Kitila Mkumbo
JF-Expert Member
- Feb 25, 2006
- 3,355
- 1,955
Kwa mara ya kwanza katika uchaguzi wa kiafrika kila mshikadau sasa amekubali na kukiri kuwa uchaguzi umeibwa. Yaani hata international community ambao hupenda kumumunya maneno kwa kuweka diplomasia sasa wametoka open na kusema Kibaki kaiba. Kimsingi uchaguzi huu umeturudisha nyuma Afrika. Tulikuwa na nafasi nzuri sana ya kuithibitishia dunia kwamba hata sisi waafrika tunaweza kuwa wastaraabu na tukaheshimu maamuzi ya watu. Lakini sasa inawezekana hii tukawa tumeipoteza. Hata hivyo nahisi bado tuna nafasi ya kuonyesha kwamba tunaweza kutatua matatizo yetu kistaraabu bila kupoteza maisha ya watu au angalau kuepusha upotevu wa maisha zaidi. Ni katika hili nawaalika tutoe mawazo yetu juu ya namna ya kuikoa Kenya na umwagaji wa damu na wakati huohuo kupata suluhisho la maana la matatizo ya kisiasa yanayowakabili.
Inawezekana mawazo yetu yasiwe na impact sana kwa yale yanayotokea na yatakayotokea Kenya, lakini najisikia kwamba tunawajibika kuwasaidia wenzetu japo kimawazo juu ya namna ya kutatua hili gogoro ambalo Kibaki ameamua kulitengeneza. Kama ni swala la amani na utulivu nafikiri sisi tuna nafasi nzuri sana ya kusaidia hapa. Je, mnafikiri kwamba tunaweza kuwashawishi hawa ndugu zetu wakakubaliana na ile falsafa yetu watanzania kwamba kama imefikia hatua ya watu kuuawa basi bwana tunakubali yaishe?
Ni wazi kuwa huyu bwana baada ya kuapishwa harakaharaka ndiye sasa ni Rais wa Kenya (ukweli unaouma) na hakuna shortcut ya kumtoa pale.Kuna options mbili kubwa ambazo zipo open kwa wana Kenya na hasa ODM supporters:
i) mtindo wa Ulaya Mashariki: maandamano hadi kieleweke; hii ni nzuri sana, lakini naogopa kwamba kwa sisi waafrika na jinsi majeshi yetu ya polisi yasivyo na utu itakuwa ni ghalika ya damu, watu wengi watauwa, na hapa ndipo nasema hii njia naona kwamba haina tija kwa wakenya wala kwa ODM
ii) Hii ndio naona mimi ni njia sawa. Madamu ODM wana wabunge wa kutosha, watumie nguvu ya bunge. Waende bungeni wabadilishe sheria kandamiza ikiwemo kumnyang'anya Rais madaraka ya kuteua tume ya uchaguzi na kuiacha mikononi mwa Bunge au chombo kingine. Kisha wabadilishe sheria ya vote of no confidence kutoka 2/3 iwe nusu; within few months wa-table kura ya kutokuwa na imani na Rais kwa madai hayohayo ya kwamba aliingia madarakani kinyemela kwa kuiba kura. Nafikiri kwamba hii ni njia nzuri zaidi. Japokuwa inaweza kuchukua muda kidogo lakini itaepusha ile nchi kuingia katika machafuko. Na mara zote ODM wasisitize kwamba haya mapambano sio kati ya Kikuyu na makabila mengine bali kati ya Demokrasia na udikteta. Hii itawavuta wengi zaidi kujiunga nao wakiwemo wakikuyu wanaokerwa na ubakaji wa sanduku la kura.
Inawezekana hii lecture yangu ikawa too late kwa jinsi mambo yanavyotokea Kenya au ikawa useless kabisa na hata mimi kuonekana mwoga kutokana na hasira zilizopo lakini nafikiri kwamba maisha ya watu wa Kenya na nchi yao ni wa maana zaidi na kama kuna njia ya kuepusha vifo basi itumike.