NB.UZI NI KWA WAKRISTO WAKATOLIKI TU.
Kuna baadhi ya mambo huwa yananikwaza kiukweli kanisani wakati wa misa.
1.Padri kuhubiri wakati ambao sio wa mahubiri. Yani padri misa inaanza tu maneno kibaoo.
Hapana mkuu. Hayo sio mahubiri ni Utangulizi yan Leo tunaongozwa neno la kutoka ....somo la kwanza na ... Injili.Tena hsomwa nia za Misa Kwa wale waliopeleka maombi misa na hayo huayunganisha na nia za kila aliyehudhuria misa hiyo na nia za wale walioomba waombewe na labda hawapo hapo kanisani kwenye misa husika. Je, hilo ni kero kwako?
Muda wa mahubiri anaongea sanaaa, vitu vilevile,
Kuongea ni karama jinsi padre mhusika anavyoweza kufafanua masomo yaliyosomwa somo la kwanza, somo la pili na injili yakiunganishwa pamoja kutoa fundisho la kimsingi la siku hiyo ambao alili-
intaduce mwanzo wa misa.
Mahubiri kimsingi huwa yanatakiwa yasizidi dk,10-15/20 ili kutokupoteza focus ya wasikilizaji. Je, hilo ni ameongea sanaa? Mbona kijiweni au bar mnaweza kuongea, kuangalia runinga hadi usiku bila kuchoka? kumbuka Ukristo ni Msalaba sio lelemama au starehe.
muda wa kumaliza misa anaanza tena kupiga porojo zizizo na msingi. Muda wa matangazo anaanza tena upya. Yani very selfish na inconsiderate.
Matangazo hutolewa na kiongozi aliyejiandaae.g. M/Kiti wa baraza au Katibu na huwa yameandikwa kwenye daftari la matangazo. Lkini usisahau Padre naye ni kiongozi anaweza kuwa na matangazo yake kwa kondoo/waumini mahalia. Mara nyingi padre hutoa matangazo
(kama anayo) na kufafanua pale inapobidi. Je, hizo ni porojo?
Kumbuka siku ya Jumapili i.e. Dominika ni siku ya Kusanyiko la Bwana. Zamani ilikuwa ni siku ya mapumziko -hakuna kufanya kazi nzito labda niwe ni pale inapobidi. Sasa Padre kwake sio siku ya mapumziko. Ni siku ya kazi ya kutangaza injili. Kwa hiyo hapo anatekeleza wajibu wake. Wajibu wako ni kusikilizaKwa bahati mbaya hakunaga kuliza maswali kwani pale anaongea kwa niaba ya Yesu Kristo sio kwa niaba yake mwenyewe. rejea mavazi anayovaa padre yenye maandishi X P yanayo ashiria ukuhani, usafi wa kiroho, na kumwakilisha Yesu Kristo (mpakwa mafuta) wakati wa Ibada ya Misa Takatifu.
Je huo ni Ubinafsi uliokithiri i.e very selfish na kutokujali i.e. inconsiderate?
Vipi, ww ungetaka afanyeje hapo? Je, unataka awe anajali mambo yako zaidi ya yale anayopaswa afanye na Boss wake .i.e Yesu Kristo.? Hata hivyo, Nakubaliana na ww kwamba kuna namna fulani ya kukereka pale inapokuwa ni too much.
2. Muda wa kutakiana amani, hakuna kitu SIPENDI kama padri kuanza kulazimisha watu waambiane kitu na kupeana mikono, mfano, mwambie jirani yako blah blah, Yani kinanikwazaga sana hiki kitu, hakina umuhimu Wala ulazima kiliturjia.
Hilo ni Parokia mahalia wala sio kila mahali. Mbona wakati wa covid hatukushikana mkono na mambo yalienda sawa tuu. Sio la lazima kiliturjia - ni kweli.
Vingine vipi ila kwa haraka ni hivi. Vinapoteza sana focus ambaye inatakiwa iwe ni kwa Yesu. Au Kama Kuna vingine ongezeni, Kama ninakosea pia nisahihishwe.
Hujakosea mkuu. Ni vizuri kwa wakatoliki wanaofunguka na kueleza yaliyo moyoni esp. Kuhusiana na Liturjia manake Adhimisho hilo ndo Sala kuu na Sadaka iliyo bora kuliko zote.