Kenya Mahakama ya mafisadi ipo kazini, Tanzania tunafeli wapi?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,915
141,874
Niko naangalia mubashara mwenendo wa kesi ya ufisadi inayomkabili Gavana Sonko wa jiji la Nairobi na wenzake wanaotuhumiwa kufisadi fedha za serikali kwenye manunuzi ya umma. Tukio hili linarushwa live kupitia Citizen Tv.

Hapa Tanzania tunayo mahakama ya mafisadi lakini sijaisikia ikiendesha kesi zaidi ya kuwaona mafisadi wakipandishwa pale Kisutu, tunafeli wapi?

Maendeleo hayana vyama!

nairobi_governor_mike_sonko_at_the_milimani_law_courts_december_11_2019_0_0.jpg

Gavana wa Nairobi Mike Sonko wakati wa kusikilizwa kwa dhamana mnamo Desemba 11, 2019.
 
Siasa tu hizo, asikudanganye mtu, isitoshe hakuna Mkenya atakwambia anaangalia TV ya TZ akifwatilia Siasa za TZ, lkn ni kawaida kukuta nyumbani kwa Mtanzania familia nzima wanafwatilia TV za Kenya.
 
Siasa tu hizo, asikudanganye mtu, isitoshe hakuna Mkenya atakwambia anaangalia TV ya TZ akifwatilia Siasa za TZ, lkn ni kawaida kukuta nyumbani kwa Mtanzania familia nzima wanafwatilia TV za Kenya.
Sasa unataka mkenya aangalie TBC au safari channel inayoonyesha majengo ya TANU?
 
CCM na wizi wa fedha na Mali za Umma ni kama uji wenye tangawizi na mgonjwa wa TB
 
Sasa unataka mkenya aangalie TBC au safari channel inayoonyesha majengo ya TANU?
Unaijua siasa za kenya wewe mleta mada?

Unajua ni kwa nini Mike Mbugi 'Sonko' amesakamwa?

Unajua mmiliki wa Citizen TV ya Kenya?

Ukiishanijibu hayo maswali ndio nita comment hiyo thread yako.
 
Wakenya hasa wana Nairobi wanamuhitaji huyu gwiji wa rushwa maana kupitia rushwa ndio anawasidia
 
Sasa unataka mkenya aangalie TBC au safari channel inayoonyesha majengo ya TANU?

Siyo swala la TANU au TBC bali ni IQ, Kenya kuna KBC kama TBC tu, pia na Wakenya wanaangalia hata Watanzania wanaangalia KBC pia badala ya tv zetu.
 
Tatizo la mahakama ya mafisadi Tanzania kutokuwa effective ni kwa kuwa kesi nyingi ziko invoved na big shots ambao hawawezi kupelekwa Mahakamani wanapeleka hao watuhumiwa kama kielelezo. Haiwezekani kesi zinamaliza miaka 3 bado upelelezi unaendelea na mutuhumiwa anabaki kolokoloni muda wote huo kwa mateso. DPP ana mandate ya kurekebisha hali hii.
 
Siyo swala la tanu au tbc bali ni IQ, Kenya kuna kbc kama tbc tu pia na Wakenya wanaangalia hata Watanzania wanaangalia kbc pia badala ya tv zetu.
Mimi huwa nashindwa kuelewa pale mtu anapokamatwa kwa kosa kama la uhujumu uchumi alafu anapelekwa KISUTU lakini anaambiwa haruhusiwi kujibu lo lote kwa vile mahakama ile haina uwezo wa kuendesha mashitaka yake. Kwa nini asipelekwe mahakama yenye uwezo huo kwa ajli ya kutenda haki?
 
Hata mimi sifahamu, siyo Mwanasheria!
 
johnthebaptist,

Hilo Bunge lenyewe la wananchi tumepigwa biti hatulioni kisa eti tutajua mengi, sasa hiyo inayoitwa Mahakama ya Mafisadi iwe live ni leo?
 
Back
Top Bottom