Kenya yapata wagonjwa wapya 23 wa CoronaVirus

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
7bf17ab408aa34287d1fe0fce998e4a6

Idadi ya wagonjwa wa virusi vya corona nchini Kenya imeongezeka hadi 672 baada ya wagonjwa wapya 23 kukutwa na virusi hivyo katika kipindi cha saa 24.

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumapili katibu msimamizi wa maswala ya Afya nchini Kenya Rashid Aman amesema kuwa idadi ya waliopona virusi yafika 239 baada ya wagonjwa wengine 32 kupona virusi hivyo.

Kati ya idadi hiyo wagonjwa 12 wameripotiwa kutoka Mombasa , sita kutoka Mandera wanne kutoka Nairobi na mmoja kutoka Kajiado

Dkt Aman amesema kwamba wagonjwa watatu wa;likuwa wakitoka katika vifaa vya karantini.

Amsema kwamba sampuli 32,097 zilifanyiwa vipimo nchini kufikia sasa.

Ili kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo , serikali imewaagiza madereva wote wa malori ya masafa marefu kufanyiwa vipimo vya lazima saa 48 kabla ya kuanza safari zao.

Waziri Utalii Najib Balala amewashukuru wafanyakazi wote wa Afya kwa kuwa mstari mbele katika vita dhidi ya ugonjwa wa corona.
Amesema kwamba sekta ya ulatii imeathiriwa sana na virusi vya corona.

''Tunataka kuifungua sekta ya Utalii polepole kwasababu ndio ilioathirika vibaya na corona'', alisema bwana Balala.
Amewaomba Waislamu kuheshimu mikakati ya kukabiliana na corona ili kuzuia maambukizi.

''Wakati unapofungua baada ya kufunga mchana kutwa , usikaribiane na watu , kula pamoja kwa makundi ni sharti kusitishwe'', alisema.
 
Wamefunga mipaka lakini kesi zinaongezeka kila siku nini tatizo? MK254

Maana ndugu zenu wanazamia kinyemela na kutuambukiza sana, haswa Mombasa sijui mnaingiaje. Mtatengwa na majirani wote, Zambia wamewafungia.
 
Maana ndugu zenu wanazamia kinyemela na kutuambukiza sana, haswa Mombasa sijui mnaingiaje. Mtatengwa na majirani wote, Zambia wamewafungia.
Basi itakuwa mmefeli ikiwa mmefunga mipaka na watu wanapita
 
Watu wabaya sana hawa watz, wanataka sambaza virus dunia nzima kwa uzembe wao!
Ona wanavomaliza majirani

Muendelee kuwatenga na kuwafukuza wakafie kwao kusiko na maendeleo hawafai hata kidogo wana undugu na Wuhan China
Maana ndugu zenu wanazamia kinyemela na kutuambukiza sana, haswa Mombasa sijui mnaingiaje. Mtatengwa na majirani wote, Zambia wamewafungia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wabaya sana hawa watz, wanataka sambaza virus dunia nzima kwa uzembe wao!
Ona wanavomaliza majirani
Muendelee kuwatenga na kuwafukuza wakafie kwao kusiko na maendeleo hawafai hata kidogo wana undugu na Wuhan China

Sent using Jamii Forums mobile app

Yamekua haya pale Zambia, jamaa wanataka kuingia Zambia bila hata barakoa...hehehe

2396251_20200511_100332.jpg
 
Back
Top Bottom