Kenya wakubali rasimu ya katiba mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kenya wakubali rasimu ya katiba mpya

Discussion in 'Kenyan News and Politics' started by mfianchi, Aug 6, 2010.

 1. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #1
  Aug 6, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Hongera wananchi wa Kenya kwa kuikubali rasimu ya katiba mpya,hongereni sana sisi wenzenu wa Tanzania bado tuko kwenye usingizi wa pono,lo!nawaonea wivu mnapopuliza Vuvuzela kushangilia ushindi,sijui ni lini na mimi hapa nitakuja kupuliza vuvuzela kushangilia mabadiliko ya katiba yetu ambayo imejaa viraka kiasi kwamba hata viraka vyenyewe vimechoka kwani vinaachia uzi kwa kuzidiwa na uzito wa kuwekwa viraka vipya kila kukicha,sasa ni wakati wa kupata nguo mpya na kuitupa hiyo iliyojaa viraka,ni Mtikira peke yake ambaye anaona hii nguo ya viraka inatuaibisha wa TZ anataka tuvae nguo mpya ili tujisitiri maungo yetu lakini loh ni kama vile sauti za mtu aliae aliye nyikani
   
Loading...