Kenya kuwa kitovu cha demokrasia na maendeleo Afrika Mashariki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kenya kuwa kitovu cha demokrasia na maendeleo Afrika Mashariki

Discussion in 'Kenyan News and Politics' started by Nyumbu-, May 6, 2011.

 1. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #1
  May 6, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 969
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Wakuu,

  Kwa kadri mambo yanavyoenda Kenya , Afrika Mashariki ijiandae kuwa koloni la Kenya. Hawa watu wako serious kwa kila kitu na si mizaha inayoendelea hapa kwetu. Ukiangalia katiba yao sasa hivi , haitofautiani sana na za nchi za Magharibi, na uwajibikaji uko wazi. Hivyo mihimili yote ya dola hujitegemea na ukiharibu unawajibika mwenyewe kisheria na si kama hapa kwetu tunapobembelezana eti tujiangalie na kuvua magamba.

  Sasa hivi unaendelea mchakato wa kumpata Chief Justice, na interview zinafanyika live na kila Mkenya na dunia kwa ujumla anaangalia. Hivyo atakayepatikana ni yule anayejua kweli atawatendea nini waKenya, na si kama boya letu Werema.

  Kwa kweli tukiendelea na mizaha hii hapa kwetu Tanzania, tujiandae kupokwa ile sifa aliyotuachia Mwalimu Nyerere ambapo watu wa Tanzania waliheshimika duniani kote.

  Ni jambo la busara sana kwa Kikwete kuacha ubinafsi na kuwatendea haki watanzania kwa kuwapa katiba wanayoitaka ili nasi tuweze kuwajibishana ili tujenge taifa letu.Huu ndio utakuwa urithi mkubwa ambao JK anaweza kutuachia Watanzania na akabaki na sifa hadi kaburini. Mwinyi alituanziashia soko huria, Mkapa akaja na kujenga uchumi, JK anatakiwa atupe katiba tunayoitaka. Anatakiwa asafishe mafisadi, na ufisadi ndani ya serikali yake na chama chake ili ajenge heshima mbele ya jamii. Akifanya hayo , atakuwa ametuweka mahali pazuri kupambana na Wakenya hatimaye tusije mezwa kama vidagaa na nchi hiyo yenye wajanja wengi. AKifanya hivyo, JK nitamsamehe kwa rafu zote alizofanya kwenye uchaguzi Mkuu 2010.

  Mungu tupe hekima katika hili
   
 2. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #2
  May 6, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Mmh mkuu mbona kuna mengi sana yanafanyika! Wafanyabiashara kariakoo wanaenda kuchukua mzigo kenya badala ya zanzibar ya zamani duu!
   
 3. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2011
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,532
  Likes Received: 2,113
  Trophy Points: 280
  Hakuna 'demokrasia' ya kweli Kenya bali ni makundi ya kikabila ''KKK" kugombania nyadhifa za kisiasa kwa kisingizio cha makabila yao Kikuyu, Kalejin, Kamba (KKK) ili kuendeleza shibe zao.

  Hakika 'demokrasia' ya Kenya haifai kuigwa na nchi yoyote ya kiafrika maana ni kama kujichimbia kaburi lako mwenyewe wakati bado upo hai. Naona niishie hapo kwani kichwa chako cha habari ni 'demokrasia' ya Kenya.

  Kuhusu suala la kupambana na mafisadi pia Kenya tunaona inavyojaribu kuwalinda mafisadi kama Uhuru Kenyatta na wenzake wa Ocampo 6 (six) wasipelekwe mbele ya sheria huko The Hague, Holland baada ya kusababisha maafa makubwa kwa wananchi wa Kenya. Hivyo kwa suala la utawala wa sheria hilo pia Kenya haina haiba ya kuweza kuigwa kuwa ni mfano.

  Na tukiingia ktk suala la kiuchumi, kila nchi ya Afrika Mashariki ina 'comparative advantages' zake. Utendaji wa Bandari ya Mombasa inaweza kuwa mfano lakini tunapokuja ktk suala la Kilimo Tanzania ni nchi ya kuigwa kwa sera zake bora za ardhi na kilimo kuliko Kenya kiasi ya kwamba mazao mengi ya Tanzania yanaliwa nchi Kenya.

