Wakuu,
Kwa kadri mambo yanavyoenda Kenya , Afrika Mashariki ijiandae kuwa koloni la Kenya. Kwa kweli tukiendelea na mizaha hii hapa kwetu Tanzania, tujiandae kupokwa ile sifa aliyotuachia Mwalimu Nyerere ambapo watu wa Tanzania waliheshimika duniani kote.
Ni jambo la busara sana kwa Kikwete kuacha ubinafsi na kuwatendea haki watanzania kwa kuwapa katiba wanayoitaka ili nasi tuweze kuwajibishana ili tujenge taifa letu.Huu ndio utakuwa urithi mkubwa ambao JK anaweza kutuachia Watanzania na akabaki na sifa hadi kaburini. JK anatakiwa atupe katiba tunayoitaka. Anatakiwa asafishe mafisadi, na ufisadi ndani ya serikali yake na chama chake ili ajenge heshima mbele ya jamii. Akifanya hayo , atakuwa ametuweka mahali pazuri kupambana na Wakenya hatimaye tusije mezwa kama vidagaa na nchi hiyo yenye wajanja wengi.