Kenya: Waziri, Katibu wa Wizara ya fedha na wenzao wapandishwa kizimbani Mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
754
3,097
Picha
Waziri wa Fedha wa Kenya, Henry Rotich, Katibu wa wizara hiyo Kamau Thugge na wenzao leo wamepandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Milimani kujibu mashitaka yanayowakabili.

Washitakiwa hao wanakabiliwa mashitaka ya ufisadi kwenye ujenzi wa mabwawa Arror na Kimwarer.

Hakimu Douglas Ogoti amesoma mashitaka yanayowakabili na wamekana.

Miongoni mwa mashitaka yanayowakabili ni matumizi mabaya ya ofisi, kuanzisha mradi bila kuwa na mpango mahususi wa kuutekeleza, kukiuka taratibu za manunuzi na kula njama ili kujipatia fedha kinyume cha taratibu

Rotich anadaiwa kukiuka taratibu za manunuzi na kutoa mkataba wenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani milioni 450 kwa kampuni ya CMC de Ravenna ya Italia ijenge mabwawa hayo.

Machi mwaka huu, Rotich alikanusha tuhuma hizo za ufisadi.
 
Binafsi niliipenda sana kauli mbiu ya Uhuruto wakati wa uchaguzi ilikuwa hivi " Tunasema na Kutenda"

Na kweli maneno na matendo yao yanaendana

Ingependeza kama CCM wakaiga hili kwa wale waliofisadi mali za chama
 
Hapo nipo utakapokuja kujua chanzo halisi cha neno SIRIKALI
 
CCM iige nini haswa?? Kuwapa wapinzani uongozi kwa karatasi au??
Kenya wenzetu hata mahojiano ya kamati za bunge yanarushwa live kupitia TV. Hapa kwetu ni siri halafu wakitoka vinaanza vijembe (Sakata la CAG) au anatumwa Musiba aongee (uhakiki wa mali za CCM)
 
Picha
Waziri wa Fedha wa Kenya, Henry Rotich, Katibu wa wizara hiyo Kamau Thugge na wenzao leo wamepandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Milimani kujibu mashitaka yanayowakabili.

Washitakiwa hao wanakabiliwa mashitaka ya ufisadi kwenye ujenzi wa mabwawa Arror na Kimwarer.

Hakimu Douglas Ogoti amesoma mashitaka yanayowakabili na wamekana.

Miongoni mwa mashitaka yanayowakabili ni matumizi mabaya ya ofisi, kuanzisha mradi bila kuwa na mpango mahususi wa kuutekeleza, kukiuka taratibu za manunuzi na kula njama ili kujipatia fedha kinyume cha taratibu

Rotich anadaiwa kukiuka taratibu za manunuzi na kutoa mkataba wenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani milioni 450 kwa kampuni ya CMC de Ravenna ya Italia ijenge mabwawa hayo.

Machi mwaka huu, Rotich alikanusha tuhuma hizo za ufisadi.
Hakuna kitu hapo tayari yupo nje kwa dhamana ya milioni 15.
 
Sijawahi fika Kenya, kwa habari zao kwenye mitandao, magazeti etc inaonekana wana utawala wa kisheria zaidi. Tanzania mfumo wa kimahakama unayumbishwa na siasa, itatuchukua muda kuyaweka mambo sawa kutumia walau viwango vya kutowatenga waharifu, na Magereza kuwa mahala pa vibaka na wezi wa kuku tu.
 
Back
Top Bottom