KENYA;- WATU WANNE WAFARIKI BAADA YA GARI KUKANYAGA BOMU MANDERA

MOTOCHINI

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
25,728
2,000
WATU wanne wamefariki, 11 wamejeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakitumia kusafiri kukanyaga kilipuzi saa sita adhuhuri Ijumaa mjini Mandera.
Kamishna wa Kaunti ya Mandera, Fredrick Shisia, amethibitisha tukio hilo la saa sita akisema gari aina ya Toyota Landcruiser lililokuwa limebeba watu 15 kutoka Elwak kwenda mjini Mandera limekanyaga kilipuzi.
“Gari hilo husafirisha abiria na lilikuwa na wasafiri 15 lilipokanyaga kilipuzi hicho," amesema Bw Shisia.
Mwenyekiti wa usalama katika kaunti amesema machifu wawili ni miongoni mwa waliotembelewa na mkasa huo.
Walioumia wamelazwa katika hospitali ya kaunti ndogo ya Lafey.
Bw Shisia amesema eneo hilo ni hatari sana kwa sababu wahalifu wamezidisha makuruhu.

Amesema idara ya usalama inafanya kulihali kuimarisha hali.
Maeneo hatari ni Fino, Lafey na Arabia kwa sababu yako karibu na mpaka.
Mei 2017 msafara wa gavana wa Mandera Ali Roba ulishambuliwa na maafisa wa polisi watano wakauawa.
Hata hivyo Shisia amekataa kuhusisha tukio la leo Ijumaa na lile la msafara wa gavana akisema katika moja lake, Al-Shabaab walikiri kuhusika.
Hajasema ni lipi hasa linahusishwa moja kwa moja na Al-Shabaab.
 
kijani11

JF-Expert Member
Jan 19, 2014
6,270
2,000
Pole kwa majeruhi wapate nafuu haraka na waliofariki wapumzike kwa amani.
 
MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
18,846
2,000
Habari za hivi punde zinasema wamefikia watano
Jamaa hawana chakupoteza
Bado mambo yanaendelea
Vipi umefutari maana naona una mihemko ya kushabikia ndugu zako hawa. Hivi mazombi mbona hata kwenye mwezi wenu huu lazima mulipuke lipuke, hamnaga hata muda wa kupumzika haya mambo ya damu. Nilijua kwenye mwezi wa mfungo ni muda wenu wa kuvaa makanzu na kuwa watulivu, lakini imekua kinyume maana duniani kote ni taarifa za milipuko tu.
 
MOTOCHINI

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
25,728
2,000
Vipi umefutari maana naona una mihemko ya kushabikia ndugu zako hawa. Hivi mazombi mbona hata kwenye mwezi wenu huu lazima mulipuke lipuke, hamnaga hata muda wa kupumzika haya mambo ya damu. Nilijua kwenye mwezi wa mfungo ni muda wenu wa kuvaa makanzu na kuwa watulivu, lakini imekua kinyume maana duniani kote ni taarifa za milipuko tu.
Kwanza hao Mazombi ndio kinanani!?
 
Zuwenna

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
1,826
2,000
Vipi umefutari maana naona una mihemko ya kushabikia ndugu zako hawa. Hivi mazombi mbona hata kwenye mwezi wenu huu lazima mulipuke lipuke, hamnaga hata muda wa kupumzika haya mambo ya damu. Nilijua kwenye mwezi wa mfungo ni muda wenu wa kuvaa makanzu na kuwa watulivu, lakini imekua kinyume maana duniani kote ni taarifa za milipuko tu.
Ila haya makundi Nani anayafadhili?
Tuanzie hapo kabla ya kulaum dini za watu
 
Jay456watt

JF-Expert Member
Aug 23, 2016
10,373
2,000
pole kwa familia zao....dah! naona wakenya wa kawaida wahamishwe kule wabaki wanajeshi pekee yake....hawa jamaa sioni kama watawahi kuisha..ni bora serikali iwahamishe raia...ila nimeshangazwa.....MOTOCHINI kafurahi watu wakifa...
 
Jay456watt

JF-Expert Member
Aug 23, 2016
10,373
2,000
Ila haya makundi Nani anayafadhili?
Tuanzie hapo kabla ya kulaum dini za watu
yaani ndio swali ambalo najiuliza kila uchao...ni nani anawafadhili hawa al shabaab? hivi hizi mabomu za kisasa wanazotumia wanazitoa wapi? kulikuwa na fununu hivi majuzi kuwa ni serikali ya Qatar ila hilo halijathibitishwa..ktk swala la dini, sijui tulaumu Islam ama kwasababu magaidi wana imani za kijinga kwel kwel...hivi, ni ukweli kuwa ukiwauwa wakristo ama kafiri utawekwa pema peponi? pengine waislamu waje wanithibitishie hili...pia, nimeskia kuwa al shabaab nia yao ni kubatilisha uongozi wa serikali ya Somalia inayosapotiwa na wamarekani ndio wawe na sheria mpya za utawala almaarufu 'Shariah law'...hilo tu ndio ninalolijua..
 
