Kero: Jirani kufungulia mziki sauti kubwa, nimfanye nini?

muchetz

JF-Expert Member
Aug 16, 2010
943
732
Nina jirani yangu(nimepanga) naye ana nyumba yake jirani na nyumba niliyopanga.

Ananifungulia muziki kama vile yale magari yanyopita barabarani kufanya promotions au adverts. Kwa kweli ananitesa sana sababu mi nafanyia kazi zangu nyumbani muda mwingi(Home office). Na to make matters worse akifungua hivyo speaker anaelekeza nyumbani kwangu, ye anatoka nje.

Nilijaribu kuwaambia juu ya kero ambayo wakuwa wakinisababishia mama na watoto wa huyu jirani lakini haijasaidia. Nikajaribu kumwambia baba wa hiyo nyumba juu ya kadhia hii lakini haijasaidia, mara anapotoka kwenda kazini mambo ni yale yale.

Naombeni ushauri wenu juu ya kero hii.
 
Hapo nimekuelewa fanya hivi siku moja na wewe fungulia mziki mkubwa funga nyumba uondoke ulale huko huko urud asubuhi kesho yake.
Adhabu watakayoipata wakikuuliza wambie hata wewe ndiyo adhabu wanayokupa

Hilo wazo nimeshalifikiria.... ngoja nimepate na mengine ... ntachugua cha kufanya.
 
Nina jirani yangu(nimepanga) naye ana nyumba yake jirani na nyumba niliyopanga. Ananifungulia muziki kama vile yale magari yanyopita barabarani kufanya promotions au adverts. Kwa kweli ananitesa sana sababu mi nafanyia kazi zangu nyumbani muda mwingi(Home office). Na to make matters worse akifungua hivyo speaker anaelekeza nyumbani kwangu, ye anatoka nje.

Nilijaribu kuwaambia juu ya kero ambayo wakuwa wakinisababishia mama na watoto wa huyu jirani lakini haijasaidia. Nikajaribu kumwambia baba wa hiyo nyumba juu ya kadhia hii lakini haijasaidia, mara anapotoka kwenda kazini mambo ni yale yale.

Naombeni ushauri wenu juu ya kero hii.

Anza kwa kushtaki kwa mjumbe, then kitongoji , kata... baraza la mazingira mwisho polisi - - mahakamani.
 
Pole. Me yalikuwa yananikuta kama yako.Nikawa nawaambia kila siku lakini wakawa hawajali. Kuna siku nilifungulia radio sauti mpaka mwisho. Nahisi walitafutana mle ndani.
Maana alikuwa hajui kama nina radio kubwa.
Akanifata akanambia radio yako inanguvu. Nikamwambia eee.tena hapa sio mwisho. Mpaka leo ananiheshimu
 
Kuna option tatu
1.ripoti kwa mamlaka husika (mjumbe,mwenyekiti wa mtaa,kata,wilayani,polisi)

2.na wewe wafanyie unyambilisi mpaka akili iwakae sawa,(i.e kodisha jenereta nawewe uwasumbue usiku,mwaga ndoo ya kinyesi kibarazani au uwani kwao au sebuleni ikiwezekana ).

3.Hama
 
sijui tatizo huwa ni nini kwa watu kama hao.

Nakumbuka mwaka 2014 nilipanga nyumba yule mpangaji alikuwa noma aisee.

Yeye zile spika alikuwa ameunganisha waya akaweka hizo spika kwenye madilisha tena juu kabisa, kero yake sasa noma sana.

Anafunga saa6 usiku na anafungua saa11 alfajili sidhani kama hata makanisa ya walokole yalikuwa yanamfikia kwa kelele!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom