya matatizo yalowakuta kwao. Kuna historia ndefu tena mbaya ya kusikitisha utaipata ukijaribu kumudadisi na akakwambia. Atakwambia kila kitu kuhusu kwao kwani nyinyi ni marafiki; mnacheka; mmeshibana. Tena utashangaa yeye mwenyewe kaanza kujianika na kusema kila kitu. Kwa mfano: Unaweza ukamsikia akisema ":Hapa tunakula wali kila jioni dah! Raha!! Kwetu wali huliwa christmas tuu!! Na nyama ndo kabisaa hakuna!" Sasa wewe unaweza kuendelea na soga. Mtakuwa marafiki na watani. Atakumisi kama haupo; nawe pia utammisi kama hayupo.

Utamshukuru Mungu kwa kujupa binti wa kazi mzuri ; mwema; wa kila sifa na kujiuliza hivi zile sifa mbaya za mabinti wa kazi mbona huyu hana? kulikoni??

Nae pia atakuwa na amani moyoni. Na kumshukuru Mungu kwa kupata Bosi mwema na familia nzuri yenye upendo. Atakuwa anajiuliza mbona nilikuwa nasikia mabosi wa mabinti wa kazi wana tabia hizi na zile lakini mbona Mama fulani hana? kulikoni!!!

kwami hujawahi kuona familia fulani toka ilipompata binti wa kazi kwa uzazi wa kwanza amekuwa huyo huyo! kamlea mtoto wa kwanza; wa pili; wa tatu; wa nne na wengine .
Alikuja akiwa mdogo na sasa amekuwa mtu mzima. Kapata bwana akuwa pale pale. Na kwa heshima kwa familia hiyo anaamua Mahali wapokee wao!Kichen part inafanikia hapo hapo kila kitu wanagharamikia familia hiyo hiyo na si kwao. Wa zazi wake na ndugu kama wapo wanakuja tu kama wageni walikwa!
Hujawahi kuona familia hizi! kama bado hujaona basi jua zipo tena nyingi!

Wewe mama kuwa na tabiaya kushiriki katika kufanya baadhi ya shughuli za nyumbani kama kuosha vyombo; kufua nguo zako na za mumeo; nguo za watoto wako kama wapo; deki nyumba au choo.

Fanya haya unapo kuwa una muda wa kutosha. Usiwe mtu wa ku kaa na yeye awe mfanya kila kazi.

Mabinti hawa hupenda sana wanapoona wanasaidiwa kazi au kazi ambazo wanahisi zilikuwa zao zinafanywa na Bosi wao tena kiroho safi yaani bila wewe bosi kufanya kazi hiyo kwa maneno aneno ya malalamiko.

3. Epuka kumgombeza

Kumgombeza mtu ni kumdhalilisha hasa kama unamgombeza mbele ya wadogo zake au watu wengine. Leo hii ukimgombeza gombeza mara kwa mara na vipigo juu mbele ya wanao nao pia hawatamheshimu. watamuona hovyo tu na kumdharau.

Epuka kukosa Kubwa wala Dogo. Kila akifanya hiki ni kosa; akigusa kile amekosea; anaosha vyombo na kwa bahati mbaya glass au sahani la udongo imevunjika maneno juu na kumtishia kumkata mshahara!.

Unamwambia mmeo kila kisa; Jamani! Unapiga simu kwao au kwa aliekuletea kwa kila kosa. Binti umempokea leo baada ya siku tatu unaanza kumshitaki kwa marafiji zako au kwa aliekuletea! Mara unapiga simu unaanza kusema :" Ndugu niambie; aisee yule binti uloniletea majanga matupu!! Amefanya hili na hili...!!!! Ya nini!!! kila mtu anakasoro! mrekebishe kasoro hizo pengine anachofanya hajui ni kosa au hajazoea/ hana mazoea. Mvumilie na mrekebishe kwa upole na upendo.

Wewe mama umekuwa wa mashitaka na malalamiko kila siku. Du Ovyo!!

kwa kufanya hivi ni kumfanya asononeke na ajisikie mkosefu kila siku na hatimae kujawa na hofu kubwa. Akikuona anogopa anapata amani ukiondoka kazini na anatamani usirudi.

4 .Epuka kumsema kuhusu chakula

Kati ya vitu ambavyo watu wengi hawavipendi ni kuwasemachakula. Na wala si tabia ya sisi watanzania.

Kumsema mtu anakula kama mchwa; ni mdokozi; hashibi; anakula matonge makubwa; sahani ya chakula anayokula hakuna anaeweza kuila! Hayo yote ni maneno mabovu a ya hovyo kumwambia mtu.Ni maneno y uchoyo; ya unyimi.

Lakini imekuwa kawaida kwa Akina mama wengi kusikia wakiwasema mabinti zao wa kazi kwa maneno hayo eitha kwa kificho na pengine hata na wao wakiwepo. Aisee; wanajisikia vibaya sana. Asume ni wewe unaesutwa namna hiyo utajisikiaje aisee!! wala si faire!.

Wengine utawasikia wakisema kuwa mabunti wa kazi wanakunywa uji au lishe ya watoto wao!

Akitoka kazini cha kwanza ni kumnyenyuwa mwanae akimpima uzito; Jamani uzito unapimwa kwa mikono! si umpeeke kwenye mizani ya bembea!!

Sasa akimkuta ni mwepesi da!da!da!da!da!!!! ataanza kumsimanga tena kwa ukali eh! umempa uji mtoto?? Mbona mwepesi hivi? akimwambia nimempa. Basi atambishia mpaka.

