Nyerere alikuwa anaipenda afrika ya mashariki yote:
(a) Alikuwa tayari kuchelewesha uhuru wa Tanganyika kusudi sote tupate uhuru pamoja;
(b) Alikuwa tayari kumsimamisha Jomo Kenyatta ndiye awe rais wa Afrika ya mashariki, yeye Nyerere mwenyewe awe waziri wa mambo ya nje tu.
(c) Alikuwa tayari kuwapokewa wakikuyu wote waliokuwa hawana ardhi huko kwao Kenya waje kusihi Tanzania, kama alivyofanya kwa warundi na wanyarwanda ambao walikumbana na migogoro ya kikabila huko kwao.
(d) Hata baada ya kuanzisha Jumui ya Afrika ya Mashariki, alikuwa tayari kuacha makao makuu ya mashirika makubwa ya jumuia hiyo kama vile Ndege, Reli, na bandari yawe Kenya.
Hata hivyo wenzetu wa Kenya hawakuwa waungwana kabisa na walitanguliza zaidi maslahi yao binafsi. Ni kutokana na historia hiyo ya ubinafsi ndiyo maana watanzania wengi tunaingalia Kenya kwa jicho la makini sana, jambo ambalo limefanya kukua wa jumuia ya Afrika ya mashariki iwe ndoto. Laiti Kenya isingekuwa mojawapo ya wanachama wa jumuia hii, nina imani kuwa jumuia ingekuwa imesharuka juu sana. Historia hiyo inaziweka nchi za Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi kwa karibu zaidi ya Kenya.