Kenya vs Tanzania: PLO Lumumba weighs in!

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
97,063
Reaction score
136,426

View: https://youtu.be/NOoBaOwO6g8?si=_q8xG3hw918zLpm7

Mwana-umajumui wa Uafrika kutoka Kenya katoa maoni yake kwenye chaneli ya Fanya Mambo Afrika kuhusu mambo yaliyojitokeza wiki iliyopita hapa Tanzania kuhusu baadhi ya wanaharakati waliokuja nchini kwa ajili ya kesi haramu inayomkabili Tundu Lisu.

Cha kuchekesha [kwa maoni yangu], huyu jamaa bado ana zile ndoto za Alinacha kuwa jumuiya ya Afrika Mashariki siku moja itaungana katika shirikisho la kisiasa na hatimaye kuwa nchi moja, hali ambayo lengo na hatima yake kuu ni bara zima la Afrika kuja kuungana na kuwa taifa moja [jambo ambalo haliwezekani].

Kazungumzia katiba mpya ya Kenya na kadokeza kuwa kuna mambo ambayo [kisiasa] Kenya yanakubalika lakini ambayo yanaweza yasikubalike Tanzania na Uganda.

Halafu hapo hapo anazungumzia habari za nchi kuungana na kuunda taifa moja 🤣.

Vilevile kazungumzia kuhusu kipenzi chenu Ibrahim Traore na hao madikteta uchwara wenzie wa huko Sahel.

Hawa majamaa nao wamejitoa ECOWAS na wameunda jumuiya yao ya AES.

Ni mazungumzo mazuri kwa ujumla. Yaangalie kisha toa maoni yako.
 
  • Thanks
Reactions: K11

Traore ni kipenzi chako we na nani, acha kudandia mambo usiyoyajua.
 
Back
Top Bottom