  Kwa maoni yangu Kenya ni mfano wa 'a failed state' ktk sehemu za kuwafaidisha wananchi walio wengi na ndiyo maana kuna vitongoji vikubwa vya mabanda a.k.a nyumba kuliko nchi yoyote ktk Afrika ya Mashariki na ya Kati.
   
 4. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #4
  May 6, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  hiyo tanzania haitatokea chini ya ccm. tuiweke ccm kwanza kando ndo tuanze mustakabali wa nchi yetu. vinginevyo kalaghabao wabongo wenzangu
   
 5. N

  Nonda JF-Expert Member

  #5
  May 6, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu.

  Hiki ni kilio,pia ni hofu.
  Yote mawili umeyatolea maelezo mazuri. Lakini unazungumza na nani?
  JK? Chama cha magamba? Au watanzania?

  Mwalimu alitambua kuwa CCM imeshapotea na imechagua hila na "janja janja" huku ikiwadanganya wananchi.

  "Ubaya wao ni kwamba jambo lenyewe walilifanya kwa hila na 'janja janja", na mpaka sasa wanaendelea kudanganya wananchi kwamba sera ya CCM bado ni Ujamaa na Kujitegemea." Uk 18

  Pia alisema.

  “Kwa kweli hata kesho Nchi za Afrika ya Mashariki zikiamua kuungana, na Tanzania ikawa ni mshiriki, naamini kuwa ni rahisi zaidi kushirikisha Tanzania yenye Serikali Mbili - ya Zanzibar na ya Tanganyika ..." Uk 11

  Uongozi Wetu Na Hatma Ya Tanzania (by Nyerere)

  Hizi hila na ujanja wa Mkulu na CCM unaonekana katika kila kitu, kujivua gamba, kupambana na ufisadi, kwenye chaguzi, sera ya muungano wa kutoka serikali mbili kuelekea moja, tatizo la umeme kuwa historia, “maisha bora kwa kila mtanzania”, katika issue ya katiba mpya….orodha ni ndefu!!! Wanapenda kudanganya umma.

  Kwa hiyo ni vyema tu tujitayarishe kuwa koloni la Kenya kama unavyosema..hiyo itatusaidia kuelewa kilio cha Zanzibar pia katika Muungano wa Tanzania.

  Sio kwamba napendelea iwe hivyo, lakini himaya za dola ziko kwa "viongozi" waliojichagua wenyewe na kwa hiyo wapo kutekeleza maslahi yao binafsi sio ya umma, sio ya wananchi wala ya taifa.

  Na unapowazindua warekebishe mambo basi watakutungia majina na kukukejeli.
  Alternative ni kuchukua uraia wa Kenya. Ili nawe uingie katika kundi la kuwa mkoloni wa Afrika Mashariki.
   
 6. n

  nomasana JF-Expert Member

  #6
  May 6, 2011
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 60
  honestly the new constitution already has and will enhance the way kenya is governed. there is a sense of accountability begin to take hold(although still very early) some government institutions are now starting to function independently and not being influenced by political figures.

  what i still fear is that there are some powerful and influential people that do not want to see the new constitution fully and correctly implemented. they want the status quo to continue. these are the forces that are threatening to derail the dawn of a new Kenya.

  i think that tanzania needs a new constitution everybody knows that but as long as CCM is in power nothing will happen. CCM has no incentives whatsoever to deliver a new constitution. they have nothing to gain from binging change in government. they want things to continue the way they are because they know that as long as nothing changes then CCM will continue its dominance in politics and hold on to power.

  FOR CHANGE TO HAPPEN IN TZ AND FOR TZ TO GET A NEW CONTITUTION, CCM GOTTA GO FIRST.
   
 7. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #7
  May 7, 2011
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Thread hatambui tofauti kati ya Mwanasheria mkuu na Jaji Mkuu. Hamna ishu...
   
Loading...