Kenya yapindua meza kwa Tanzania kwa kuuza bidhaa 30%

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,048
49,731
Unaweza kusema Kenya imepindua meza kwa kurejea kwenye nafasi yake katika biashara baina yake na Tanzania, baada ya kuipoteza mwaka uliopita.

Ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) iliyochapishwa Desemba 31, 2023 inaonyesha, Kenya iliuza bidhaa zake nchini kwa asilimia 31 zaidi ya kiwango ambacho Tanzania iliuza kwao, ikiwa ni tofauti na mwaka uliotangulia ambapo Tanzania iliuza katika nchi hiyo kwa asilimia 10 zaidi.

Hiyo ikiwa na maana kuwa, bidhaa za Sh1.06 trilioni ziliingizwa nchini kutoka Kenya ikilinganishwa na bidhaa za zaidi ya Sh724.32 bilioni za Tanzania zilizouzwa nchini kwao mwaka 2022/2023.

Hiyo ni tofauti na mwaka 2021/2022 ambapo Tanzania iliuza zaidi nchini Kenya bidhaa za zaidi ya Sh993.42 bilioni, huku ikinunua bidhaa za Sh892.82 bilioni.

“Huenda hali iliyotokea sasa hivi kati ya biashara ya Kenya na Tanzania ilitokana na sitofahamu iliyokuwa ikiendelea nchini huko,” alisema Mtaalamu wa masuala ya biashara na uchumi, Oscar Mkude.

Soma zaidi kwenye tovuti ya Mwananchi
(Imeandikwa na Aurea Simtowe)

My Take
Kuporomoka Kwa Shilingi ya Kenya Dhidi ya Tanzania Kwa zaidi ya 10% ni mojawapo ya sababu zilizoisaisia Kenya kuuza Nje zaidi
Screenshot_20240108-111149.jpg
 
Wewe unalinganisha ufanisi na maendeleo yako na mtu au malengo yako?
Ukilielewa hili hutasumbuka na maisha, na utapiga hatua kubwa sana.
 
Back
Top Bottom