Lis
JF-Expert Member
- Jun 2, 2012
- 471
- 346
Nimeshindwa hii inshu niiweke kwenye jukwaa gani, nikaona hata hapa si mbaya sana, nina Jirani yangu tunaishi nyumba tofauti lakini ziko karibu, yeye kila ikifika saa moja asubuhi ni mama wa nyumbani huamka na kufungulia sauti ya juu sana kiasi kwamba kama ulikuwa umelala lazima utaamka, imekuwa ni tabia yake ya siku nyingi, nikaamua nimfuate kwa ustaarabu nimwambie naomba awe anaweka sauti ya chini, akanielewa baada ya wiki akarudia tena.
Nikamfuata kwa Mara ya pili nikamuomba tena na anapoweka sauti ya juu, ni kuanzia SAA moja asubuhi hazimi redio hadi SAA moja jioni ndio hupunguza sauti na kuweka ya kawaida hata akienda Dukani au mbali kwa masaa kadhaa, ataacha ikiwa hivo kitendo hiki kimenichosha hadi nimeamua yafuatayo:
Nimeamua ikifika usiku wakati yeye ndio amepunguza sauti na mimi ndio niwashe sasa yangu coz anawahi sana kulala ili nimsumbue na yeye apate kero kama tunayopata sisi, je nitakuwa nimefanya makosa?
Naomba mnipe ushauri njia ya kufanya tafadhali, ukizingatia mama mwenyewe ni mjamzito muda wowote anajifungua, nishawaza tena nimsubiri ajifungue ili akiwa na mtoto mdogo hatataka kelele na mimi ndio niwashe sabufa yangu sasa, nitakuwa nimekosea?