Kenya: Mgonjwa wa kwanza wa Corona afariki dunia

MGONJWA WA KWANZA WA CORONA AFARIKI KENYA

Kenya imetangaza kifo cha kwanza cha mgonjwa wa virusi vya #Corona, mgonjwa huyo wa kiume alikuwa na umri wa miaka 66 na alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kisukari amefariki mchana wa leo katika Hospitali ya Agha Khan.

Kenya imetangaza kifo cha kwanza cha mgonwa aliyekuwa akiugua virusi vya corona.

Mwathiriwa huyo ambaye ni raia wa Kenya mwenye umri wa miaka 66 aliaga dunia nyakati za mchana katika chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali ya Agha Khan ambako alikua amelazwa.

Raia huyo ambaye alikua akiugua ugonjwa wa kisukari alikuwa amewasili nchini tarehe 13 mwezi Machi kutoka Afrika Kusini kupitia Swaziland.

Katika taarifa yake iliotiwa saini na waziri wa Afya Mutahi Kagwe, serikali ilisema kwamba ilipokea kwa huzuni habari za kifo cha Mkenya huyo ambaye alikuwa amekutwa na virusi hivyo baada ya kupimwa

View attachment 1400131
Rip
 
Kama amekosea kwa nini nisimsahihishe?
Amekosea lugha ama ujumbe umekosewa na haueleweki? Iama ni lugha basi wengi wanakosea. Ila ujumbe unaeleweka. Lugha sio sababu kubwa sana tuijadili maana kwenye lugha hakuna aliekuwa perfect sana.
Mbona wewe umeandika kwa nini badala ya kwanini
 
Kiukweli lockdown...inaogopesha...maana ni mawili...

Tufe kwa njaa au tufe kwa CORONA.
Maskini tutaumia SANA...wale tuliozoea kupima unga nusu na robo...

Everyday is Saturday....................... :cool:
nilidhani Tanzania chakula ki'tele, kumbe munahofia njaa?
 
Back
Top Bottom