Kenya: Msikiti wenye jina la "Jesus Christ sun of Mary"

Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,944
18,654
Kenya mjini kisumu, umeanzishwa msikiti mpya wenye jina la " The Mosque of Jesus Christ the son of Mary".

Hii imetoa gumzo kubwa hasa kwenye mitandao wa kijamii huku wengi wakihoji huu ni msikiti au kanisa.

Abdul Rashid ambaye ni Mwadhini wa msikiti huo, alihojowa na gazeti la The Standard la Kenya na kusema kuwa '' Tumekuwa na mvutano wa muda mrefu kuhusu ardhi na hii ni moja ya sababu zilizotufanya kuchagua jina hili. Sisi hatuna uadui na Wakristo,'' alisema.

Amesema kuwa Waislamu pia wanaamini Yesu na kuwa alikuwa sambamba na manabii wanne akiwemo Mtume Muhamad (S.A.W).

''Waislamu wanaamini katika Yesu Kristo . Uchaguzi wa jina pia ni shukrani ya Yesu Kristo ambaye tunaamini atarudi tena," Rashid aliliambia gazeti la The Standard.


Mipango ya kujenga msikiti wa kudumu inaendelaa ingawa Waislamu wanaoabudu kwenye eneo hilo wamejenga jengo la muda mfupi kwa ajili ya kuswali.

Baadhi ya waumini wa Kikristo wamepokea kwa mikono miwili hatua hii wakisema kuwa itajenga hali ya kuishi kwa amani.

Hili si tukio geni hata hivyo kwani jina la The Mosque of Jesus Christ" limepewa pia Msikiti ulio katika mji wa Madaba, Kusini mwa mji mkuu wa Amman huko Jordan, Msikiti huu ulianzishwa mwaka 2008 kwa ajili ya kutoa ujumbe wa umoja na kustahimiliana miongoni wa dini hizo mbili.

Source:BBC swahili.
_116049488_8ea5cb09-cccb-4335-b7dc-abb2b91469e5.jpg
 
Hawa wamekili kuwa ni mtoto wa Mariam. Hii haina uhusiano na Mungu, mbona hata mimi naitwa mtoto wa Bi. Eliza
Wangesema ni mtoto wa Joseph sasa kama sio wa mungu, kwanini waseme wa maliamu? Wewe kwenye jina lako wapi kuna jina la mama yako?
 

Philippians 2:11

and every tongue acknowledge that Jesus Christ is Lord, to the glory of God the Father.

Wafilipi 2:11

na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.
AMINA
 
Yule tajiri wa Jordan Al Oteibi alihojiwa kuwa kwanini msikiti alioujenga yeye aliupa jina ''The Mosque of Jesus Christ' akajibu hivi :-
Screenshot_20201213-171859~2.jpg
 
Wangesema ni mtoto wa Joseph sasa kama sio wa mungu, kwanini waseme wa maliamu? Wewe kwenye jina lako wapi kuna jina la mama yako?
Kwani sio mtoto wa Maria/Mariam?
Kwangu hakuna jina la mama kwenye ukoo ila naitwa mwana wa Bi. Eliza, hilo nalo linataka ukoo kujua mama yangu mzazi?
 

Philippians 2:11

and every tongue acknowledge that Jesus Christ is Lord, to the glory of God the Father.

Wafilipi 2:11

na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.
Hujui kusoma ama huna uwezo wa kuelewa kilichoandikwa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom