Kenya Kusaini mikataba na Dubai

Kikwajuni One

JF-Expert Member
Mar 18, 2013
13,142
6,947
WAKATI baadhi ya wanasiasa wa upinzani na wanaharakati wakipinga mpango wa kampuni ya DP World ya Dubai kuwekeza kwenye bandari ya Dar es Salaam, Kenya imetangaza maamuzi ya kusaini mikataba ya uwekezaji na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Rais William Ruto ametangaza kupitia akaunti yake ya Twitter leo kuwa amefanya mazungumzo kwenye Ikulu ya Nairobi, Kenya, na Waziri wa Mambo ya Nje wa UAE, Sheikh Shakhboot bin Nahyan Al Nahyan, kujadili fursa za uwekezaji.

"Kenya na Umoja wa Falme za Kiarabu watasaini makubaliano ya uwekezaji ambayo yataimarisha uhusiano kati ya nchi zetu na kutengeneza fursa kwa wananchi wetu," Rais Ruto alisema.

Alisema kuwa makubaliano hayo ya uwekezaji kati ya Kenya na UAE yatajikita kwenye maeneo mbalimbali, ikiwemo miundombinu ya usafirishaji.

Waziri Shakhboot wa UAE pia amefanya ziara kwenye Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kukutana na Rais Felix Tshisekedi kujadiliana kuhusu fursa za uwekezaji.

Zambia pia nayo imekuwa ikifanya jitihada kubwa kuvutia uwekezaji kutoka UAE.

Serikali ya Ruto imeanza jitihada kubwa ya kutafuta wawekezaji binafsi kama DP World kwenye bandari zake na miundombinu mingine ya usafirishaji.

Kampuni ya DP World ya Dubai, ambayo ndiyo kitovu cha uchumi cha UAE, mwaka jana ilifanya mazungumzo na Serikali iliyopita ya Rais Uhuru Kenyatta kuhusu uendeshaji wa bandari za Kenya, ikiwemo Mombasa.

Wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Kenya mwaka jana, umoja wa upinzani wa Kenya Kwanza unaoongozwa na Ruto ulipinga mpango wa Rais Kenyatta wa kujadiliana na DP World na kumshutumu kuwa anapanga kuuza bandari.

Lakini baada ya kuingia madarakani, serikali ya Rais Ruto imegeuka na kufufua mpango wa kutaka kukodisha bandari za nchi hiyo kwa wawekezaji binafsi kama DP World ili kuongeza ufanisi.

Wakati Kenya wanachukua hatua za haraka kuvutia uwekezaji kutoka Dubai, nchini Tanzania kumekuwa na mjadala mrefu kuhusu mpango wa kampuni ya DP World kufanya uwekezaji kwenye bandari ya Dar es Salaam.

Licha ya makelele mengi yanayopigwa na viongozi wa upinzani na wanaharakati, uwekezaji binafsi kwenye bandari siyo jambo geni nchini Tanzania.

Kampuni ya TICTS yenye makao makuu Hong Kong, ilipewa mkataba kuendesha eneo la makontena la bandari ya Dar es Salaam kwa zaidi ya miaka 22 chini ya uongozi wa marais Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na John Magufuli.

Mataifa mbalimbali duniani, ikiwemo Marekani, Uingereza, China, Canada, Uholanzi, Korea Kusini, Afrika Kusini, Brazil, Norway, Uswisi, Ujerumani, Ufaransa, India, Uturuki, Australia, Msumbiji, Senegal, Misri na Rwanda yameingia mkataba na DP World kuendesha bandari zao.

Rais Samia Suluhu Hassan ameonya hivi karibuni kuwa iwapo Tanzania haitachukua fursa ya uwekezaji binafsi kwenye bandari ya Dar es Salaam kwa haraka, inaweza kupoteza fursa hiyo na ikachukuliwa na nchi jirani.

Kumekuwa na upotoshaji mkubwa kwenye mjadala wa uwekezaji binafsi katika bandari ya Dar es Salaam, huku baadhi ya wanasiasa wakisambaza uongo kuwa bandari imeuzwa ili kuibua taharuki kwa wananchi.
 
Mkataba wanao saini Kenya sio wa kindezi ndezi Kama huu wa kwenu.
Kumbuka mawaziri wa Kenya Ni wazalendo na wanajua kiingereza halafu wanaa akili.
Kumbuka mkataba wetu mesainiwa na Mbarawa lakini MTU wa upande wa DP hakuandika jina Wala cheo chake halafu sinye kaweka Kama sio yake.
Yaani Mbarawa kasainishwa na jini.
 
Mpumbavu wewe,naona kila siku unaokoteza links na video uchwara za kuwasifia hao mabwana zako waarabu ili kutushawishi tukubaliane na mipango yenu ovu ya kuuza bandari ZETU Watanganyika.
 
Tanzania endeleeni kusikiliza porojo za watu wajinga na wapumbavu ambao hakuna Cha maana wanachangia kwenye uchumi wa Nchi.

Nazidi kuwakumbisha Dunia Inajua pesa Kwa Sasa ziko Kwa Waarabu.

Naona threads za kutosha kuhusu DP world na sifa kedekede! Nakushaur ukileta thread kuhusu Kenya na DP world weka na mkataba wakenya walioingia na DP world ili tuone kama hauna kikomo ama la
 
Adui mkubwa wa mwaafrika ni mwaafrika mwenywe na sio mgeni. Ona upumbavu hapa. Kwani makubaliano ya Kenya na nchi nyingine yanafanana na Tanzania? Na je watz wameshindwa kueendsha na lazima tufanane kama nchi nyingine? Hii nchi bora tungepasula kila mkoa iwe nchi kamili; baadhi ya watu ni hovyo!
 
WAKATI baadhi ya wanasiasa wa upinzani na wanaharakati wakipinga mpango wa kampuni ya DP World ya Dubai kuwekeza kwenye bandari ya Dar es Salaam, Kenya imetangaza maamuzi ya kusaini mikataba ya uwekezaji na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Rais William Ruto ametangaza kupitia akaunti yake ya Twitter leo kuwa amefanya mazungumzo kwenye Ikulu ya Nairobi, Kenya, na Waziri wa Mambo ya Nje wa UAE, Sheikh Shakhboot bin Nahyan Al Nahyan, kujadili fursa za uwekezaji.

"Kenya na Umoja wa Falme za Kiarabu watasaini makubaliano ya uwekezaji ambayo yataimarisha uhusiano kati ya nchi zetu na kutengeneza fursa kwa wananchi wetu," Rais Ruto alisema.

Alisema kuwa makubaliano hayo ya uwekezaji kati ya Kenya na UAE yatajikita kwenye maeneo mbalimbali, ikiwemo miundombinu ya usafirishaji.

Waziri Shakhboot wa UAE pia amefanya ziara kwenye Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kukutana na Rais Felix Tshisekedi kujadiliana kuhusu fursa za uwekezaji.

Zambia pia nayo imekuwa ikifanya jitihada kubwa kuvutia uwekezaji kutoka UAE.

Serikali ya Ruto imeanza jitihada kubwa ya kutafuta wawekezaji binafsi kama DP World kwenye bandari zake na miundombinu mingine ya usafirishaji.

Kampuni ya DP World ya Dubai, ambayo ndiyo kitovu cha uchumi cha UAE, mwaka jana ilifanya mazungumzo na Serikali iliyopita ya Rais Uhuru Kenyatta kuhusu uendeshaji wa bandari za Kenya, ikiwemo Mombasa.

Wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Kenya mwaka jana, umoja wa upinzani wa Kenya Kwanza unaoongozwa na Ruto ulipinga mpango wa Rais Kenyatta wa kujadiliana na DP World na kumshutumu kuwa anapanga kuuza bandari.

Lakini baada ya kuingia madarakani, serikali ya Rais Ruto imegeuka na kufufua mpango wa kutaka kukodisha bandari za nchi hiyo kwa wawekezaji binafsi kama DP World ili kuongeza ufanisi.

Wakati Kenya wanachukua hatua za haraka kuvutia uwekezaji kutoka Dubai, nchini Tanzania kumekuwa na mjadala mrefu kuhusu mpango wa kampuni ya DP World kufanya uwekezaji kwenye bandari ya Dar es Salaam.

Licha ya makelele mengi yanayopigwa na viongozi wa upinzani na wanaharakati, uwekezaji binafsi kwenye bandari siyo jambo geni nchini Tanzania.

Kampuni ya TICTS yenye makao makuu Hong Kong, ilipewa mkataba kuendesha eneo la makontena la bandari ya Dar es Salaam kwa zaidi ya miaka 22 chini ya uongozi wa marais Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na John Magufuli.

Mataifa mbalimbali duniani, ikiwemo Marekani, Uingereza, China, Canada, Uholanzi, Korea Kusini, Afrika Kusini, Brazil, Norway, Uswisi, Ujerumani, Ufaransa, India, Uturuki, Australia, Msumbiji, Senegal, Misri na Rwanda yameingia mkataba na DP World kuendesha bandari zao.

Rais Samia Suluhu Hassan ameonya hivi karibuni kuwa iwapo Tanzania haitachukua fursa ya uwekezaji binafsi kwenye bandari ya Dar es Salaam kwa haraka, inaweza kupoteza fursa hiyo na ikachukuliwa na nchi jirani.

Kumekuwa na upotoshaji mkubwa kwenye mjadala wa uwekezaji binafsi katika bandari ya Dar es Salaam, huku baadhi ya wanasiasa wakisambaza uongo kuwa bandari imeuzwa ili kuibua taharuki kwa wananchi.
Tanzania kanisa na wafanya biashara wezi wanaofanya kazi zao kupitia makanisa ndilo linalopinga.

Hakuna siri, tutazame waliopinga wote ni kanisa na wakristo. Kanisa halijawahi kuwa na nia njema na Tanzania kama nchi, hata wakati watu wanagombea uhuru wa Tanganyika, kanisa lilijitenga na kuwa pamoja na watawala. Walimtenga yeyote aliyekuwa na wagombea uhuru.

Kama hiyo haitoshi? Hivi hatukioni kinachoendelea?
 
Mpumbavu mkubwa wewe ulaaniwe kwa ujambazi wa kuuza Mali za Tanganyika,hayo yote mtalipa tuu
 
Na sasa tunataka MoU ya Serikali na Kanisa ifutwe. Wizi umefanyika kwa miaka mingi tumekaa kimya, sasa hatukubali, tunafunga mianya yote ya wizi wa kanisa.
 
Back
Top Bottom