Kwa utafiti mdogo ulofanyika ni kwamba imegundulika kuwa mabinti wa kazi hufurahi sana na kujisikia amani wanapoona mtoto ametoka kliniki akiwa ameongeza kilo!

Mtoto akiwa na kilo zile zile za mwezi ulopita basi atasimangwa kuwa anakunywa uji wa mtoto ndo maana mtoto hapandi kilo.

Basi huyo mtoto akipungua kilo; mwe! mwe! mwe! mwe! ndo kiama !!!! Atahubiliwa kila zaburi!! na kwa bahati mbaya au nzuri huyo binti wa kazi apate kunenepa toka afike tu! Ndo itakuwa gear point kuwa yeye ni kula tu lishe na chakula cha mtoto. Imani inapingua kwake.

Acheni Mambo hayo! Hivi inawezekana kweli hata wewe mwenyewe upike uji wa mtoto usinywe hata kijiko kimoja cha uji! Au umeshawahi kumimina uji kwenye kikombe au sahani halafu ukampa mwanao akaunywa wote bila kubaki? Je ukibaki kwenye kikombe au sahani baada ya yeye kushiba unaumwaga? Si unaunywa? Sasa yeye akiunywa anakosa gani? Kwa nini yeye apike kitu ambacho hawezi kuonja!!

Basi Tuepuke haya kwani mabinti hawa hupoteza imani na kuadhirika kisaikolojia; hujawa na hofu hivyo kupunguza upendo kwa mtoto.

5. Epuka kumsema vibaya kabila lake.

Katika vitu vibaya ambavyo watu wengi hawavipendi ninpamoja na kuwadharau hasa kudharau kabila lake. Hakuna mtu ambae anapenda adhalaurike kwa kabila.

Sasa wewe boss epuka kumsema vibaya binti wa kazi kuhusu kabila lake. Maneno kama haya: Kabila lako ni machangundoa sana; kabila lako linaongoza kwa ma barmaid!; kabila lako niwachawi sana! kabila laki alina wasomi! Kabila lako watu ni masikini; halina matajiri! Kabila lako linaongoza kwa ma house girls n.k! Kumbuka utakapo mwambia hivi au kila siku unakandia kabila lake unamfanya ajisikie vibaya na kusononeneka.

Binti wa kazi msifie kwa kila kitu.Sifia kabila lake
6. Mpe motisha ( incentives)

Kila mtu anapenda kuwa motivated. Na hapa namkumbuka Abraham Maslow kwenye thiory yake ya Maslow's Hierarchy of Needs.

Wewe Bossi kuwa na tabia ya kumpa vizawadi vya hapa na pale huyu binti tena mpe kama surprise.

Mnunulie nguo; mafuta ya kupakaa; lotion; perfume; pads; na kama ni mkubwa wa umri kama miaka 16 na kuendelea na anamiliki simu; msaidie kwa mala moja moja hela ya vocha!

Mnunulie viatu na kama ni siku ya siku kuu na umeamua kuwanunulia wanao basi na yeye mnunulie nguo. Siku za juma pili mpe nauli kama analazimika kupanda gari kwenda kanisani na pia mpe na hela ya sadaka.

Unapo fanya hayo yote usije mkata hela hiyo kwenye mshahara!!!

Mpe ushauri mbali mbali na muahidi kumtendea mambo mbali mbali mazuri hapo mbeleni kama kumwendeleza kielimu; kumnunulia mashine ya cherehani; kumfungulia ka biashara kadogo n.k

Basi; kwa kumfanyia hivo atakushukuru sana na kukuona wa mhimu kuliko hata ndugu zake. Atasahau hata shida alizokuwa nazo huko nyumbani kwao na kujiona amehamia ulimwengu mwingine kabisa. Mwanao atampenda zaidi na zaidi.

KUMBUKA

"Hakuna mtoto wa kike aliezaliwa kuwa binti wa Kazi! Pia hakuna mzazi aliejifungua mtoto na kusema anatamani awe Binti wa kazi!"

Hawa mabinti wa kazi hupatikana kutokana na

1. Hali duni ya Maishai kwao.

2. Baada ya mambo yote kufeli

3. Ugomvi katika familia

4. Mimba za utotoni

n.k

Kwa maana hiyo basi, unapompata binti wa kazi anakuwa na msongo wa mawazo; anakuwa amekata tamaa ya maisha; anakuwa na psychological problems. Kuja kwako ni kuanza maish mapya na jamii mpya pia.

Kwa hiyo Bossi yampasa kuonesha upendo wa hali ya juu kwa binti wa kazi ili nae amfeel; amuone kuwa nimkombozi wake.

Mpende kwanza huyu binti wa kazi ndipo ampende huyo mtoto alokuja kumlea!

Mfano mziri ni usiano kati ya Mwalimu;Mwanafunzi na Somo. Ili Mwanafunzi apate kupenda na kuelewa somo; lazima ampende kwanza mwalimu wa somo hilo; Hayo yakiwepo mwanafunzi hufauli hilo somo.

kuwepo na uhusiano mziri baina yao na ndipo mwanafunzi huyo aweze kuelewa somo.

Ndivyo ilivyo kwa hawa mabinti wa kazi.

Nawasilisha.
 
Ukweli mtupu kiongozi sema nao wakipata wanaume huko mtakoma nyumbani, hawatulii dharau, kiburi na mambo mengine
 
Ngoja niiweke kipolo nitakuwa naisoma kidogokidogo hata wiki 2 hadi niimalize makala nzima maana ni zaidi ya kitabu cha Erick Shigongo.
 
Back
Top Bottom