Kinachofanywa na Ruto wa Kenya Kinathibitisha Kwamba Kinachoitwa Katiba Mpya ni Fix ya Wanasiasa waroho Kutafutia Madaraka

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,115
49,832
Mara kadhaa Chadomo imekuwa ikiwaaminisha watu kwamba Katiba Mpya ndio muarobaini wa Maisha Bora,Utawala Bora na Maadili Bora.

Kwa kinachoendelea Kenya chini ya William Ruto,Pasi na shaka Kinathibitisha Kwamba Katiba Mpya ni "bosheni" ya kuwadanganyia wajinga.

Kwa miezi 3 ya Maandamano Toka yameanza ni zaidi ya watu 30 wameuwawa huku Wanasiasa wa Upinzani akiwemo Rais Mstaafu wakifanyiwa Harassments na vyombo vya Dola..

Kenya ,South Africa nk wanafanya hayo yote mbele kabisa ya Kinachoitwa Katiba Mpya inayohubiriwa na Chadema.

Naendelea kuwakumbisha watu kwamba Katiba Mpya haitekelezwi na malaika Bali na Hawa Hawa watu,Katiba Mpya bila watu wenye Maadili ni sawa na chupa Mpya ila mvinyo ni Ile Ile.

Mwisho Naomba Chadomo mnipe jibu,Iko wapi Katiba Mpya Mnayohubiri Kuzuia hayo yote?

My Take
Acheni Fix na "Utapeli wa Kisiasa" kudanganya Wajinga Ili muwafanye ngazi za uhoro wenu wa madaraka.
 
Back
Top Bottom