Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,315
- 45,624
Ikiwa ni miaka 13 tangu Kenya iwe na katiba mpya bado katiba hiyo inaonekana kushindwa kutatua mambo ya msingi, haya ni baadhi
1. Ufisadi na Rushwa
Kenya bado inaendela kuwa mojawapo ya mataifa yenye kiwango kikubwa cha ufisadi barani Africa. Pesa za umma zinaibwa kwa kiwango cha juu sana. Katiba yao mpya haijaleta utofauti wowote katika suala hili.
2.Ukabila
Tatizo la ukabila bado ni sugu Kenya. Kura katika uchaguzi bado zinapigwa kwa mrengo wa makabila, ajira katika baadhi ya kaunti zinatolewa kwa ukabila, pia ajira za serikali kuu awamu zinatolewa kwa ukabila ambapo nafasi nyingi muhimu zinachukuliwa na watu kabila la Ruto, mfano katika wizara ya nishati ya Kenya nafasi zote za juu wamepewa Wakalenjini.
3.Udini
Kwa sasa nchini Kenya hakuna msitari kati ya dini, siasa na uongozi. Siasa zinafanyika katika makanisa na misikiti na pia dini hasa ya Ukristo imegeuza ofisi za serikali hasa Ikulu kuwa jukwaa lake la mahuburi na ibada.