Kenyela atolewa u RPC

Kenyela atolewa u RPC

Mkuu unaweza kutupatia source ya hii taarifa ili tuutafute ukweli? Manake hii pandisha vyeo ya Kova na Kamuhanda inasababisha tufukunyue kila mahali ili kujua kinachokwenda kutokea.

Btw kama failures ndio wanakwenda kurundikwa makao makuu, ufanisi wa jeshi la polisi ni dhahiri kuwa unakuwa mashakani.

Mwita uliona walichomfanyia SIMON SIRRO, hata kumpa U DC P ni sababu ya rekodi yake njema na wakubwa wameona aibu ila fitna anazopigwa ni balaa sana. IGP na kundi maslahi lake wanapandisha vyeo wawatakao tu, kwangu DCP Sirro atabaki kuwa shujaa, askari msomi huyu mwenye nidhamu na kusoma nyakati katika kujenga jeshi la polisi la kisasa.
 
Mi nilikuwa namkubali sana Kenyela. Hata ukionana naye mnasalimiana vizuri bila shida. Kwa kweli ni mtu wa watu. Anyway, TUMWOMBEE MUNGU AZIDI KUMSIMAMIA VYEMA HUKO ALIKOPELEKWA, AZIDI KUNG'AA PALIPO NA GIZA TOTOLO.
Inshallah Kenyela, Mungu awe nawe-SIMAMIA HAKI HATA KAMA UTAKUFA KESHO.
 
Mtumishi wa serikali anaweza kuhamishiwa mahali po pote wakati wo wote. Siyo lazima awe ametenda kosa.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums


Na akiwa amefanya makosa je kama Kamuhanda na mauaji ya Mwangosi na madereva bodaboda kule Ruvuma???!!!

Anapaswa kupandishwa cheo,marupurupu na kupigiwa makofi???!!

Kweli ukiwa sehemu ya watu wachafu utatetea uchafu na utajiona hauuoni uchafu hata ukiambiwa na kuonyeshwa,ni hasara kwa taifa na ni upuuzi kusikiliza hoja za kipuuzi zaidi ya mara moja!!!
 
Mbona jamaa anapiga kazi sana inakuwaje sasa? Kweli ccm haitaki wasema kweli
 
Kagusa maslahi ya wakubwa, madanguro na madawa ya kulevya. To be honest Hamas Yuko vizuri but ndiio hivyo
Bora wamemwindoa maana kila siku alikuwa anadili na machangudoa huku majambazi yakitesa mtaani...
 
Alikuwa Polisi Pekee niliyekuwa namuamini , kwa maana hiyo hivi sasa simuamini yeyote ndani ya jeshi hilo !
 
Mtumishi wa serikali anaweza kuhamishiwa mahali po pote wakati wo wote. Siyo lazima awe ametenda kosa.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
Ndiyo apelekwe kwenye benchi makao makuu?
 
Nani atasimamia ile kamatakamata ya akina dada wanaojiuza sehemu mbalimbali Kinondoni!

Kwa hiyo wale madadapoa ambao Waliberali CUF wanataka wapewe Hakiiii!!! Watapeta sana mwaka huu!
 
source ni mke wangu anafanya kazi makao ya polisi na ndiye aliyechapisha bafua ya kuhamishwa kenyela
mhhhh

mkuu huoni kwamba unahatarisha kazi na maisha ya mke wako pamoja na familia yako kwa ku-disclose source ya taarifa hii kwa namna ulivyofanya?

Si mara zote mtoa habari analazimika kutaja source yake ya habari, na nadhani hii ni basic and founding principle and ethics za journalism.

Anyway lane anasema thank you very much mkuu Kigogo for sharing this with us
 
Last edited by a moderator:
kupanda na kushuka yote ni majaliwa yake Mungu
 
Mwita uliona walichomfanyia SIMON SIRRO, hata kumpa U DC P ni sababu ya rekodi yake njema na wakubwa wameona aibu ila fitna anazopigwa ni balaa sana. IGP na kundi maslahi lake wanapandisha vyeo wawatakao tu, kwangu DCP Sirro atabaki kuwa shujaa, askari msomi huyu mwenye nidhamu na kusoma nyakati katika kujenga jeshi la polisi la kisasa.

Mkuu PhD kweli bana umenikumbusha huyo Kamanda Sirro namkumbuka alikuwa mweledi sana katika kazi zake wakati alipokuwa RPC Rukwa, Tanga na baadae Mwanza. Mara tu baada ya uchaguzi mkuu wa 2010 wakampeleka makao makuu kusoma magazeti kwa sababu alishindwa kuwapiga Chadema Mwanza na hatimaye tukachukua majimbo yote mawili ya jiji la Mwanza.

Na ndio maana jeshi hili la polisi halifanyi kazi zake kwa weledi kwakuwa akionekana kamanda anafanya kazi zake kwa kufuata weledi wanamuweka benchi na wale wajingawajinga wanaokiuka sheria na kuwaua wananchi na kuwabambikia makosa ndio wanaonekana wa maana.
\
Angalia Kamuhanda ameua Ruvuma akapandishwa cheo na kuhamishiwa Iringa, baada ya kuua tena amepandishwa cheo kwa mara nyingine. Kuna Constantine Massawe alikuwa OCD Tarime baada ya kuua wananchi kule north mara wakampandisha kuwa ACP na kuwa RPC Tarime/Rorya. Hao ni kwa uchache sana lakini list ni ndefu sana.
 
Last edited by a moderator:
Kenyela ni hivi karibuni tu alipokea bachelor yake pale Kinondoni @ OUT.

Huenda jeshi halihitaji ustaarabu na usomi kwa watendaji wake ktk ngazi za RPC.
 
Kenyela ni hivi karibuni tu alipokea bachelor yake pale Kinondoni @ OUT.

Huenda jeshi halihitaji ustaarabu na usomi kwa watendaji wake ktk ngazi za RPC.

kachelewa sana..watu wa umri wake wanapata phd sio bachelor tena ya library information sijui nini
 
Ameshindwa kuwadhibiti/kuwauwa CDM!

Mara ya mwisho nakumbuka aliwekewa SUMU kwenye soda(?)/maji(?) ikabidi kwenda kui flush kutoka mwilini!
Kamanda Kenyela naye alishapewa ile polonium 210 isotope?kweli hakuna kuaminiana
 
Back
Top Bottom