Kero kero kero! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kero kero kero!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Bishanga, Mar 6, 2011.

 1. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #1
  Mar 6, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Kila kukicha kinamama wana MMU kazi kutusimanga,sasa leo na mimi ngoja niwatolee uvivu.Kinamama mnatukera kwa haya yafuatayo:
  1.Utegemezi: Unambeep mmeo/hawara/bf,nini mama?unamuuliza, 'naomba unitumie vocha',sawa nakurushia ya elfu kumi,muda mchache baadae unanibeep,nakupigia 'luku imeisha baba'sasa nambieni hiyo vocha elfu kumi huwa mnampigia nani? au ni kwa ajili ya kupigia umbea,'Eh mwenzangu jana si nikamwona Bishanga anaingia gest',inahusu?
  2.Wivu: Mara upekenyue simu yangu,nikirudi nyumbani 'oh ulikuwa wapi' mara 'nani huyo ulimpakia kwenye gari',nikivua nguo mara unuse kufuli langu, jamani ya nini yote haya? mbona sisi hatuwafatilii hivyo?
  3.Kununa: Mara unune,mara uvimbe,mara unisonye kwa mbali,nimekukosea nini? nikuuliza husemi kitu,mkoje jamani?
  4. Gubu:Hata kama nilikukosea mwaka 1947 na nikakuomba radhi ukajitia umenisamehe ni bure tu,nikikukosea kidogo leo ,utasikia 'oh ndo mana nilikubamba na hausgel'sasa jamani tukio la 1970 unalibebea bango mpaka leo,we umenikosea mangapi mbona huwa sirudii kuyakumbushia?
  5.Mnaongea mno: Wanawake mnaongea jamani, pich pich pich pich,du,hamchoki mkaacha na waume/hawara/bf zenu wakaongea?
  6.Uvivu: Sasa kuajiri housegirl ndo iwe sababu ya huyo housegirl kufua hadi kufuli zangu,na kibaya zaidi baba akiumwa eti yeye ndo anamkumbusha dawa,chakula anampakulia yeye,halafu mzee akimfanzia mnakuja juu.
  7.Ubinafsi: Nikilipa schoolfees za mdogo wako poa tu,paa la nyumba ya shangazi yako likiepuliwa na kimbunga nikatoa pesa ya mabati poa tu,mama yako akiumwa nikampeleka India poa tu,lakini shuhudia mtoto wa dada yangu akose karo nimlipie au nimnunulie ka gari baba yangu mstahafu,huo mziki wake utaukoma,'eh ndo mana hatuendelei sijui nini sijui nini' lol!
  Ngoja nipumzike kwanza ntarudi baadae,nina hasira flan hivi.
   
 2. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #2
  Mar 6, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  hayo kweli kabisa!wape vidonge vyao
   
 3. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #3
  Mar 6, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Aisee hiyo namba nne ndo kiboko. Leo mkeo kakuudhi nini jamani?
   
 4. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #4
  Mar 6, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  We acha tu kuna kitu kimeni put off big time!
   
 5. k

  kisukari JF-Expert Member

  #5
  Mar 6, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,754
  Likes Received: 1,038
  Trophy Points: 280
  mmmh,mwenzangu sio wote tupo hivyo jamani.labda huyo wako,inabidi umueleweshe,kama haelewesheki,basi potezea hizo longolongo zake.
   
 6. Papa Mopao

  Papa Mopao JF-Expert Member

  #6
  Mar 6, 2011
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 3,353
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Ukitaka kuwajua wa dizaini hizo, angalia mawazo yao yakoje katika shughuli za kila siku hapo ndo utapata kitu cha kuwapotezea!
   
