Mabadiliko ya Katiba ya Kenya, wanaodai Katiba Mpya Tanzania mnalo la kujifunza

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
9,895
22,659
Bunge la Kenya lipo kwenye mjadala wa kufanya mabadiliko makubwa ya Katiba yake kwa kinatajwa na muungano wa Kenya Kwanza ya Rais Ruto kuunganisha taifa, hii ni baada ya mpango wa Rais Kenyatta wa BBI kukataliwa na Majaji huku pande mbili za kieleweke na tangatanga zikiumana kipindi hicho.

Katiba ya Kenya ya mwaka 2010 iliyotangazwa na marehemu Mzee Kibaki na mshindani wake Raila wakiwaambia wakenya kuwa italiweka pamoja taifa kitu kilichoshindika ,italeta maendeleo kitu kilichoshindika hali ya maisha ya wakenya ni ngumu licha ya Serikali kuzidiwa madeni ya ndani na nje.

Hapa Tanzania kuna kundi tangu mwanzo linadai eti katiba mpya italeta usawa na kuwa jawabu la mambo yote ya kiuchumi na kijamii kitu ambacho si kweli, usalama wa Kenya uko hoi mauaji, utekaji, na wanasiasa sasa wanaopinga Ruto wanatamani kukimbia nchi licha ya katiba mpya huku wapinzani wakiandamana kupinga matokeo na kutotambua matokeo kuwa kuwa tume ya uchaguzi ilimpendelea rais Ruto kama hapa Tanzania wapinzani wakigomea matokeo ya 2020

My take: Baada ya Tanzania kupata Katiba tutajikuta matatizo yetu yapo palepale maana watu ni walewale tu


USSR
 
Mtu wa Ntwara anatamani afike Dar. Akifika Dar anatamani afike Johannesburg. Akifika huko anatamani afike Ulaya.

Ndivyo walivyofanya Kenya. Wameenda hatua nzuri wameiona nyingine mbele ni nzuri zaidi.

Sisi bado tuko gizani na katiba ya kikoloni iliyobadilishwa heading tu
 
Kenya wametuacha mbali mno ktk jinsi wanavyoisimamia Serikali,

Au jinsi Serikali inavyowajibika Kwa wananchi.

Tutachukua tahadhari tusifanye makosa walofanya.

Bt Kwa ujumla, kupata KATIBA mpya ni jambo muhimu sana Kwa ustawi wa Nchi yetu.

Aaamen
 
Makubaliano ya nyerere na karume hayatuhusu kwa Sasa , tunahitaji katiba ya wananchi wa Tanganyika wa Zanzibar
 
Rais wa muungano anatakiwa azungumzie mambo yanagusa pande zote mbili sio Tanganyika tu
 
Akili zako zimesimama mahali, nenda kazichukue, unawashangaa wakenya kupiga hatua kuelekea kujikomboa kijamii na kiuchumi kwa kuifanyia marekebisho katiba yao, hujui hao ndio watawahi kufika kabla yetu.

Wakati sisi hata katiba Mpya bado hatujaipata, hatujafahamu itakuwa na mapungufu gani ili tuyafanyie kazi, wenzetu wakenya wanazidi kusonga mbele, ajabu wewe unataka sisi tuendelee kusimama hapa hapa tulipo.
 
Back
Top Bottom