KENYA: Wanafunzi wamshushia kipigo Mkuu wa Shule kisa uji hauna sukari

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,121
Wanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari God Bura iliyoko Homa Bay Kenya,wamemvamia mkuu wa shule hiyo kisha kumshushia kipigo katika kile kilichodaiwa amewapa uji hauna sukari.

Mwalimnu huyo aliyetambulika kwa jina la Collins Omondi alivamiwa na wanafunzi hao alipokuwa nyumbani kwake Ijumaa mwishoni mwa wiki kisha kumpiga na kuahidi kumpeleka polisi.

Inasemekana wanafunzi hao walimtoa nje ya nyumba yake kisha kumpiga mateke na makofi huku wakimshtumu kwa kuruhusu wapishi kuwapa uji bila sukari.

Tovuti ya Tuko imesema, mwalimu Omondi alikimbizwa Hospitali ya Magunga kwa uchunguzi zaidi kutokana na majeraha ya kifuayaliyotokana na kipigo hicho.

Tukio hilo kwa sasa linachunguzwa na polisi wa Kaunti ya Homa Bay na Wizara ya Elimu, huku baadhi ya wazazi vwakishukiwa kushiriki.

Pia, wanafunzi walimshutumu Omondi kwa kusimamia vibaya shule hiyo, huku wakisisitiza kumpeleka katika Kituo cha Polisi cha Magunga akaeleze jinsi fedha za shule hiyo zinavyotumika.

Mwenyekiti wa Chama cha Wakuuwa Shule za Sekondari, Paul Mbara amelaani tukio hilo,akiwataka wazazi na wanafunzi kutafuta mbinu nyingine za kutatua migogoro."Kumvamia walimu sio suluhu la matatizo yanayozikabili shule. Kuwe na njia mbadala za kutatua migogoro," amesema Mbara.
 
Pale wanafunzi wanapoamua kuwa makini na hela za wazazi wao, hawataki hata mia ipotee,kapewa kipigo na bado tena wanataka wasema hela zimeenda wapi, hawa wakiwa wakubwa kuingia barabarani kukiwasha ni sekunde
 
Back
Top Bottom