 7. CPU

  CPU JF Gold Member

  #7
  Mar 6, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mkuu, ingawaje hasira hazijengi lakin naunga mkono hoja ya kuwapa kwinini wameze. Maana kuna mambo mengine wakifanya wao utasikia "oooh mume ndio sababu ya mke kutoka nje, hamjali mke wake" yaani full utetezi, wakifanya wanaume sasaaaaaaaaa utaanza kusikia nyimbo "oooh nyie wanaume ndio mlivyo, hamtosheki"
  Leo ngoja nivae uso wa mbuzi, wape hao banaa
   
 8. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #8
  Mar 6, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mengine yote hayanihusu ila no.4 mmmh!Tatizo ni kwamba hua sisahau kitu!Pole kwa kuboreka!
   
 9. CPU

  CPU JF Gold Member

  #9
  Mar 6, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hao tunawaita FEMINIST
   
 10. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #10
  Mar 6, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  ki-sugar ushauri gani huu inaonyesha huu ni uhusiano wa muda mrefu na labda wana watoto,badala ya kusuluhisha unataka ampotezee utamkaribisha kwako ?
   
 11. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #11
  Mar 6, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Pole sana
   
 12. k

  kisukari JF-Expert Member

  #12
  Mar 6, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,754
  Likes Received: 1,038
  Trophy Points: 280
  kama yeye mwenyewe alivyosema ana hasira.unajua kuna baadhi ya watu hata umueleweshe vipi haelewi ni kama tabia ya mtu.sasa utakasirika kwa kila jambo?inabidi mambo madogomadogo uyapuuze,otherwise utajitia presha bure.kwani juu ya maudhi,yapo mengine ambayo ni mazuri.life is too short jamani
   
 13. Keren_Happuch

  Keren_Happuch JF-Expert Member

  #13
  Mar 6, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 1,880
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Pole sana Bishanga, naona uko na hasira kwelikweli!! Ila taratibu tu usije ukachapa bakora wasiohusika. Ninaamini katika mawasiliano, kama hufurahii kitu kwa mwenzi wako, ni vizuri ukamweleza; kama kweli anakupenda, atabadilika.

  Ila hapo penye red, kama kuna mwanamke anafanya hivyo, huyo amepitiliza....:A S 13::A S 13::A S 13:
   
 14. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #14
  Mar 6, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Mbona ukiandika scientific paper unafanya reference ya kazi za zamani, iweje leo mke wako akifanya reference ya matendo yako mabovu ya zamani uchukie?

  Mtafiti mzuri ni yule anayeweka historia ya utafiti wake kwa kuangalia nini kilifanyika kabla.
   
 15. Kingcobra

  Kingcobra JF-Expert Member

  #15
  Mar 6, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Pamoja kaka!
   
 16. M

  Matarese JF-Expert Member

  #16
  Mar 6, 2011
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 519
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Aithee Bishanga uliyoandika YOTE NI KWELI TUPU 100%!, sometime wanakera sana baadhi ya hawa wamama HASA HIYO NAMBA 7, YAANI HIYO SIO BAADHI ILA NI WAMAMA WOTE!
   
 17. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #17
  Mar 6, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Asante BintiMkongwe!Kwanzia leo ntakua nakumbushia bila wasi wasi kabisa!
   
 18. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #18
  Mar 6, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,827
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye namba nne. Mtu anakwambia umenikosea unamuomba samahani anakwambia nimekusamehe lakini kauli na matendo yake hayaonyeshi kama kweli amekusamehe hili mimi hunikosesha raha sana. Neno "samehe" lina uzito mkubwa sana hivyo unapolitamka basi uonyeshe kweli kama umesemehe na siyo kulitamka tu kirahisi rahisi.
   
 19. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #19
  Mar 6, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Wewe embu kua na heshima kidogo!Wengine roho za kichoyo na ubinfsi hatukupewa...Unless hatuko kwenye kundi la wamama!
   
 20. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #20
  Mar 6, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Tatizo sio matendo kana kwamba utaendelea kununiwa ila kusahau kunashindikana kwahiyo ukirudia tena unakumbushiwa!
   
Loading...