KENYA : Serikali kupeleleza mawasiliano ya simu za raia

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
70e23c16bb09654a3b10a67c5a407c87.jpg
Mamlaka nchini Kenya imeanzisha harakati ya kuzishurutisha kampuni za simu nchini kuruhusu vitengo vya kijasusi kudukua mawasiliano ya raia

Mamlaka ya mawasiliano nchini humo CAK imewaandikia wahudumu wa Simu ikitaka kuchunguza Mitandao yao, hatua itakayowapatia uwezo kudukua simu zinazopigwa, ujumbe mbali na shughuli za kifedha

Mpango huo utasababisha wamiliki milioni 30 wa Simu nchini humo kupoteza hali yao ya faragha pamoja na uaminifu

Wahudumu hao wa Simu ni Safaricom, Airtel na Orange

Mamlaka hiyo inasema kuwa mpango huo ambao pia unalenga kupiga marufuku simu bandia unatarajiwa kuidhinishwa ifikiapo wiki ijayo

Hata hivyo kumekuwa na ukosoaji mkubwa wa mpango huo katika vyombo vya habari

Chanzo: BBC /Swahili
 
Back
Top Bottom