MOTOCHINI

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
25,728
2,000
pole kwa familia zao....dah! naona wakenya wa kawaida wahamishwe kule wabaki wanajeshi pekee yake....hawa jamaa sioni kama watawahi kuisha..ni bora serikali iwahamishe raia...ila nimeshangazwa.....MOTOCHINI kafurahi watu wakifa...
Sifurahii watu kufa
Ila kama ungelikuwa humu jf muda kidogo unge elewa,
Tumekuwa tukiwaeleza wakenya
Hawa watu hawana chakupoteza
Hawa ni habari nyingine kabisa
Mjiulize kwanini Marekani alikimbia Somalia!?
Mnapaswa kulinda mipaka yenu
Na mkubari Mna jeshi la hovyo.
 
MOTOCHINI

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
25,728
2,000
yaani ndio swali ambalo najiuliza kila uchao...ni nani anawafadhili hawa al shabaab? hivi hizi mabomu za kisasa wanazotumia wanazitoa wapi? kulikuwa na fununu hivi majuzi kuwa ni serikali ya Qatar ila hilo halijathibitishwa..
Jiulize hayo
Lakini mtu pekee mchafua mambo ni Mmarekani
Shangirieni kupewa misaada ya siraha na huyo
Lakini mjue mtaendelea kuwa chambo.
Serikali ya Kenya kunavitu inaficha,
Kuna kinamama wakikenya zaidi ya 300
Wanashikiliwa mateka
Nakufanyiwa vitendo vya hovyo
Ktk misitu ya Somalia,
Wanakusanywa kila siku
 
Jay456watt

JF-Expert Member
Aug 23, 2016
10,373
2,000
Sifurahii watu kufa
Ila kama ungelikuwa humu jf muda kidogo unge elewa,
Tumekuwa tukiwaeleza wakenya
Hawa watu hawana chakupoteza
Hawa ni habari nyingine kabisa
Mjiulize kwanini Marekani alikimbia Somalia!?
Mnapaswa kulinda mipaka yenu
Na mkubari Mna jeshi la hovyo.
ooooh nimekuelewa sasa....kumbe ni hili jambo la Kenya vs TZ...haya nimekubali...wanajeshi wetu ni hovyo...I assume sasa utasema TZ forces are stronger...right?
 
MOTOCHINI

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
25,728
2,000
ooooh nimekuelewa sasa....kumbe ni hili jambo la Kenya vs TZ...haya nimekubali...wanajeshi wetu ni hovyo...I assume sasa utasema TZ forces are stronger...right?
Hayo niyako
Lakini huko mie siko
Nacho kizungumzia ni kile kinacho onekana
Imalisheni ulizi wenu kwanza,
Somalia ni mfupa ulio mshinda fisi
 
Jay456watt

JF-Expert Member
Aug 23, 2016
10,373
2,000
Hayo niyako
Lakini huko mie siko
Nacho kizungumzia ni kile kinacho onekana
Imalisheni ulizi wenu kwanza,
Somalia ni mfupa ulio mshinda fisi
ulinzi unaimarishwa kila uchao...nazan hawa magaidi hawawezi wakaisha kabisa...sioni wakiisha...cha msingi ni kuwa relocate wakenya waliopo Mandera mahali pengine wabaki wanajeshi pekee yake...they are becoming easy targets for terrorists...karibu wamwue Gavana wa Mandera hivi majuzi...duh!
 
aganza

JF-Expert Member
Mar 9, 2017
1,452
2,000
Vipi umefutari maana naona una mihemko ya kushabikia ndugu zako hawa. Hivi mazombi mbona hata kwenye mwezi wenu huu lazima mulipuke lipuke, hamnaga hata muda wa kupumzika haya mambo ya damu. Nilijua kwenye mwezi wa mfungo ni muda wenu wa kuvaa makanzu na kuwa watulivu, lakini imekua kinyume maana duniani kote ni taarifa za milipuko tu.
Umefutari=umefurahi
 
MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
18,846
2,000
Umefutari=umefurahi
Mbona unanilazimisha kusema kitu tofauti na nilichokusudia, kwani kwenye huu mwezi kawaida jioni huwa mnakula nini hicho kama sio futari.
Huyo hapo namuuliza kama amefutari kabla hajaanza mihemko ya kushabikia magaidi kwenye mwezi huu niliodhani huwa mnavaa makanzu na kuwa watulivu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom