Kenya wazima simu fake!

Twilumba

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
11,540
12,398
Mamlaka ya mawasiliano nchini Kenya yazima kiteknolojia simu zote zilizofeki ambazo zimekua zikitumiwa na wakenya.


Mtangazaji wa Citizen Tv/Radio William Tuva ameripoti kwamba wakenya walionunua simu feki wapo kwenye wakati mgumu na itawabidi wanunue simu original kwa sasa ili kurudi tena kwenye mawasiliano.



Ameripoti pia kwamba inasemekana katika mtandao wa simu za mkononi wa Safaricom peke yake ni wateja laki sita ambao wameripotiwa simu zao kuzimwa kwa sababu ni feki.



Kwenye line nyingine Tuva ameripoti pia kwamba Kenya imepoteza mabilioni ya shilingi kutokana na simu feki ambazo zimekua zikiingia sokoni kwa njia ambayo sio halali.



Baadhi ya wananchi ambao simu zao zimefungwa wamekaririwa wakisema waliamka asubuhi na kukuta simu zao hazifanyi kazi, kumbe tayari zimeshazimwa kiteknolojia na tume ya mawasiliano nchini humo ambapo kwa mujibu wa BBC ni wateja milioni mbili na nusu ambao simu zao zimezimwa.


Mmoja wa watu hao amekaririwa akisema “usiku ninawekaga alamu nataka saa 11 niamke, sikusikia naamka tu naona nje kunapambazuka na simu yangu wamezima’

MY Take: Hii ni njia moja wapo ya kudhibiti Bidhaa fake na kwa kufanya hivi ni onyoo kwa wale wanaoingiza bidhaa hizo.

Swali: Je Tanzania haiwezi kuiga mbinu na teknolojia kama hiyo kudhibiti utitiri wa bidhaa fake kama simu ambazo mwisho wake ni athari kwa watumiaji?

Kwa kufanya hivyo tume itakuwa imeonesha juhudi na makali ya kutetea wananchi wake!
 
Hapa Bongo wanaopaswa kuzizima ndio hao hao wenye maduka ya simu feki. Wakizima, Yesu atashuka!!!
 
wakizima hapa wauza chips na mshkaki sijui tutakua tunawatafutaje kuweka order jikoni :biggrin1:

Tatizo ni kuwa asilimia kubwa ya waingizaji wa hizo simu fake ndo wenye kutoa maamuzi!
subiri uone siasa zitakavyokuwa nyingi hy issue ya kuzizima simu fake ikiwa introduced!
kuna wanasiasa watakufa kwa pressure!
 
Hawa wenzetu wako serius na kazi na bidhaa feki
najua kama tukiamua tunaweza ila sisi tz hatuna haja ya
kuzima simu tuzuie ufisadi kwanza ,usafirishwaji wa twiga nje
haya yatakuja tu
 
Mi nafikiri wakileta hapa kwetu zote zitafanya kazi kama kawa!

Kwanini Tanzania yetu isiige hili?? Ama hawana vyombo paswa kwa kazi hiyo??
 
Mimi nadhani ni bora na TCRA wachukue hatua ya kuzima....ni bora tuanze kuchukua hatua mapema. Hata kama katika watumiaji milioni 20 wa simu za mkononi,milioni 18 tukiathirika mimi naona ni sawa.
 
Hapa Bongo wanaopaswa kuzizima ndio hao hao wenye maduka ya simu feki. Wakizima, Yesu atashuka!!!
Kuna thread moja iliwekwa hapa ikisema kwa nn kila mara tunaipigia Kenya mfano. Pamoja na matatizo yao kadhaa, lakini nadhani Kenya itabaki kuwa mwalimu kwa Tz. Mambo kama haya ni muhimu kujifunza toka kwao.
 
Hivi ni kuzima simu fake au laini ambazo hazijasajiliwa? If it is the former how is it practically possible? educate me please
 
kwani lazima tuige kila kitu kenya? mbona kuna bidhaa feki nyingi toka hk hk kenya ? nakwanini tusianze na pikipiki feki nguo vyombo vyakula madawa feki kwanza ?kwani lazima cm ?kwanini ? au kwasababu kenya wameanza ? tuache hizo tujifunze kuwa na maamuzi yetu binafc
 
Mbna watatutesa huku mtwara maana mtu anaweza akaikataa blackberry mbele ya mchina
 
Tanzania nayo ifanye jambo hilo. Tumechoka na bidhaa feki za kichina. Tena Tanzania hiyo teknolojia ikija iende mbali zaidi kwa kuhakikisha bidhaa zote feki zilizoko sokoni na zilizonunuliwa hazifa nyi kazi. Hiyo itakuwa ndio mwisho wa kuingizwa kwa bidhaa feki nchini..................., hilo ni wazo tu, wataalamu wa teknolojia watafafanua kuona kama jambo hilo linawezekana.
 
Hapa Bongo wanaopaswa kuzizima ndio hao hao wenye maduka ya simu feki. Wakizima, Yesu atashuka!!!

Haswa wale wakuu wa tech ndio wamililk na waingizaji wakubwa wa sim fake.
Hawawezi hata kidogo kuzizima !
 
je hapa kwetu tz, watawala wamechukua hatua gani kuzuia gharika la simu hizo hapa kwetu maana importers wa kenya wataleta bidhaa hizo hapa nchini for obvious reasons?! au wameupiga wapono ili baadae waunde tume ya kuchunguza na kujichotea mamilioni?!
 
Back
Top Bottom